Elections 2010 Ridhiwani Kikwete Avunja Makundi Iringa Na Kumpatanisha David Mwakelebela na Monica

chibingo

Member
Feb 7, 2009
46
8
Hii imekaaje wana JF, Kweli Mwakalebela ana furaha au basi tu kakubali yaishe.

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM)Taifa, Ridhiwani Kikwete ,amewakutanisha Monica Mbega na Davidi Mwakalebela baada ya kuwapatanisha na kuvunja makundi katika kikao cha Baraza la Vijana mjini Iringa jana.
Monica ni mgombea ubunge Jimbo la Iringa mjini na Mwakalebela alienguliwa kuwania nafasi hiyo
 
Attachments

  • IMG_5767.JPG
    IMG_5767.JPG
    18.6 KB · Views: 101
Kuvinja kikundi ni suala jingine na kunyimwa wana-Iringa mgombea wao ni suala lingine. Jee, anaweza Riz-One kuwashawishi wana-Iringa kumchagua mtu wasiyempenda, pamoja na kumpa Mwakalebela ahadi ya U-DC kutoka kwa dingi wake? Tusubiri Oct 31. CCM ni chama cha ajabu kweli kweli!!!!!
 
Huyu Dogo hana kazi za kufanya au anafikiri Tanzania ni mali ya familia ya Baba yake.
 
Tatizo moja ni kuwa hata hao wanaoonekana kununuliwa na kutumia professional zao wanachofanya hakiingi akilini mwa watu wazima!! Sasa kama babake alipita, kuna logic gani ya kuuhadaa umma ati huyu ndiye kavunja hayo makundi, propaganda hizi ili muendelee kuimiza nchi si nzuri hata kidogo. Sasa hao walionunuliwa wanajitahidi kweli, walau wangejitahidi kumuelimisha babake, maana kinachofanyika sasa ni utoto na sidhani sie wote tungali wachanga na wasio na uwezo wa kufikiri kama wao!
 
RIZ One, makundi hayavunjiki kihivyo. Wala makundi hatayavunji Mwakalebela, bali makundi huvunjwa na watu wenyewe mioyoni mwao wakiridhika sababu zilizosababisha kuwepo kwa makundi.

Nakuhakikishia kuwa makundi bado yapo. Na baba yako piga, ua, hatarudi tena ikulu baada ya 31.10. UDC ni danganya toto tu kwa Mwakalebela. Maana watu wa Iringa wanaitaji mwakilishi wao katika bunge la Jamhuri na si DC. Subiri uje uone mafuriko.
 
siasa ni unafiki... akiondoka watu wanapenda m=na majungu

fuatilieni dodoma, buchosa, magu, nyamagana, ilala, kigamboni, nk

Riz is just being used
 
Ridhwani ccm wenyewe wanamng'ong'a, wanambeza, ndio maana hata kule Mbozi wale jamaa walimwambia ukweli, hawezi kuwapatanisha kwa kua hawahitaji kura za wanaCCM wasio waunga mkono, walikataa unafiki.
kijamaa ni kama hakijasoma, kuutwa na kujilambalamba na babake.
 
He is just a goat (cricket). Ukiangalia kwa makini picha ya Mwakalebela utaona kabisa amejaa uzandiki usoni. Anaonekana ametabasamu lkn moyoni si hivyo. Anajua kuwa aikibisha kuvunja makundi hakimu atamshughulikia. Sasa afanyeje? Ni kukubali yaishe kjwani jela kubaya. Mimi nauhaakika wa asilimia 100, kuwa Monica Mbega hawezi kushinda Iringa. Chadema washajichukulia jimbo lao. Ridh-One unatumia vibaya pesa za walipa kodi. Unazurula nchi nzima kwa pesa zetu.
 
Hivi haya makundi si tuliambiwa yalishaisha? yalirudi tena? mbona mnatuchanganya watoto wa wenzenu?
Huyo kijana kama hana kazi za kufanya huko anakozurura si atulie tu home? hivi kwani hajaajiriwa? na ofisini kwake anafanya kazi lini? kwa kweli mimi sasa ananikalia shingoni
 
Hii imekaaje wana JF, Kweli Mwakalebela ana furaha au basi tu kakubali yaishe.

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM)Taifa, Ridhiwani Kikwete ,amewakutanisha Monica Mbega na Davidi Mwakalebela baada ya kuwapatanisha na kuvunja makundi katika kikao cha Baraza la Vijana mjini Iringa jana.
Monica ni mgombea ubunge Jimbo la Iringa mjini na Mwakalebela alienguliwa kuwania nafasi hiyo

Ni kama anasema: Nawapatanisha ninyi ili makundi yenu yampigie kura baba na wala si kwa faida yenu wala ya chama changu.
 
Hii imekaaje wana JF, Kweli Mwakalebela ana furaha au basi tu kakubali yaishe.

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM)Taifa, Ridhiwani Kikwete ,amewakutanisha Monica Mbega na Davidi Mwakalebela baada ya kuwapatanisha na kuvunja makundi katika kikao cha Baraza la Vijana mjini Iringa jana.
Monica ni mgombea ubunge Jimbo la Iringa mjini na Mwakalebela alienguliwa kuwania nafasi hiyo

Mhh.. kuwapatanisha huko kuna walakini, leo katika uchambuzi wa magazeti nimesikia kwamba Ridhiwani na Mwakalebera imebidi watimue mbio kukwepa mkongoto wa kina 'kamwene' wasio kubali upuuzi na uzandiki huu!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom