Ridhiwani Jakaya Mrisho Kikwete, Mtetezi wa ajira kwa vijana

A4.

JF-Expert Member
Mar 16, 2014
671
0
Mbunge wa Chalinze;
Ni mbunge wa kwanza kumsikia akitetea vijana katika maswala ya ajira bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuweka wazi ukiritimba uliopo katika taasis na mashirika ya Umma.

"Mheshimiwa mwenyekiti, unakuta mwanafunzi amemaliza chuo, anaenda kuomba ajira anaambiwa awe na uzoevu usiopungua miaka miwili, atautoa wapi huo uzoevu? Waajirini wapate uzoevu. Kuna baadhi ya Taasis kama T. R. A kuna ukiritimba wa ajira, ajira zinatolewa kwa kujuana"

Naunga mkono mia kwa mia kwani ni kweli huu ukiritimba wa kupeana ajira kwa vimemo upo katika taasis na mashirika mengi kama vile; T.R.A, TANAPA, B.O.T, TPDC, n.k. Haya mataasis haya yamekubuu kwa uchafu huo.

Nasubiri mbunge atakayemuunga mkono Ridhiwani hata kupeleka hoja binafsi bungeni ya kuangaliwa upya mfumo wa ajira katika hizi taasis.

Mfano kule TANAPA unakuta kaajiriwa baba,mama na mtoto acha wajomba, mawifi na wengineo! Hizi taasis zimekuwa kama ni za familia! Aibu hii!

"Natoa shilingi hadi huu ukiritimba angalau upungue na naomba wananchi wenzangu waniunge mkono"
 

manucho

JF-Expert Member
Apr 20, 2012
3,406
1,195
Hii ni system ambayo tumejiwekea sisi ukoo wa panya.
Kama Baba yako au mama yako hakuwa huku kwenye ukoo utajijua. Hii nchi ni yetu sisi Watu WACHACHE. Riz1 mwenyewe anajua.
 

iMad

JF-Expert Member
Aug 4, 2013
1,833
0
Yaani hiyo system si imesetiwa na chama chake au..maana chama chake ndo kimeshika serekali..tra ipo chini ya chama chao..kwani wapinzani huwa wanaongea nini..jukwaani hap watu wanaongea nini..wahusika si wao..?! Nani kawajibishwa kutokana na hiyo hali..?! Inashangaza..!
 

Mkoroshokigoli

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
14,605
2,000
Haya mambo si ndo yameanzia huko kwenye siasa zao???sasa kuna shida gani yakija huku???hapo alilalamika tu na ataendelea kulalamika,tatizo tunachanganya kulalamika na kuchukua hatua,shemeji mwenyewe ni mlalamikaji
 
Jan 5, 2014
66
0
Kwa hili la kujuana, ni kweli kabisa utakuta kuna taasisi, zimejaa watu wa kabila moja au jamii fulani au watu wa mkoa fulani tu, hii sijui imekaaje?
 

mtwa mkulu

JF-Expert Member
Sep 11, 2013
4,433
2,000
Amekutuma we? mbona unaandika kama Division 0?Ameongea ukweli lakini yeye si wakwanza. Namshangaa Liz Kiritimba Mpinga ukiritimba
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom