Ridhiwani Kikwete mdaiwa sugu bodi ya mikopo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ridhiwani Kikwete mdaiwa sugu bodi ya mikopo?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by nngu007, Feb 14, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Feb 14, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  [h=1][/h]

  [​IMG]
  Na Mwandishi wetu - Imechapwa 01 February 2012

  [​IMG][​IMG]
  WATOTO wawili wa Rais Jakaya Kikwete ni miongoni mwa wahitimu wa vyuo vikuu waliotangazwa kama wadaiwa sugu wa mkopo wa elimu ya juu uliotolewa vipindi tofauti kati ya mwaka 1994 na 2009 katika vyuo mbalimbali nchini.


  Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) wiki iliyopita ilitangaza majina ya wadaiwa sugu kwenye tovuti yake www.heslb.go.tz baada ya kuona wengi wa waliokopeshwa hawajarejesha hata shilingi.

  Kulingana na taarifa yake, Bodi imeagiza wadaiwa hao wanaokadiriwa kufikia 80,000 wajisalimishe ndani ya siku 21, si hivyo watachukuliwa hatua za kisheria, ikiwamo kuwazuia kusafiri nje ya nchi.


  Watoto wa Rais Kikwete ambao majina yao yamekutwa katika tovuti ya bodi hiyo ni Ridhiwan J. Kikwete aliyehitimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Salama Kikwete aliyehitimu katika Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba Muhimbili (MUHACS).


  Inasemekana Salama ni mke wa Ridhiwan.


  Mbali na hao, orodha ya wadaiwa sugu inaonesha wamo watoto wengine wa wanasiasa mbalimbali, wanasiasa wenyewe pamoja na watoto wa viongozi waandamizi serikalini wakiwemo waliokwishastaafu kazi katika utumishi wa umma.


  Wengine wanaosakwa na bodi hiyo ambao majina yao yamehusishwa na majina ya wanasiasa au watumishi maarufu wa umma, ni Alfred J. Nchimbi anayedhaniwa kuwa kaka wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Emmanuel Nchimbi na Anna Rajab Kiravu anayehusishwa na Rajab Kiravu, aliyestaafu kuwa Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi (NEC).


  Wadaiwa wengine wa mikopo ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ni Mbunge wa Viti Maalumu (CHADEMA), Christina Lissu na Afisa Mwandamizi Idara ya Sera na Utafiti wa Chama hicho, Mwikwabe Mwita.


  Katika orodha hiyo pia yamo majina ya Raphael Augustine Mrema anayehusishwa na Augustine Mrema ambaye ni mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP) na Charles J. Warioba anayehusishwa na Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba.


  Pia wameonekana Baraka Hamis Msumi anayedhaniwa ni mtoto wa aliyekuwa Jaji Kiongozi, Hamis Msumi ambaye ameshastaafu, na Judith D. Mwakyusa ambaye anadhaniwa kutoka familia ya Profesa David Mwakyusa aliyekuwa Waziri wa Afya kipindi kilichopita na mbunge wa Rungwe Magharibi.


  Kampuni nne za udalali, Msolopa Investment Co. Ltd, Nakara Auction Mart na Sikonge International Co. Ltd ya Dar es Salaam na nyingine ya Dodoma Universal Trading Co. Ltd ya mkoani Dodoma zimepewa jukumu la kuwasaka wadaiwa hao.


  Wengi wa wahitimu wanaodaiwa na bodi hiyo walisoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).


  Kwa mujibu wa taarifa, wadaiwa hao wanatakiwa kuwasilisha bodi maelezo yao kuhusu mahali waliposoma, mwaka wa masomo, namba za simu na mahali wanakopatikana kwa sasa.


  Baada ya muda waliopewa kumalizika, wadaiwa watalazimika kuongezewa riba ya asilimia 5 kila mwaka, gharama za kuwatafuta, majina yao yatatumwa kwenye taasisi za fedha ili kuwazuia wasipate mkopo wa aina yoyote.


  Wadaiwa hao pia watazuiwa kupata ufadhili wa masomo ya juu ndani na nje ya nchi na taarifa zao zitawasilishwa Idara ya Uhamiaji na balozi zote ili wasiruhusiwe kusafiri nchi yoyote nje.   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Feb 14, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Haya PRINCE amekuwa kama watoto wa Gadaffi na Saddam Hussein... inatisha...
   
 3. k

  kulwa12 Senior Member

  #3
  Feb 14, 2012
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sasa hii inamantiki gani mkuu??
   
 4. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #4
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kwa hao bodi hawajui kazi ya Riziwani mpaka wasbindwe kumkata hayo makato?
   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hapa tu nimechoka kuendelea kusoma taarifa hii.. Salama ni mtoto wa Kikwete sio mke wa Ridhiwan
   
 6. K

  Keil JF-Expert Member

  #6
  Feb 14, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135

  Waandishi wa Bongo wakati mwingine mnatia kichefuchefu, juu mwandishi anasema Salama Kikwete ni mtoto wa Kikwete. Then from no where anaongeza, "Inasemekana Salama ni mke wa Ridhiwan"! Hapa sioni tofauti ya Mwandishi wa Mwanahalisi na mwandishi wa magazeti ya udaku yaliyojaa waandishi kanjanja wanaoganga njaa ili mkono uende kinywani.

  Wakati mwingine waandishi huwa mnajitakia kesi za bure, huyo dada akiamua kuwashitaki kwa kumdhalilisha/kumzushia kwamba ameolewa na kaka yake mtajitetea kwa lipi?

