Ridhiwani Kikwete katika kashfa nzito Chalinze

Huu sasa ndo unafiki
Njoo na issue nyingine aise mimi siamini kabisa kama dogo ana njaa kali kiasi hiki
ACHA KUMWONEA BANA
Sio suala la kutoamini. Mimi nipo Chalinze, hii ndio fact. Kama unaweza njoo mamlaka ya maji hapa Wami uone watakachokuambia
 
Mtoa mada kasema Ridhiwani amekula pesa za kufanikisha upatikanaji wa maji! Mbona mnakwepesha mada!

Kwakuwa hizo hela alipewa ridhiwani akawagawie wahusika wa maji.

Tatizo la maji lipo lakini khs kula hela hapo nasita kukubali japo hicho chama na huyo mbunge siwafagilii kabisa ila ni ngumu kumeza kuwa amekula hizo pesa.
 
IKWETE

Naomba ufafanuzi; ilikuwaje fedha kwa ajili ya mradi wa maji zikafika kwa Ridhiwani na wapambe wake?
 
Last edited by a moderator:
Waache wakazi wa Chalinze wale matunda ya kura zao. Kwani hawakujua udhaifu wa baba yake? Jimbo la Chalinze lina shida ya maji tangu baba yake mtoto akiwa mbunge sasa wamemchagua mtoto.

Kwani hawakujua kuwa nyoka hawezi kuzaa nge? Nyoka atazaa nyoka tu. Kwa hiyo wakazi wa Chalinze watulie tuli kama wananyolewa sehemu mpaka miaka mitano mingine iishe.
 
Hata RIZ-1 akila anavyotaka, ni haki yake, ni mtoto wa Panya mkuu na kwa historia, mapanya yote ni majizi...haijalishi yanakulaje, yamepataje mlo, au vinginevyo...yanaiba na kula tu...

Chalinze, HIYO NDIYO KURA YENU KWA WEZI NA MATOKEO YAKE, SHANGILIENI BADALA YA KULIA LIA...na bado!
 
Imekuuma sana we mpambe wa mbunge...

Mimi sio mpambe wa Mbunge, na ninawachukia sana hawa ma-CCM, ila jamani hata kama ni chuki zetu, kuna mambo ya kuyajadili. Tena wakati mwingine tuwe pia tunaangalia hata na akili za waleta mada humu jamvini.

Kwa akili yako, kuna mbunge yoyote kwa sheria za nchi hii anaweza ku-access ela za miradi, isipokuwa ela za mfuko wa jimbo tu. Inaingiaje akilini mbunge ale mil. 450? Huu mwingine sasa ndio unaitwa unafiki wa jirani wa kina - Mcharo
 
Naomba ufafanuzi; ilikuwaje fedha kwa ajili ya mradi wa maji zikafika kwa Ridhiwani na wapambe wake?
Mkuu mimi pia ninaishi Chalinze ingawa nina muda kidogo sijatokea pale. Ni kuwa Ridhiwani ame-influence kuzipata hizo hela kupitia kwa wapambe wake ambao ni wajumbe kwenye bodi ya mamlaka ya maji Chalinze.

Wakazi wa Chalinze wanamlaumu Ridhiwani
 
Mkoa wa pwani kwa ujumla wake una shida kubwa sana ya maji;
chama kitakachokuja na sera ya kuwapatia watu maji hakika kitapita.

Inashangaza sana MTO wami na ruvu unapita pwani lakini wananchi hawana maji, bonde la ruvu pamoja na rutuba yote hawalimi kilimo cha Mpunga cha kisasa , cha ajabu zaidi ni kwamba posta na kariakoo ni nadra sana maji kukatika lakini kimara yanapopita hayo maji watu wanataabika sana
 
Tafuteni ukweli ndiyo mlete post sahihi ndiyo tuchangie. Inawezekana kuna ukweli lakini mleta mada ameshindwa kuwakilisha vizuri!
 
Mkuu mimi pia ninaishi Chalinze ingawa nina muda kidogo sijatokea pale. Ni kuwa Ridhiwani ame-influence kuzipata hizo hela kupitia kwa wapambe wake ambao ni wajumbe kwenye bodi ya mamlaka ya maji Chalinze.

Wakazi wa Chalinze wanamlaumu Ridhiwani
Kama hicho ndicho kiolichotokea, kwa nini maisanze kuwalaumu hao wajumbe wa Bodi ambao walikubali kutoa fedha na kumpatia mtu miwngine kinygumke na matumizi yaliyoidhinishwa?
 
uongo namna hii ni heri uvae sketi tu tujue moja kuliko shida unazopata kujipitishapitisha
 
Back
Top Bottom