esther mzava
Member
- Sep 23, 2015
- 6
- 40
Mtoto wa Rais mstaafu na mbunge wa Jimbo la Chalinze (CCM) Ridhiwan Jakaya Kikwete, ameshtakiwa na kampuni ya Mount Meru Hotel ya mjini Arusha baada ya kushindwa kulipa deni analodaiwa la tsh 891,600/= na kukiuka mkataba waliongia.
Kwa mujibu wa wakala wa hotel hiyo katika ukusanyaji wa madeni kampuni ya Marcas Debt Collectors ,ndugu Ridhiwan Kikwete anatakiwa kulipa deni hilo ndani ya siku saba toka jana tar 27th May 2016.
Moja binafsi kubwa hapa ni kwanini mh Ridhiwan Kikwete hakulipa hili deni ilhali ni fedha ndogo mno hata ukilinganisha na mshahara wake wa mwezi kama mbunge?
Ama mh Ridhiwan ametaka kuudhibitishia umma juu ya yale yanayosemwa kila siku kuwa yeye ni fisadi,tapeli na amekua anatumia vibaya madaraka yake? maana ni mara kadhaa imeripotiwa kuwa ni mdaiwa sugu ila tukakosa ushahidi timilifu wa madeni hayo kutoka kwa walalamikaji mbalimbali waliowahi kujitokeza na kudai wanamdai fedha ama kutapeliwa na mh R. Kikwete?
Lakini hili pia linatia mtia doa mh Ridhiwan Kikwete na kwa hakika inaonesha ni jinsi gani mh si muaminifu kwa jamii yake na hofu yangu inazidi kwakuwa yeye ni mwakilishi wetu pale Bungeni, je, kweli huyu anatakua muaminifu kwa maslahi ya umma?