GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,427
- 108,531
Akizungumza katika uzinduzi wa Visima katika Kijiji cha ' Matwipiri ' huko Chalinze Mbunge wa Chalinze na Mtoto wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Ridhiwani Kikwete alitoa ' kauli ' ambayo iliambatana na ' mwonekano ' wa ' hasira ' kutoka kwake kana kwamba ile siku ya jana alikuwa anaisubiri kwa ' hamu ' mno ili aweze kutema ' nyongo ' yake pengine aliyokuwa nayo muda mrefu.
Alipopewa tu nafasi ya kuzungumza kama Mbunge wa eneo husika Ridhiwani Kikwete alisema maneno haya huku akiwa ' amefura ' kabisa na namnukuu bila kuongeza au kupunguza chochote " nyie Viongozi wa Serikali tunaomba msije hapa na mikodi yenu ya ajabu ajabu na ya kukomoana katika hii miradi inayoendelea katika Jimbo hili kwani miradi hii inalenga kuwakomboa hawa Wananchi wenye shida ", mwisho wa kumnukuu.
Ukitulia sana na kuifanyia tafakuri tunduizi ( critical thinking ) hii kauli ya Mheshimiwa Mbunge Ridhiwani Kikwete unaweza kupata ' picha ' nyingi ' tata ' na yawezekana ile ' kauli ' alikuwa anamlenga Mtu fulani ambaye pengine ana ' hasira ' nae pengine kutokana na sababu zake anazozijua.
Naomba kuwasilisha.