Ridhiwani Kikwete akabidhi mradi wa maji safi na salama

mamayoyo1

JF-Expert Member
Jul 25, 2018
1,011
1,019
Mbunge wa Jimbo la Chalinze kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ridhiwan Kikwete amekabidhi mradi wa maji safi na salama katika shule ya Sekondari Mboga iliyopo Jimboni humo.

Akikabidhi kisima hicho, Kikwete amewataka walimu na wanafunzi kutumia kisima hicho kwa uangalifu wa hali ya juu ili kiweze kudumu kwa muda mrefu zaidi.

Pia Ridhiwani amewataka walimu kuwaruhusu wananchi wanaozunguka maeneo hayo kutumia maji hayo ili na wao wanufaike kupitia kisima hicho ambacho kimekuwa ni mkombozi kwa shule na wananchi.

Aidha, sambamba na kukabidhi mradi huo wa maji, pia amezindua mabweni ya wasichana katika shule hiyo na kuahidi kuendelea kujenga mabweni mengine ya wavulana ambapo amesema mabweni hayo yataweza kuwapunguzia adha mbalimbali wanazo kumbana nazo wanafunzi hao.

”Tukishamaliza kujenga mabweni ya wavulana, mahitaji ya maji yatakuwa makubwa zaidi, hivyo sisi viongozi tutajenga tanki kubwa lenye ujazo mkubwa zaidi ili kuweza kuendana na mahitaji yatakayokuwa yanahitajika kwa kipindi hicho,”amesema Kikwete
 
Back
Top Bottom