Ridhiwani: Mapambano na Madawa ni kama yameanza

Rais2020

JF-Expert Member
Jul 14, 2016
3,248
5,537
Ni mwendelezo wa kupambana na MADAWA ya kulevya, ndugu Ridhiwani kikwete ameunga juhudi zinazofanywa na Paul makonda kutokomeza biashara haramu ya MADAWA ya kulevya. Ni wakati sasa wabunge wakaiga mfano wa huyu mbunge katika vita ya madawa ya kulevya. Pongezi kwako mheshimiwa kwa kuunga mkono juhudi Kali ya kupinga mihadarati

Jukumu la kutokomeza biashara hii ni la watanzania wote.
d14e1062c51e299f4e7806e18f8a6cdc.jpg

Je, Ridhiwani ni kweli anaunga mkono au anajisafisha tu kutokana na kutajwa kwake mara kwa mara kwenye madawa ya kulevya?.

Tujadili pamoja. Karibu

==================================================
Alichosema Ridhiwani 15/02/2017 wakati akihojiwa na East Africa Redio
==================================================
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete, atoa pongezi za dhati kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kwa kuanzisha vita dhidi ya madawa ya kulevya na kutaka wahusika wachukuliwe hatua.

Akiongea Jumatano hii katika kipindi East Africa Breakfast cha EA Radio, Ridhiwani ameishauri serikali kuifikisha mwisho vita hiyo, ili kulimaliza kabisa tatizo hilo kwa kuwa limepoteza vijana wengi wenye uwezo mkubwa na mchango katika taifa.

Ameeleza kinagaubaga, vita dhidi ya madawa ya kulevya ni agenda ya Taifa nzima, ijapokuwa mwisho wake ni mgumu kwani hata ukiangalia nchi zilizo endelea kiuchumi kama Marekani bado zinapambana na vita hii takribani miaka 80 sasa.

“Kwanza nataka kusema hii vita ni jambo jema sana, unajua jamii yetu hasa hasa kama hayajakukuta kwenye familia yako huwezi kuelewa ukubwa wa tatizo na madhara yake, Kwa mfano mimi katika maeneo ambayo naishi, kuna watu ambao walikuwa katika umri wetu tumewapoteza, kwa mmfano vijana kama akina Langa wale, tumejaribu kuwasaidia mpaka ikaonekana hakuna njia ambayo unaweza ukawasaidia tena, sisi kwetu tunaumia kwa kuona hawa vijana walikuwa na future nzuri sana”. amesema Ridhiwani Kikwete.

Amewaomba watanzania kutoa ushirikiano wa dhati kwa timu iliyoundwa ya kutokomeza madawa ya kulevya kwani anaamini kupitia ushiriakiano huo Sianga na timu yake itafanya vizuri katika vita hii.

”Bwana Sianga ambaye kwangu mimi ni mtu ambaye nikisoma CV yake ni mtu mzuri sana na makini, ni mmoja kati ya Watanzania wachache ambao walipata nafasi ya kwenda kusomea madawa ya kulevya”.

Pia Mbunge uyo alimshukuru Mkuu wa mkoa kwa kukabidhisha majina yale, anaamini kabisa uchunguzi wa kina utafanyika, kwa watakao kutwa na hatia iliongezea washughulikiwe ili jamii yetu iwe salama.
 
Umaskin na mawazo potofu unakuchanganya...
Usimsee mtu kama huna sababu maalum za kumshutumu na ushahid wa kujiridhisha..hata kama ungelikuwa bi weqe sidhan kama ungefurahia

Bora wewe mwenye mawazo elevu,

Kwan hao waliotajwa kuna ushahid wa kujiridhisha.
 
Umaskin na mawazo potofu unakuchanganya...
Usimsee mtu kama huna sababu maalum za kumshutumu na ushahid wa kujiridhisha..hata kama ungelikuwa bi weqe sidhan kama ungefurahia
Sasa si watuhumiwa wanatajwa?Yeye kamtaja Ridhione kikwete kuwa ni dealer,hayo ndio mapambano yenyewe!
 
Ni mwendelezo wa kupambana na MADAWA ya kulevya, ndugu Ridhiwani kikwete ameunga juhudi zinazofanywa na Paul makonda kutokomeza biashara haramu ya MADAWA ya kulevya. Ni wakati sasa wabunge wakaiga mfano wa huyu mbunge katika vita ya madawa ya kulevya. Pongezi kwako mheshimiwa kwa kuunga mkono juhudi Kali ya kupinga mihadarati

Jukumu la kutokomeza biashara hii ni la watanzania wote.
d14e1062c51e299f4e7806e18f8a6cdc.jpg

Je, Ridhiwani ni kweli anaunga mkono au anajisafisha tu kutokana na kutajwa kwake mara kwa mara kwenye madawa ya kulevya?.
54a31e1fb5eaf640d6eb4f00cb024f15.jpg
.
Tujadiri pamoja. Karibu
Tafadhali. Matumizi ya maneo "ra" na "la" yazingatiwe. Sio tujadiri pamoja ni tujadili pamoja. Anza upya
 
Riz1 mmekua mkimuhusisha na kila kitu kibaya na kizur chenye pesa nyingi mara Lake oil,Madawa ya kulevya,Gsm .nk,lakn tukumbuke kuwa hyo yote ni hear say just a street talks labda nikuulize wewe kama wewe je una ushahid wowote wa kumuhusisha na madawa ya kulevya? Kumtuhum mtu ni1 lakn kuthibitisha pas na shaka ndio kitu cha msingi kabisa,Acha arud Dodoma kwanza tuendelee ns series ya Mwanza Boy...!
 
Tafadhali. Matumizi ya maneo "ra" na "la" yazingatiwe. Sio tujadiri pamoja ni tujadili pamoja. Anza upya
Asante mkuu kwa marekebisho. Si unajua tena wakurya *r* na *l* ni shida kidogo
 
Kumpongeza kwake ni kujipendekeza ili asitajwe maana nayeye kwenye msafala huo yumo, ni suala la muda kila kitu kitabaki hadharani
 
Back
Top Bottom