Ridhiwani awapa siku 7 Dr. Slaa na Mtikila kukanusha utajiri wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ridhiwani awapa siku 7 Dr. Slaa na Mtikila kukanusha utajiri wake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OgwaluMapesa, May 2, 2011.

 1. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #1
  May 2, 2011
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Baada ya kujitangaza kuwa Milionea na kukanusha Ubilionea. Leo hii ameamua kukutana na waandishi wa Habari katika hoteli ya hadhi yake ya New Afrika. Mashuhuda wetu wameshavinjari eneo la mkutano huo na wakati Milionea Rizwani atakapoanza kumwaga data za wapi alipata umilionea wake na kukanuasha kufikia ubilionea, watakuwa wakitupatia taarifa.
   
 2. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #2
  May 2, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Stupid mongol rz1 days are numbered
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  May 2, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Anataka wasafisha akina Chenge, Rostam na Lowassa
   
 4. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #4
  May 2, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Mh. Membe, hii thread inuliza juu ya Press Conference ya Mukama, hayo ya riz1 yapeleke kwenye thread yake.

  Walioko huko Peakock, tupeni updates!
   
 5. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #5
  May 2, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Iko wazi kuwa ana miliki Hotels hizi Morogoro, na walikuwa wanakamilisha ujenzi wa ghorofa ambayo ingekuwa kubwa refu zaidi kwa sasa hapa moro, akishirikiana na yule aliyekuwa mhasibu wa Bagamoyo aliyeondolewa madarakani(aliyempa Muro kesi). Riz1 anaonekana mara kwa mara kwenye usimamizi waujenzi wa Hotel hizo, na kukagua pia zile ambazo zinafanya kazi.

  Tunamtaka ajitokeze, afafanue kuwa anapata wapi hizo billions za kujenga na kumiliki mahotel hayo hapa Moro...
   
 6. Wa Kwilondo

  Wa Kwilondo JF-Expert Member

  #6
  May 2, 2011
  Joined: Sep 15, 2007
  Messages: 1,083
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  yetu macho! kama ni kweli mkuu anahusika moja kwa moja!
   
 7. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #7
  May 2, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,150
  Likes Received: 3,339
  Trophy Points: 280
  Tutazitaifisha.
   
 8. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #8
  May 2, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Muda ukifika kila kitu kitaeleweka, kijana hawezi kuwa na mali kwa haraka kiasi hicho kama si ufisadi
   
 9. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #9
  May 2, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  hoteli zipi hizo?
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  May 2, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,194
  Trophy Points: 280
  Hana maelezo ndiyo maana anapata kigugumizi. Ngoja tuendelee kusubiri labda atatwambia ni mali za Rostam.
   
 11. Uliza_Bei

  Uliza_Bei JF-Expert Member

  #11
  May 2, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 3,109
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  NASIKIA NI HOTEL ZINAZOITWA '''GWAMI HOTEL'''' Mbona nasikia pia wana hisa 30% katika mradi wa Mzindakaya kule Sumbawanga ndiyo maana eti pesa za TIB wamemkopesha Mzindakaya pamoja na kuwa ana deni bado la uwekezaji ule wa mwanzo:::::r1 mbona waweza jitokeza japo kusema ndiyo au siyo?
   
 12. Uliza_Bei

  Uliza_Bei JF-Expert Member

  #12
  May 2, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 3,109
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  NASIKIA NI HOTEL ZINAZOITWA '''GWAMI HOTEL'''' Mbona nasikia pia wana hisa 30% katika mradi wa Mzindakaya kule Sumbawanga ndiyo maana eti pesa za TIB wamemkopesha Mzindakaya pamoja na kuwa ana deni bado la uwekezaji ule wa mwanzo:::::r1 mbona waweza jitokeza japo kusema ndiyo au siyo?
   
 13. D

  DoubleOSeven JF-Expert Member

  #13
  May 2, 2011
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 661
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ... ongezea na ile plot Samora Avenue kabla ya NBC. Iko wazi mda sasa.... haiskamatiki labda umuone yeye!!
   
