Ridhiwani Kikwete, hasira zako za jana ulikuwa unazielekeza kwa nani hasa?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,363
108,403
Akizungumza katika uzinduzi wa Visima katika Kijiji cha ' Matwipiri ' huko Chalinze Mbunge wa Chalinze na Mtoto wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Ridhiwani Kikwete alitoa ' kauli ' ambayo iliambatana na ' mwonekano ' wa ' hasira ' kutoka kwake kana kwamba ile siku ya jana alikuwa anaisubiri kwa ' hamu ' mno ili aweze kutema ' nyongo ' yake pengine aliyokuwa nayo muda mrefu.

Alipopewa tu nafasi ya kuzungumza kama Mbunge wa eneo husika Ridhiwani Kikwete alisema maneno haya huku akiwa ' amefura ' kabisa na namnukuu bila kuongeza au kupunguza chochote " nyie Viongozi wa Serikali tunaomba msije hapa na mikodi yenu ya ajabu ajabu na ya kukomoana katika hii miradi inayoendelea katika Jimbo hili kwani miradi hii inalenga kuwakomboa hawa Wananchi wenye shida ", mwisho wa kumnukuu.

Ukitulia sana na kuifanyia tafakuri tunduizi ( critical thinking ) hii kauli ya Mheshimiwa Mbunge Ridhiwani Kikwete unaweza kupata ' picha ' nyingi ' tata ' na yawezekana ile ' kauli ' alikuwa anamlenga Mtu fulani ambaye pengine ana ' hasira ' nae pengine kutokana na sababu zake anazozijua.

Naomba kuwasilisha.
 
Sasa hilo si ovyo la kawaida tu.. ukitaka aongee kama anaimba taarabu..!?
 
Anabahati coz mshua wake alikuwa mkulu aombe tu mshua wake aendelee kuishi hasa kipindi hiki cha mzee pumba maharagwe adhawaizi angeshakamulia since day 10
 
Anabahati coz mshua wake alikuwa mkulu aombe tu mshua wake aendelee kuishi hasa kipindi hiki cha mzee pumba maharagwe adhawaizi angeshakamulia since day 10

Mkuu unaonekana kama vile kuna mengi ya huyo ' Kijana ' unayajua hebu ' funguka ' basi kwa ' kutiririka ' zaidi ili nasi tusiojua nini kinaendelea tuweze kufahamu hayo yaliyojificha.
 
Kodi lazma ilipwe,wakwere ndo nani wasikipe nani awalipie?
Wao wakae chini ya minazi siku nzima kucheza bao sisi huku tunafia mashambani alafu tuwalipie sisi ,eboo!

Magufuli raisi wangu japo sikukupa kura naomba sana uanzie kupeleka maafisa wa TRA jimbo la Chalinze
 
Back
Top Bottom