Ridhiwani Kikwete: Mradi wa uwekaji vigingi ni sehemu ya Uimarishaji wa mipaka ya Tanzania

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,798
21,369
Serengeti. Serikali ya Tanzania na Kenya zimekamilisha uwekaji vigingi katika mpaka unaoigawa Tanzania na Nchi ya Kenya katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti na hivyo kufanikiwa kumaliza mgogoro wa mpaka uliokuwepo hususani katika sekta ya utalii kati ya nchi zote mbili.

Akizungumza baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maliasili na Utalii kufanya ziara kukagua utekelezaji wa mradi huo katika hifadhi hiyo, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ridhiwani Kikwete amesema kuwa mradi huo ni sehemu ya mradi wa uimarishaji wa mipaka kati ya Tanzania.

Amesema kuwa katika bajeti ya mwaka 2021/22 Serikali ilitenga zaidi ya Sh 5.7 bilioni kwaajili uimarishaji wa mipaka kati Tanzania na Kenya lengo likiwa ni pamoja na kuimarisha na kukuza mahusiano na kuondoa migogoro isiyokuwa ya lazima kati ya nchi zote mbili.

Ridhiwani amesema uwekaji vigingi katika mpaka huo wenye zaidi ya Kilomita 60 utaiwezesha Serikali kuimarisha ulinzi ndani ya mipaka ya hifadhi hiyo kwa usalama wa hifadhi na nchi kwa ujumla sambamna na mapato yatokanayo na hifadhi hiyo.

Amefafanua kuwa hivi sasa vigingi hivyo vimewekwa kwa umbali wa mita 250 tofauti na zamani ambapo vilikuwa na umbali wa zaidi ya mita 500 hali ambayo ilikuwa ikichanganya watu na kusjindwa kutambua mpaka halisi ni upi.

‘’Katika kipindi cha mwaka mmoja Serikali ya Rais Samia na ile ya Kenya ziliweza kuingia katika makubaliano ambayo matokeo yake yamewezesha kutatua sintofahamu ya mipaka iliyokuwepo katika mpaka ndani ya hifadhi ya Serengeti na kuleta heshima kubwa kwa nchi zote mbili.

Naibu Waziri huyo amesema kuwa uimarishaji wa mipaka utaendelea kati ya mipaka ya nchi nyingine jirani ikiwemo Uganda, Malawi na Kongo ikihusisha mupaka ya majini na nchi kavu.

Naibu Waziri wa Utalii, Mary Masanja amesema kuwa awali kulikuwa na changamoto ya utambuzi wa mipaka hivyo uwekaji wa vigingi utakuwa na manufaa zaidi kwa wizara yake.

"Kwasababu ilikuwa ni vigumu kutambua mipaka katika eneo hili kulikuwa na tabia ya watu kuingia hadi huku kwetu na sababu ikiwa ni mipaka kutokuoneka kwahiyo hapa sasa hakuna atakayeingia huku kwetu bila kufuata taratibu" amesema

Kwa upande wake Mwanyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Ally Makoa amewaagiza watendaji wa Wizara kuhakikisha wanatekeleza kazi hiyo na kuharakisha uweka vingingi katika mpaka, ili kuondokana na adha iliyopo katika utambuzi wa mipaka inayoigawa Tanzania na chi jilani.

“kazi hii iliyofanyika ni kazi nzuri sana na tunatamani sasa maeneo yetu yote yaliyohifadhiwa yawe na vigingi vya mipaka vinayoonekana kwa malengo yaleyale tuliyoyafanya hapa katika maeneo yote ya nje na ndani ya nchi kuwe na vigingi vivyoonekana ili pasiwe na uvamizi” amesema Makoa

Amesema kuwa anaamini kuwa wizara ya ardhi itaendelea kutekeleza maelekezo ya Serikali na yale ya kibajeti na kutoa kipaumbele katika utatuzi wa migogoro baina ya Nchi jirani kwa kuweka vingingi katika mipaka ambavyo awali viliwekwa na wakoloni katika umbali mrefu na kusababisha sintofahamu katika baadhi ya maeneo.

Source;? Gazeti la mwananchi
 
Back
Top Bottom