Ridhiwani, Januari walikwina? Ushauri wa bure tu kwa waotamani uongozi!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ridhiwani, Januari walikwina? Ushauri wa bure tu kwa waotamani uongozi!!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mdondoaji, Jun 25, 2010.

 1. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Na Ezekiel Kamwaga
  Imechapwa 26 May 2010


  ALIPOUAWA mtawala wa Urusi, Nicholaus II, 17 Julai 1918, mauti hayakumfika yeye peke yake. Aliuwawa na watoto wake watano; Alexei, Olga, Maria, Tatiana na Anastasia.

  Hata mkewe wake, Alexandra, daktari wake, nao waliuawa pamoja naye. Nicholaus II aliuwawa kwa kupigwa risasi na wale waliojipachika jina “Bolshevik” – wapinzani wa utawala wa kifalme wa Urusi.


  Hasira ya wananchi wa Urusi ilikuwa kwa ukoo wote wa kifalme. Kama Wakomunisti wale wangepata nafasi wangetekeza ukoo mzima wa mtawala huyo.


  Baada ya Bolshevik kumiminia risasi Nicholaus na familia yake, mabinti wale wanne walikuwa hawajakata roho. Kwa sababu kila mmoja alikuwa amevaa vidani na nguo zilizodariziwa kwa almasi kiasi kwamba risasi hazikuweza kupenya milini mwao.


  Walichokifanya wauaji, ni kuwasogelea karibu mabinti hao – Olga, Maria, Tatiana na Anastasia – kisha kuwaua kwa kuwakata vichwa kwa kutumia mapanga na mashoka!


  Ni ukatili ambao ni vigumu kuueleza kwa binadamu wa kawaida. Na hii ndiyo hatari ambayo naiona kwa wanasiasa ambao wanajitahidi kuingiza familia zao kwenye ulingo wa siasa.


  Kinachotokea ni kwa jamii nzima kuichukia familia nzima badala ya mtu mmoja.


  Kwanza niseme mapema kwamba mimi si miongoni mwa watu wanaopinga watoto wa wanasiasa kuingia katika siasa hususani katika mwaka wa uchaguzi kama huu.


  Roho yangu haisononeki kabisa kwamba Amani Abeid Karume, amekuwa rais wa Zanzibar nafasi ambayo baba yake, Abeid Amani Karume aliishikilia kwa miaka nane.


  Wala sitakuwa na shida iwapo, Balozi Ali Abeid Karume na Dk. Hussein Mwinyi watakuja kuwa marais ama wa Zanzibar au Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


  Aidha, siwezi kuwa na kinyongo iwapo, January Makamba, Kippi Warioba, Ridhiwani Kikwete, Nape Nnauye, John Mongella, Dk. Mwele Malecela, Makongoro Nyerere, Mohammed Moyo, Vita Kawawa na wengine, watabahatika kupata utukufu ambao wazazi wao walikuwa nao huko nyuma.


  Kusema kwamba hawafai kwa sababu tu, baba zao walikuwa wanasiasa ni kuwaonea. Hii ni sawa na kupingana na asili. Kila mmoja anastahili kujiandikia historia yake.


  Tatizo langu kubwa lililopo kwa viongozi wetu, ni kule kutaka “kuchomeka” watoto wao, ambao hawana uwezo wa kuongoza. Kwamba mtu anapanda vyeo kwa sababu ya wadhifa wa baba yake.


  Kama Amani Karume ana sifa na uwezo wa kuwa rais, hakuna sababu ya kutompa nafasi. Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alisema, “Tusichague rais kwa kutokana na kabila lake, dini yake au ukoo anaotoka.”


  Lakini pia hatuwezi kukataa kuchagua kiongozi kwa kuwa tayari baba yake alishika nafasi hiyo.


  Kwenye fani nyingine, kwa mfano kwenye mpira, mtoto atapata mafanikio tu iwapo atakuwa na uwezo. Kwamba Ngassa anaweza kucheza Yanga kwa sababu alikuwa na uwezo.


  Kama angekuwa hajui kucheza mpira kama mimi, asingepangwa Yanga hata kama baba yake angekuwa Imani Madega. Ndiyo maana watoto wa Pele hawapangwi kwenye timu ya Brazil. Kama mtu hana uwezo, hawezi kupangwa.


  Kwenye siasa, mtu ambaye alikuwa hafahamiki wala kujulikana, ghafla anapanda vyeo na kuwa na ushawishi mkubwa mara mzazi wake au ndugu yake anapokuwa na madaraka ! Hapa ndipo kwenye matatizo.


  Nicholas aliuawa kwa sababu hakuwa kiongozi mzuri. Alifanikiwa tu kuwa mtawala wa Urusi kwa sababu baba yake, Alexander III alikuwa Mfalme na alipokufa yeye akamrithi.


