Ridhiwani Kikwete ahojiwa na tume dawa za kulevya, asema roho imesuuzika

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,189
2,970
Mbunge wa Chalinze jana alihojiwa na tume ya kupambana na kudhibiti madawa ya kulevya. Alipoulizwa kuhusu kuitwa huko, mwenyekiti wa tume hiyo, jaji Siang'a amesema walimuhoji kweli na kila anayetuhumiwa hawatamuacha, watamuita na kumuhoji, wakibaini analo kosa watachukua hatua. Amedai yeye anaamini ni bora kukera baadhi ya watu kwa kutenda sahihi ya anachokifahamu kuliko kuridhisha mtu kwa muda ilhali akifahamu akitandacho si sahihi.

Upande wake, Ridhiwani amesema amefurahi kupata fursa ya kueleza ukweli na wamebaini kuwa hauzi wala kusafirisha madawa ya kulevya. Amedai roho yake imesuuzika na taharuki iliyokuwepo miongoni mwa jamii kuwa huenda anauza dawa za kulevya sasa ianaondoka.

Zaidi, gazeti la Jamhuri

Pia soma: Ridhiwani: Tumeishi na RC Makonda vizuri ila kutajwa kwenye madawa, kama familia tunamwachia Mungu

=====
Visa vya watu maarufu wengine waliowahi kutuhumiwa au kukamatwa na madawa ya kulevya
 
Tangu zamani tulisema... kuitwa kwa Rizimoko ulikuwa ni mkakati wa Riz na Bashite hata kama Rizimoko alijifanya kulalamika!!

Ilikuwa ni lazima Bashite aorodheshe jina lake kimya kimya ili hatimae aitwe!! Baada ya kuitwa, angehojiwa kama alivyohojiwa na hatimae angeonekana hahusiki... CLEANED!!
 
Tetesi za yeye/washirika wake wa karibu kuhusika na hayo mambo zimekuwepo kwa muda mrefu sana,yawezekana kuitwa kwake kulikuwa na lengo la kumsafisha zaidi na si kutaka kufahamu uhusika wake kwenye hayo mambo.

Hizo ni hadaa tu lakini wauzaji/waingizaji wa madawa ya kulevya wanafahamika,hata yule kondakta wa zamani wa Daladala ya "Mungu hana choyo" iliyokuwa inafanya shughuli zake pale jijini Mwanza,anafahamu kuwa alichokuwa anakifanya hakikuwa kupambana na wauzaji bali kuwaficha kupitia majina feki ya watu wasio na hatia.Aliyeweza kumiliki na kutumia majina na vyeti feki anashindwaje kuwa na mipango feki na mapambano feki?
 
Aisee kweli ridhiwani ni mjanja sana, roho yake imesuuzika kwa kuitwa na tume ya kudhibiti madawa ya kulevya, bashite anachekelea kimya kimya, sisi wananchi hatujaelewa kitu tetetetetetete
 
Hata chizi hawezi kuamini kuwa huyu ni msafi eti tatizo lake ni marafiki alionao..wadanganyeni wajinga
 
Kwanini anasema roho imesuuzika?? Ina maana alikuwa na hamu ya kuitwa kuhojiwa? Hii nchi vituko havitaisha..
 
Back
Top Bottom