Ridhiwani Kikwete atawazwa kuwa chifu wa wanyakyusa!

Hivi hiyo Kamati ya utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM)Taifa ina wajumbe wangapi na hao ni kina nani na wanafanya nini wakati huu wa kampeni?

Hapa kuna neno!!
Laiti jibu la swali likipatikana litatupeleka kwenye maswali mengine hata kuweza kuuona upande wapili wa pazia kwa uwazi kana kamba pazia halipo.
 
Wanayakyusa kwa kujipendekeza wamezidi! Hakuna wazee huko walau wenye Busara?

Sio Wanyakyusa hao wazee na wala sio machifu. Hilo jina la huyo so called chief halijawahi kusikika katika koo za kichifu ni utapeli wa hali ya juu mno.
 
tumeshaona wengi tu wakitawazwa kwa makabila mbalimbali, sioni kama ni issue... its ceremonial

na upumbavu wa hali ya juu. Huwezi kuwa chifu wa kabila fulani ilhali wewe si kabila hilo. Uchifu una issues zinazoambatana na chimbuko na mila za kabila husika. Ndiyo maana hata wakwere hawajampa hata Jakaya uchifu wa kabila lao. Kuna mambo mazito kwenye cheo hicho na ndiyo maana makabila mengi yanaogopa kuwa na cheo hicho. Huyo anayejiita chifu wa kinyakyusa yumkini ubongo wake ni matope matupu kama ridhiwani kwani huwezi kumpa mtu uchifu kirahisirahisi ambaye hatokani na ukoo wa kichifu wa kabila husika.
 
Kaazi kwelikweli.. Kikwete na familia yake tutawatambua wazd... Mara mama salma kikwete, mara riz1.. Ezi za akina Mkapa hata sikubahatika kulifahamu jina la mwanae hata mmoja, Mwinyi pamoja na uruksa wake naye sikumfahamu mwanae japo kwa jina... Kweli Tz imepata raisi... Uswazi mtupu...
 
Tanzania, Tanzania, nchi iliyo na watu wanaougua ugonjwa wa woga kwa viongozi kunakoambatana na kujipendekeza kulikopitiliza. Mnafikiri hao waliompa uchifu ukiwauliza sababu ya kumpatia uchifu watakuwa na jibu...!!..?? Ni obvious kuwa huko ni kujipendekeza kwa familia ya Kikwete ili wapate shibe katika mantiki ya hela, kupelekewa vitenge / kanga, T-Shirt, na kutembelewa mara kwa mara na viongozi wa juu.

My Tanzania, jamani, kwa nini wananchi wako hawafunguki akili na kutambua mema na mabaya..!!..?? Kwa nini wananchi wako hawajui kutengenisha pumba na mahindi..?? Kwa nini wananchi wako wanashangilia wasichokijua (fuata mkumbo)..?? Kwa nini wananchi wako wananunulika kirahisi kwa pesa za karanga...???

Uchifu unaweza ukatolewa kwa mtu ambaye si wa kabila hilo au ukoo huo endapo ni kiongozi maalumu wa serikali kama vile Waziri Mkuu, Rais, Makamu wa Rais. Mimi sioni unless siku hizi wana -refer kwa kusema Waziri Mkuu & Family, Rais & Family, Makamu wa Rais & Family kwenye kila rights za uongozi wa nchi. Nasikia siku hizi hadi watoto wa JK wanawakimbiza wakuu wa mikoa...!!! Kweli nchi hii.....!!! Tutakoma mwaka huu...!!
 
Kwa kweli inasikitisha sana kuona jinsi jamii za kitanzania zinavyopoteza Mila zao,
hadi kufikia kama hapa tunavyoona sasa mtoto wa Kikwere leo akitawazwa kuwa Chifu wa Wanyakyusa!
Hili sio jambo la utani hata kidogo, ndo maana acha hata Mizimu ikasirike na mambo yaende kama yanavyokwenda sasa.
It's no wonder mvua zinanyesha bila kufuata majira yake, na majanga mengine kibao tunayoyashuhudia sasa,
Ni matokeo ya kuzinajisi Mila zetu kama hivi.
 

Chifu Mwailemale (Ridhiwani Kikwete) akiwa amekalia kigoda baada ya kutawazwa kuwa chifu wa kinyakyusa.

Machifu wa kinyakyusa Ernest Mwailemale (kushoto) na Glasswell Mwakalukwa wakimvisha golole,Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM)Taifa,Ridhiwani Kikwete, alipotawazwa kuwa chifu wa kinyakyusa na kuitwa Chifu Mwailemale juzi katika mkutano wa kampeni za ndani za kuweka mikakati ya kuipatia CCM ushindi wa kishindo,juzi katika Kata ya Ipinda, Kyela.
http://1.bp.blogspot.com/_HO8ijU76ZcQ/TKGokVc4yvI/AAAAAAABQLk/IVYJC5uJsps/s1600/IMG_5637.JPG
Chifu Mwailemale (Ridhiwani Kikwete) akihutubia baada ya kutawazwa kuwa Chifu wa Kinyakyusa.​


Chifu Mwailemale akishangiliwa alipokuwa akikhutubia baada ya kutawazwa kuwa chifu wa kinyakyusa​


Maoni Yangu:
Kweli njaa mbaya, huyu bwana mdogo ana nini cha maana hadi kutukuzwa kiasi hiki?.,Wanyakyusa mmeniangusha sana kwa kweli.​
 
6f2y4o.jpg



huyo ni kuku wa kafara tu hakuna jingine

Anyisile hujakosea, Kuku ndani ya mfuko wa plastiki????? Mzima au kibudu?????
 
Kyela hatuna machifu ,wa mwisho walikuwa akina Koroso,Mwakalukwa na wengineo,hao wanaojiita machifu ni waganga njaa tu,uchifu haupo kabisa Kyela.Njaa za kununua matoki ndio zinawasumbua hao watu wa Ipinda
 
Hivi hiyo Kamati ya utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM)Taifa ina wajumbe wangapi na hao ni kina nani na wanafanya nini wakati huu wa kampeni?

Kuna vijana 30 tuliambiwa wanaunda timu ya kampeni naye akiwemo..
Hivi wengine wanakampenia wapi..? Sijawahi kuwasikia..
 
Absurdities never lack believers!!! And as long as some believe in absurdities we shall have atrocities.

In 2005 some believed his father was the son of a Chagga chief!!!!!!. So no wonder this grandson of a chief is now a Nyakyusa mtemi. Hongera.

Hopefully that is the highest he can climb. VOTE FOR SLAA!!!!!!!
 
Nadhani watu wa CCM inabidi wawe wakweli. Ili suala la kutumia kivuli cha Baraza Kuu la Umoja wa vijana wa CCM katika kumtambulisha Ridhwani ni kuwalaghai wapiga kura. Mimi nadhani watuambie tuu kuwa huyu mtu anapata hiyo nafasi kwa kuwa Baba yake ni Rais.
 
a bad egg never hatches a good chick!It goes through the biological processes for sure.....But in vain!
 
Chifu Mwangupili Dr Jakaya Mrisho Halfan Kikwete akiwa na Chifu Mwailemale Riziwani Kikwete

IMG_0383.jpg

 
Back
Top Bottom