  Katika kitabu cha Guns of August, mwanahistoria Barbara Tuchman aliandika kwamba mfalme Alexander III alikuwa hajampa mafunzo yoyote mwanaye (Nicholaus) kuhusu mambo ya utawala.


  Alikuwa amepanga kumpa mwanaye huyo mafunzo rasmi atakapokuwa ametimiza umri wa miaka 30 lakini kwa bahati mbaya mfalme akafariki wakati mtoto ana umri wa miaka 26.


  Kwa hiyo, kwa sababu tu Nicholaus alikuwa mtoto wa mfalme, akapewa fursa ya kurithi bila ya kujua kitu kuhusu utawala.


  Katika kitabu hicho, Tuchman anaeleza tukio moja kumhusu Nicholaus, kwamba wakati alipopewa taarifa za awali kuhusu mashambulizi yaliyokuwa yakifanywa na Wakomunisti hao, “aliisoma taarifa hiyo na kisha kuiweka mfukoni kabla ya kuendelea kucheza tennis.” Hakufanya lolote!


  Ni vema, katika mwaka huu wa uchaguzi, wanasiasa wetu wakawa makini sana katika namna ambavyo wanahusisha familia zao na mambo ya siasa.


  Kama mtu alikuwa si lolote wala si chochote kabla baba au mama hajawa rais au waziri mkuu, anakuaje kila kitu wakati baba anapokuwa mkubwa?


  Uongozi unahusu ugawaji na matumizi ya rasilimali za taifa. Ni vema, kwa kiongozi na familia yake, akafahamu wananchi wanapomka wanakuwa na uchungu sana na matumizi ya rasilimali zao.


  Kama kiongozi anaona mkewe au mwanaye ana sifa na uwezo wa kuwa kiongozi, ni vema akamruhusu ili asilinyime taifa uongozi murua.


  Lakini, atakuwa anafanya jambo la hatari sana kama ataruhusu watu wake wa karibu kutumia cheo na ushawishi wake kujiingiza kwenye mambo ya nchi.


  Hapa atakuwa anaiingiza familia yake katika matatizo makubwa bila ya kufahamu. Wakati utakapofika wa yeye kuondoka madarakani, afahamu hataondoka peke yake, ataondoka na familia yake.


  Na kama walifanya vibaya, afahamu kwamba ataandamwa, yeye na familia yake, kwa kiwango ambacho kuna kipindi hakuna mtu wa familia huyo atapenda kutumia ubini wao kujitambulisha.


  Kabla kiongozi hujamruhusu mwanao au mkeo kuingia kwenye siasa wakati wewe ni mtawala, ni vizuri ujiulize ni kwa nini hawakuingia kwenye siasa kabla hujawa kiongozi.


  Kwamba inakuaje ghafla wanakuwa na sifa za uongozi baada ya wewe kuwa madarakani? Mbunge wa Njombe, Dk. Ndembela Ngunangwa, alikemea hilo kwa kuuliza: Walikwina – walikuwa wapi - kabla ya wewe kuwa madarakani?


  Kimsingi hili ni jambo rahisi sana kulifanya. Hakuna sababu ya viongozi wetu kuingiza familia zao kwenye matatizo. Makosa yao yanaweza kusamehewa na kizazi cha jana na leo.


  Nani ajuaye kizazi cha kesho kitakuwa na maamuzi gani?  Source:
  Mwanahalisi.


  Mtazamo: Waungwana waheshimiwa wa kesho kabla hamjakimbilia zaidi mjiulize maswali yafuatayo:-
  a. Baba au Mama yako mzazi aliyekuwa kiongozi alifanya yepi mema kwa watanzania???
  b. Je mimi (mtoto wa muheshimiwa) ninaweza kuyaendeleza yale mazuri???
  c. Je yale mabaya ya mzazi vipi yanaweza kutibiwa? na mie nitaweza kuyatibu????
  d. Ni mifano gani ambapo wananchi walipochoka wameamua kuchukua sheria mikononi mwao kwasababu ya kurithishana???

  Kumbuka sio kila anayezaliwa katika ukoo lazima arithi alichokuwa nacho mzazi kwani elimu, uongozi ni vitu mungu humbariki mtu na sio mtu kuzaliwa nacho!!!!
   
 2. T

  Tanzania Senior Member

  #2
  Jun 25, 2010
  Joined: Jun 6, 2008
  Messages: 114
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ubarikiwe
  1. Moyo wa upendo ulionao juu ya Viongozi na familia zao
  2. Moyo wa upendo na maendelea ya nchi na Watanzania wote.