 14. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #14
  May 2, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mungu waaibishe na CCM yao
   
 15. N

  Nzogupata Member

  #15
  May 2, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naamini kuna m2 kama si bb sijui nani mwingine wakumwamini ampe kazi hiyo? Mjadala uko wazi ni ngumu asiemtambua wala kuwa nae karibu ampe usimamizi. It is obvious kama anaonekana hapo ni zake au zao
   
 16. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #16
  May 3, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  MTOTO wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani Kikwete amesema, Watanzania wasimhukumu kwa kumuona akiendesha magari ya bei ghali na wazipuuze kauli zinazotolewa na wanasiasa wawili wa upinzani kuwa yeye ni bilionea. Amekanusha tuhuma dhidi yake kuwa ni bilionea na kutoa siku saba kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa na Mwenyekiti wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila, kuthibitisha tuhuma hizo.

  Ridhiwani amewataka viongozi hao wakanushe tuhuma walizomtupia au kuthibitisha kwa vielelezo, vinginevyo atawaburuza mahakamani kwa kumchafua yeye na familia yake. Ridhiwani aliwataka Watanzania wasimhukumu kwa kumuona mitaani akiendesha magari ya bei ghali kama vile Benz na kuelezea kuwa, hiyo inatokana na namna alivyolelewa na wazazi wake kuhusu namna ya kuishi na watu. “Hapa mjini jamani tunaishi kimjini si kila kitu unachomuona nacho mtu ni cha kwake,” alieleza Ridhiwani katika mkutano wake na waandishi wa habari Jumatatu Dar es Salaam.

  Amesema, Dk. Slaa na Mtikila wamekuwa wakimzushia kuwa yeye ni bilionea na kwamba anamiliki kampuni ya malori 150 na ya ujenzi pamoja na ghorofa za kupangisha, jambo ambalo si kweli. Aliita habari za viongozi hao kuwa ni za uongo na uzushi na zimelenga kumchafua yeye na mzazi wake na kupandikiza chuki dhidi ya familia yake na jamii. “Nachukua nafasi hii kuwaeleza umma kuwa mimi nawaheshimu sana hawa wazee na ingekuwa busara kwa umri wao na mamlaka waliyonayo ndani ya jamii na vyama vyao vya siasa wajitokeze na kutoa ushahidi juu ya wanayosema dhidi yangu katika vyombo vya habari ili hatua zichukuliwe,” alisema Ridhiwani.

  Alisema, akiwa kijana aliyemaliza shule hivi karibuni, haiwezekani kumiliki mali zote zilizotajwa na kama kweli anamiliki, itakuwa rahisi kuthibitisha kwa kuwa ukiwa na kampuni lazima kuwe na jina la mmiliki na akaunti ambako fedha za kampuni hiyo zinakwenda. “Huwezi kuandika akaunti ya mtu hivi hivi ukadai kuwa una kampuni akikuibia?,” Alihoji. Alisema, yeye si bilionea kama wanavyodai wanasiasa hao, na kutaja mali zake kuwa ni shamba lililopo Bagamoyo la ekari moja na nusu, gari aina ya Toyota Cami na akaunti mbili katika benki za Stanbic na NBC. Aliwataka viongozi hao kama itathibitika kuwa habari walizomtuhumu ni uongo, wautangazie umma na kuliweka hilo bayana kwa sababu hiyo siyo mara yao ya kwanza kuongopa na kutoa taarifa zisizo za kweli.

  Alitolea mfano habari aliyowahi kuitoa Dk. Slaa kipindi cha uchaguzi mwaka jana kuwa watu wasiopungua 50 walikutana jijini Mwanza katika Hoteli ya La Cairo pamoja na Rais Jakaya Kikwete wakati huo mgombea urais, jambo ambalo kwa mujibu wa Ridhiwani halikuwa la kweli kwa kuwa yeye mwenyewe alikuwa Nachingwea na Rais Kikwete Kibaha. Alisema, pia Dk. Slaa aliwahi kudai kuwa na uthibitisho wa kontena la kura kukamatwa Tunduma mkoani Mbeya, jambo ambalo halikuthibitishwa. Kwa upande wa Mtikila, alisema amewahi kukiri kuongopewa.