  Salama ni binti wa JK, hata graduation yake wazazi wake walihudhuria na wala si miaka mingi iliyopita. Mke wa Ridhiwan, sikumbuki jina lake lakini for sure najua ni mwanasheria.

  Simple question ilikuwa ni kwamba, je wakati huyo Salama [anayesemekana ni mke wa Ridhiwan] akisoma Muhimbili alikuwa kaishaolewa tayari kiasi kwamba alibadilisha jina na kuitwa Salama Kikwete?

  Maadili ya uandishi yanataka mwandishi kuwasiliana na mhusika kabla ya kutoa habari hiyo ili iwe verified.
   
 7. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #7
  Feb 14, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Jamaa wazishi...mi nshamaliza kulipa ila wamenitoa
   
 8. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #8
  Feb 14, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  salama ni mke wa ridhiwan!!!!?? Wanamsema huyu aliyepata sponsorship ya kwenda uk na watoto wa maskini kunyimwa,au macho yangu na memory yangu vimeanza mgomo?
   
 9. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #9
  Feb 14, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Ni nani Mkweli? Waandishi wetu au Serikali inayoficha Ukweli?
   
 10. m

  mbongopopo JF-Expert Member

  #10
  Feb 14, 2012
  Joined: Jan 24, 2008
  Messages: 1,112
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  umeandika pumba
   
 11. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #11
  Feb 14, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  umesahau kuwa wakati wa mgomo wa drs walikuwa wanaripoti kuwa hali ni shwali na watu wanakatika
   
 12. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #12
  Feb 14, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,465
  Likes Received: 19,841
  Trophy Points: 280
  -waanddishi wetu kama walipata div sawa na ile ya mwanaisha mnategemea nini sasa?
   
 13. KASHOROBANA

  KASHOROBANA JF-Expert Member

  #13
  Feb 14, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,249
  Likes Received: 406
  Trophy Points: 180
  mna maanisha uyu riz1 trilionea toto wa mkuu wa kaya? kama kweli atakuwa amesahau kuwa ana vijiden pia uko tirdo (HESLB)
   
 14. K

  Keil JF-Expert Member

  #14
  Feb 14, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ni jukumu la mwandishi kufanya udadisi ili aweze kupata ukweli wa habari yenyewe. Tatizo la waandishi wetu wengi ni kwamba sio wadadisi, na ndio maana wengi wao huwa wanaishia kupokea Press Release pale Idara ya Habari Maelezo na kwenda kui-reproduce kama ilivyo wenye gazeti.
   
 15. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #15
  Feb 14, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Huu uandishi ni hatari! Hata hivyo waliokopeshwa walipe madeni yao ili na wengine wakopeshwe.
   
 16. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #16
  Feb 14, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,106
  Likes Received: 7,363
  Trophy Points: 280
  Mahakamani Silipi,
  Na Mkopo Siendi!!!
   
 17. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #17
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Ni kumwonea Rais, mtoto akishafikiza utu uzima na kazi yake anawajibika mwenyewe kwa taifa lake. Hakuna kipengere kwenye fomu za mikopo kinachosema baba wa mtoto ndiye atadaiwa. Le us be fair.

  Mimi naona hapa Ridhwan Kikwete kamwaibisha baba yake ambaye ni mkuu wa nchi. Hakika naamini Jk alikuwa hajui hili pengine akisikia atapigwa butwaa kama nasi tufanywavyo. Bila shaka atawaelekeza watoto kwenda mara moja kusawazisha hali hiyo.

  Tatizo kubwa la bodi ya mikopo haitoi hati yoyote ya madai kwa wanafunzi wa vyuo vikuu wanapomaliza masomo. Hakuna anayejua anadaiwa pesa ngapi na kwa mchanganuo upi. Ni wizi mtupu. Na wao wana sehemu ya kulaumiwa. mfumo wao wa kukusanya madeni na kuwajibisha wasiolipa ndio chanzo cha madeni ya miaka nenda rudi. wameshindwa kukusanya madeni tangu 1994 karibu miaka 20 ndipo kwa mara ya kwanza wametangaza majina. Kama wangekuwa na utaratibu huo tangu awali wengi wangeogopa kuchafuka. lakini pia kwa nini wanatumia website yao tu badala ya kutangaza majina hayo pia kwenye magazeti?
   
 18. p

  papito Member

  #18
  Feb 14, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Huu ni utumbo mtupu!
   
 19. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #19
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Uzito wa fedha ambayo hajalipa RIZ na salama kikwete sioni tofauti na uzito wa fedha ya mtoto wa mkulima, zote zina athari kwa maendeleo ya elimu nchini.

  Ni vema tukaelekeza nguvu kubwa kuwaambia wote wanaodaiwa wakalipe wengine wapo hata hapa JF wanajitahidi kupindisha mada ili mzigo wa lawama abebe Riz na salama peke yao.

  wajibikeni kalipeni acha ukanjanja wenu. mafisadi wa elimu wote wakubwa mnaturudisha nyuma.
   
 20. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #20
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0

  Tatizo lako unaleta siasa za chadema na CCM kwenye mambo ya uwajibikaji? ndio suala hili linamtia doa rais lakini huwezi kuondoa ukweli kwamba Riz na salama kikwete ni watu wazima wanaofanya kazi ni wajibu wao kumkinga Rais na kashfa zao.
  Kama Riz anapitaga humu JF ni budi asijione hana kosa bali baba yake.
   
Loading...