  Nimekuwa natafakari jambo hili kwa zaidi ya miaka miwili sasa, hasa baada ya kufuatilia tofauti za Naibu waziri wa Nishati na Madini (wa sasa) Kigoma Malima na Mengi. Sikuweza kuamini kama Mh. Kigoma Malima anasifa za kuongoza hata kikundi cha watu 10.
  Anyway, nisimuonee sana maana wako wengi sana.

  Nani wa kulaumiwa? Jibu ni Watanzania. Hasa wale ambao tumepata nafasi ya kwenda shule na kujua namna gani Utawala wa nchi unakuwa chanzo cha Umaskini na maisha duni ya watu na nchi kwa Ujumla.

  Naamini si kila mtanzania anajua kuwa maisha duni ya watanzania yanasababishwa na Utawala.
   
 3. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2010
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Well said..........but opportunity is never lost when it presents itself!
   
 4. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #4
  Jun 25, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mtanzania kwanini sasa tuaachia hali hii kuendelea???
   
 5. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #5
  Jun 25, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Ni kweli but also let me ask you how many of them were given such an opportunity to compete one another? Au opportunity inakuwa presented for choosen few to grab it. Inakuwa kama ile stori ya muhindi unafukuza watu wote wanaoweza kumshinda mwanao darasani na kubakia wale ambao mwanao anawashinda ili useme si unaona ametokea wa kwanza kati ya 10 darasani wengine 40 hawajafanya mtihani so even though yeye ni wa kwanza yes but ratio ni kwamba yeye ni wa kwanza kwa 1/4 ya darasa sasa ndio opportunity hiyo????
   
 6. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #6
  Jun 25, 2010
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Africa hakuna fair play ndugu yangu........utaumiza kichwa bure!
   
 7. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #7
  Jun 25, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Sio Africa hakuna fair play duniani hamna fair play but this is the focal point Africa watu hugeuka kuwa wanyama saa zengine haki ikizidi kupotea sasa sijui unasemaje hapo? Mfano Senegal, Angola, Rwanda, Sudan etc sijui wasemaje.

  Ikitokea Mwinyi anataka mtoto wake, Kikwete mtoto wake, Salim mtoto wake mwisho wa siku kuna kundi la watu litajengeka kujiona wao wataendelea kunyonywa tu na kutawalia. Hawa watakuwa na chuki dhidi ya watawala na ndio hapo atatokea mtu mfano wa Hitler, Idd Amin and akina BNP (Uingereza) wataeneza siasa za chuki kupata support.
   
 8. DMussa

  DMussa JF-Expert Member

  #8
  Jun 25, 2010
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 1,301
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Afrika jamani is a dark continent!!
   
 9. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #9
  Jun 25, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  The allegory of the Bolshevik story beats me, nways hata hivo endeleeni na siasa zenu uchwara , mnavuna ubua na mtaendelea kuvuna ubua milele.
   
 10. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #10
  Jun 25, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Pamoja na historia ndefu na maelezo mazuri lakini yasiyotaka kujicommit kwenye specifics, ili kuwa na mchango wa maana huwezi kuepuka specifics.

  Basically kinachosemwa na article nzima ni kwamba "tusiwape watu nafasi kwa sababu ya majina yao, lakini tusiwakatalie watu nafasi kwa sababu ya majina yao pia". Well and good, hata mimi nilishawahi kusema hili hapa, wengi wetu - ukiacha wale wanaoleta passion iwaambie nini cha ku vote- wako reasonable enough kujua hilo.

  Kitu ambacho tungependa kujua, kitu ambacho kingeweza kuwa na mchango zaidi, ni specifics.

  Kati ya hao wote uliowataja, kwa sababu unatuambia tusichague kwa majina, na wala tusikatae kuchagua kwa majina, ila kwa uwezo, ni nani ana uwezo na nani hana? Na kwa sababu gani?

  So long as umeamua kuandika, changia kitu solid.Ukiweza kuandika article hiyo, kwa usomi na uchunguzi huo huo, utakuwa umesaidia zaidi ya hii general truism ambayo haitufumbui macho kwa lolote tulilokuwa hatulijui wengine.

  This sitting on the fence business and saying generally "tusichague/kuwapa nafasi watu kwa sababu ya majina, lakini pia tusiwakatalie watu nafasi kwa sababu ya majina" is rather tired and smacks of fake modesty to me.

  Al Pacino anakwambia if you want to shoot, shoot, don't talk. Kama unataka kuwablast wablast live, sio unakuja na half steps.
   
 11. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #11
  Jun 25, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  I don't care much about name recognition and whatnot. So long as the person running has the bonafides...I have no qualms.
   