  Aliwataka viongozi hao wawili kuacha kuwa makanjanja wa kutengeneza habari katika njia ya kutafuta sifa za kisiasa na badala yake watoe ushahidi juu ya wanayoyasema, vinginevyo baada ya siku saba atawaburuza mahakamani. “Kwa umri wao na nafasi walizonazo ni fikra zangu kuwa wataacha kuwa wasema hovyo na kuendeleza utamaduni unaonekana kukua kwa watu kuanza kutumia vyombo vya habari bila kuwa na ushahidi wa kutosha wala kuheshimu haki za watu,” alisema.

  Akijibu swali juu ya viongozi hao kuwa huenda wanatumiwa na mafisadi wanaompiga vita Rais Kikwete, Ridhiwani alisema: “Kuhusu suala hili kuhusishwa na ufisadi siwezi kulizungumzia, ila kama wananishambulia kwa sababu mzee anapiga vita ya ufisadi, jambo hili si la Ridhiwani au baba, bali ni la Watanzania,” Aliongeza “haitopendeza hata kidogo na wala sitaki kuamini kuwa viongozi hao wawili wanatumiwa.”

  Hivi karibuni, Dk. Slaa akiwa katika moja ya mikutano ya hadhara mkoani Tabora, alisema Ridhiwani amemaliza shule miaka michache iliyopita, lakini hivi sasa ni bilionea na kwamba ameupata utajiri huo katika mazingira ya kutatanisha.

  Wakati Mtikila kwa upande wake akizungumza na waandishi wa habari alidai Ridhiwani amegeuka bilionea kwa muda mfupi “kwa mgongo wa baba yake.” Alienda mbali na kudai kijana huyo ambaye Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana (UVCCM), aliingiza magari makubwa ya mizigo zaidi ya 100 na yanafanya kazi ya kusomba mizigo DRC na mengine ameyauza. Aidha, alidai pia kuwa mtoto huyo wa rais anamiliki kampuni ya ujenzi wa barabara na maeneo mengi ya ardhi kwa lengo la kujenga ghorofa za kupangisha.

  Habari Leo
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #17
  May 3, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,194
  Trophy Points: 280
  Quote of the Week:

  “Hapa mjini jamani tunaishi kimjini si kila kitu unachomuona nacho mtu ni cha kwake,”

  ~~Ridhiwan
   
 18. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #18
  May 3, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,194
  Trophy Points: 280
  Mhhhhh!....Mercerdez Benz kwa hisani ya Rostam, suti kwa hisani ya Nimrod Mkono, kiatu cha bei mbaya kwa hisani ya Chenge. Na ile nyumba ya bei mbaya kwa hisani ya Al Adawi. Anazikimbia mali zake kama Rostam alivyoikana na kuikimbia Richmond/Dowans. Kazi kweli kweli!
   
 19. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #19
  May 3, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  hahahahah lol
  hivi ni vichekesho
  "Hivi kweli unategemea aseme YES mimi ni billionaire "
  lazima atajitetea jinsi nilivyosoma hapao juu anaongea
  kwa maringo na kujigamba ..
  mtoto wa Nyoka ni Nyoka
   
 20. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #20
  May 3, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,194
  Trophy Points: 280
  Awamu za uwazi na ukweli hizi AD! Kila mtu aliye kwenye ngazi za uongozi na familia yake inabidi waanike mali zao hadharani. Sasa atazikimbia mali zote na kusema si zake. Ngoja tuone kasheshe hii itaelekea wapi? Siku saba zikiisha labda atafungua kesi na hapo ndipo Dr Slaa ataanika mali zote za Ridhiwan na kuweka uthibitisho kwamba ni zake na Bin Kikwete atadai mali hizo si zake bali ni za Rostam, Al adawi na Mkono. Kazi kweli kweli!
   
Loading...