Ridhiwani na wana wa kanali gaddafi & hosni mubarak | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ridhiwani na wana wa kanali gaddafi & hosni mubarak

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MWananyati, May 2, 2011.

 1. M

  MWananyati Senior Member

  #1
  May 2, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 155
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Ni ukweli usiofichika kuwa watawala wengi wa afrika bado wana kasumba ya uchifu na utemi wa mababu zetu. Suala la kurithishana vyeo na kumiliki mali za umma limekuwa kama jambo la kawaida kabisa ambalo watawala hawa hawashtuki kabisa.

  Suala ambalo lipo hot kwetu ni mabilioni na miradi ya mabilioni ya bwa mdogo ridhiwani. Hakuna haja ya kushangaa kwamba imekuaje huyu dogo ni bilionea saiv. Wengi wa marais huwajengea uwezo watoto wao kupitia uanzishaji wa makampuni mbalimbali ambayo yatakua yanapata tenders mbalimbali za serikali na hivyo kuwawezesha kupata mamilioni ya wavuja jasho. Katika dunia ya leo, hakuna biashara yenye faida kubwa na nono kama ya kufanya na serikal. serikali zenyewe hizi zetu ni hopeless kabisa ndo mana ukiangalia tangu 2003 kumekua na makampuni mengi yanayochipua kama uyoga. wenyewe tunawafahamu.

  Angalia watoto wa gaddaf na mubaraka, wanakula tu nchi na kuiba rasilimali za wananchi wa huko. Hivyo ndivyo RZ1 anavyofanya saivi. mabilioni hayo ni through dirty deals with government offices in the name of presidency.

  SULUHISHO:
  1. KATIBA irekebishe hikama ya uongozi wa nchi ambapo saiv uraisi umekua ni mali ya familia na rafiki zao
  2.RZ1 ajue kuwa siku zinahesabika. Hata wana wa gaddafi na mubarak hawakuijua siku hio, ila ipo siku around the corner. Watanzania si wajinga milele, wanaona, wanaumia, but ONE DAY YES!
   
Loading...