 12. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #12
  Jun 25, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  The author beats around the bush a lot to make one basic point which is we should elect leaders based on merit regardless of their last names. The author makes a good point in saying that there are people who come from political families who actually have the potential to be good leaders but there are those who clearly are in place simply because of name recognition.

  Well it is hard to fault these children from political families. How many of us wouldn't do the same if we were in their position? How many of us haven't used some form of connection in order to get ahead? How many of us are where we at purely because of merit and our own doing? Could be we are just angry at people who were lucky enough to be born with a silver spoon in their mouths. Could be deep down inside we want the same opportunities they have.

  This argument can be made for either side of the coin. Depends on how you view life in general. Mostly likely if one is born into prestige they will be against this argument & naturally I feel those of us who were born into normality would feel that we are in an unfair position. Just food for thought however.....if any of us ever succeed, how many of us won't use our money or connections to insure our children get ahead in life? Interesting topic.
   
 13. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #13
  Jun 25, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Pronto,

  But the question remains, who has the bonafides and who is a pretender ? Zaidi ya hapo tutazunguka tu kwa kukubaliana generalities bila ku address specifics.
   
 14. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #14
  Jun 25, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Kumuuliza mtu ambaye hana access na privilege angeweza au asingeweza kujizuia na vishawishi vya kutafuta ukubwa bila ya kuwa na uwezo is most disingenuous.

  Huwezi kutuweka katika a time machine, ukatupeleka katika an alternate universe ambako tumegeuka watoto wa marais na wakubwa wengine na kutuangalia tutakavyoishi, na kwa sababu huwezi kufanya hivi, huna haki ya kusema au ku entertain mawazo kwamba tusingeweza kujizuia na vishawishi vya kutaka ukubwa.Mbona hata sasa kuna watoto wa "wakubwa" kibao hawataki kusikia habari za kuwaingiza katika siasa hata kidogo? Sasa utaweza vipi kusema sisi tusingeweza kuwa kama wao? This mind experiment is based on a fallacy (to my knowledge alternate universes and time travel are still a realm of science fiction) and at best is an exercise in futility.

  Let's talk about what we know to be the case in this universe, not some conceptual speculation based on a nonexistent alternate universe.
   
 15. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #15
  Jun 25, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  "Don't wait for extraordinary opportunities. Seize common occasions and make them great. Weak men wait for opportunities; strong men make them".

  Where were the Ridhiwanis a time before?

  I repeat, only Idd Amin like people would see their political powers an opportunity for their incapable children.
   
 16. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #16
  Jun 25, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Nahisi kuna watu wanajidanganya wana uwezo wa kuamua nini kitokee baadae kwasababu wana control za sehemu nyeti za uongozi wa nchi yetu. Wanafanya makosa makubwa sana. Time will tell...nachojua we need to have strong leaders. Tumeshachoka na majina ya watu ambao hawafanyi lolote la maana kwa Taifa hili. Mifano ipo mingi tu.....wana madaraka kwasababu ya majina ya baba zao. Ipo siku ufalme huo utanyan'ganywa na kupewa watu wengine.
   
 17. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #17
  Jun 25, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Does it mean we should keep quiet even if we see there is a problem?
   
 18. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #18
  Jun 25, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Hata mimi nakubaliana na wewe 100%. Tunachojiuliza kiko wazi...ni ule ule uswahili na ushabiki ndio msukumo wa kuhakikisha mtoto anakuwa mrithi hata kama hastaili au ni kweli mtoto yule anastahili. Tanzania ya leo sio ya kesho.Kuna watu wanajidanganya mambo yataendelea kuwa mtelemko. Kuna influence kubwa sana sasa hivi inayolazimisha mitazamo ya watu kubadilika.
   
 19. m

  magee Senior Member

  #19
  Jun 25, 2010
  Joined: Jun 3, 2009
  Messages: 126
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  we need positive thinking to change things.....it is true very true that there's no fair play in africa but admiting in na kuishia kumkatisha mwenzio tamaa kwamba ataumiza kichwa bure.....thats bad,very bad and it is a sign of cowardness!!
  We need fighters,strong man to influence the society.........
   
 20. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #20
  Jun 25, 2010
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mkuu usifikiri mi napenda hii kitu.....la hasha, najua hata kama haina effect kwangu lakini ndugu, jamaa, marafiki, watoto wetu wataathirika kwa uongozi mbovu wa kupachikana! Tatizo ni kuwa uamsho bado uko mbali......................hivyo watu wana-take advantage....na wenzetu walioendelea kidemokrasia wanakaa kimya kwa vile wananufaika na ubovu huo, wanajua kiongozi asiye makini hana msimamo

  [FONT=&quot]"Water which is too pure has no fish"[/FONT]
   
Loading...