Ridhiwani Kikwete atawazwa kuwa chifu wa wanyakyusa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ridhiwani Kikwete atawazwa kuwa chifu wa wanyakyusa!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ngambo Ngali, Sep 28, 2010.

 1. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #1
  Sep 28, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  [​IMG] Chifu Mwailemale (Ridhiwani Kikwete) akiwa amekalia kigoda baada ya kutawazwa kuwa chifu wa kinyakyusa.
  [​IMG]Machifu wa kinyakyusa Ernest Mwailemale (kushoto) na Glasswell Mwakalukwa wakimvisha golole,Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM)Taifa,Ridhiwani Kikwete, alipotawazwa kuwa chifu wa kinyakyusa na kuitwa Chifu Mwailemale juzi katika mkutano wa kampeni za ndani za kuweka mikakati ya kuipatia CCM ushindi wa kishindo,juzi katika Kata ya Ipinda, Kyela.
  [​IMG][​IMG]Chifu Mwailemale (Ridhiwani Kikwete) akihutubia baada ya kutawazwa kuwa Chifu wa Kinyakyusa.

  NB: Inawezekanaje mtu ambaye sio mnyakyusya atawazwe kuwa chifu wa wanyakyusa????? Chifu Mwailemale pamo akamanya inyiho.

  Huyo Chifu wa sasa kaachia ngazi ( abdicate) ili kumpisha Ridhwani na ni sababu ipi iliyomfanya aachie ngazi na mila zinasemaje????

  Unyakyusa ni sehemu kubwa sana Je yeye ni chifu wa sehemu gani ya unyakyusa???

  Mafumu wanasemaje kuhusu hili?????

  Kigezo gani kilitumika ili kumfanya Rizwani kuwa chifu na wanyakyusa wangapi walishirikishwa katika hili???????

  Mwenye majibu atupatie jamani, tuna kiu ya majibu haya...

  PR stint hii?

   
 2. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #2
  Sep 28, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,470
  Likes Received: 5,847
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Sep 28, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  tumeshaona wengi tu wakitawazwa kwa makabila mbalimbali, sioni kama ni issue... its ceremonial
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Sep 28, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,533
  Trophy Points: 280
  Ngambo Ngali, sasa hii inakuwa too much, kila kukicha Riz1 kafanya hivi, mara Riz1 kafanya vile!, it becomes like obsession at the end of the day sasa itageuka ni majungu au chuki binafsi dhidi ya kwa nyota yake kuzidi kung'aa.

  Wangapi wanatawazwa machifu wa makabila kibao siyo yao na watu hamuulizi, leo katangazwa Riz sasa ndio imekuwa nongwa!
  Mwacheni Chifu Mwailemale aendelee kuchapa kazi nzuri anayoendelea nayo angalau kujaribu kuokoa baadhi ya kura, hivyo kupunguza nakisi.
   
 5. F

  Froida JF-Expert Member

  #5
  Sep 28, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Ajabu na kweli haijawahi kutokea kwa wanyawakyusa hawajawahi kumtawaza mtu asiyetoka kwenye koo zao za kinyafyale hizi pesa zinawafanya watu wawe vipofu kweli mmh makubwa ni mwandosya au mwakyusa wanajipendekeza ili wababki mawaziri upuuzi mtupu
   
 6. N

  Nyumbu- JF-Expert Member

  #6
  Sep 28, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 969
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Mambo ya Mwakipesille, we acha tu!
   
 7. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #7
  Sep 28, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Wakuu mbona mnachanganyikiwa kwa Kijana Riz One kuwa Chifu Riz Mwailemale?
  Mwaka wa uchaguzi huu ,kachagua mahali penyewe kabisa!
  Mbona juzi alikuwa Masasi na Mtwara huko alikosoma na kukulia, hata kumpa ujumbe wa kumi kumi hawakumpa
  Ha ha ha!
   
 8. Smarter

  Smarter JF-Expert Member

  #8
  Sep 28, 2010
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 455
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Jamani Haina ubaya tukijua RAisi namba2 wa TZ anafanya nini,
   
 9. J

  Jembejipya Member

  #9
  Sep 28, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wewe hii pic sasa ndo nana unasemaje???hujaelewa habari hapo juu au una homa ya ubongo?
   
 10. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #10
  Sep 28, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Hivyo ndio kuua tamaduni zetu
   
 11. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #11
  Sep 28, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Hivi kwa nini huhu Kikwete anatumia nguvu kubwa sana kuupata huu u rais? Mimi naheshimu sana usemi kuwa "Chema chajiuza kibaya cha jitembeza". Inatia kero sana.
   
 12. Mentee

  Mentee Senior Member

  #12
  Sep 28, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 142
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Unajua, ngoma ikivuma sana hupasuka. Ebu tuone mwisho wa ukoo huu unaotufanya watanzania zezeta kwa kunyamaza kimya na kuburuzwa. Si msomi sana wa historia, lakini nakumbuka kulikuwa na kiongozi ambaye watu walipochoka walimtoa madarakani wakachinja na familia yooooote. Sasa hawa smiling faces wasitusukume Watanzani kwenda huko. Hawa wazee nao wa Mbeya michosho tu ....
   
 13. Mentee

  Mentee Senior Member

  #13
  Sep 28, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 142
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Like father like son.... sishangai na cheap popularity
   
 14. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #14
  Sep 28, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Picha safi sana.

  Tatizo ni kuwa baba yake hajui kwa nini sisi ni MASIKINI.

  Tangaza hii VIDEO kwa watu wengi uwezavyo:  [​IMG]
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #15
  Sep 28, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  i still dont see this as an issue
   
 16. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #16
  Sep 28, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Waziri Mwakyusa mbona simuoni hapo?????? Maana naye ni chifu.
   
 17. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #17
  Sep 28, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  duuuh,ila nadhani wanamuandaa kuwa somebody in this country
   
 18. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #18
  Sep 28, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Acid naona hii ni issue, itakuwa sio issue kama maswali niliyouliza juu yatajibiwa. Kama makabila mengine yanakubali mtu anatoka aliko na kuja kutawazwa kuwa chifu kwa watu wengine ni sawa basi ni juu yao. Kukubali kwao kusifanye makabila mengine nayo yakubali.

  Kuna vitu vya msingi mtu kuwa chifu jee vilifuatwa?????
   
 19. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #19
  Sep 28, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Pasco kama makabila meengine hayaulizi basi uchifu wao ni fake. Uchifu wa kweli kitu kama hicho kakiwezi kutokea asilani mbona hajawa mangi au Omukama? Ningeuliza hata angekuwa mtu mwingine sijauliza hayo maswali shauri ya Rizwani.

  Unyafyale ni institution isiyo ya mchezo, ndio maana nauliza.

  Ona tabora alivyofariki fundikira wameburuzana mahakamani alijipachika hakustahili. Kwa nini tusiseme?????
   
 20. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #20
  Sep 28, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Gwakisa, hatuchanganyikiwi ila issue ni kuwa hastahili kuwa chifu wa wanyakyusa hata kidogo
   
Loading...