Ridhiwan, Sofia, Mwanri, Dk. Kimei wafikishwa TAKUKURU


Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,611
Likes
634,716
Points
280
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,611 634,716 280
Ufisadi Ardhi wamtisha Waziri Anna Tibaijuka
• Ridhiwan, Sofia, Mwanri, Dk. Kimei wafikishwa TAKUKURU

na Ratifa Baranyikwa


amka2.gif
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, ameanza kazi kwa kuwataka watu ama vigogo waliochukua maeneo ya wazi na waliojipatia viwanja isivyo halali kujisalimisha mara moja kabla mkondo wa sheria haujachukua nafasi yake. Tibaijuka alitoa agizo hilo jana wakati wa mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo, jijini Dar es Salaam.
Waziri huyo ambaye alikuwa ameongozana na Naibu wake, Goodluck ole Madeye, Katibu Mkuu, Patrick Rutabanzibwa, pia alisema kama kuna watu wamevunja sheria kwa kujipatia maeneo isivyo halali aidha kwa kushirikiana na maafisa wa wizara hiyo, hawatabaki salama.
Tibaijuka alisema wanaotumia jeuri ya fedha kwa kuvunja sheria nao hawatabaki na kuongeza kuwa kama sheria ina upungufu katika eneo linalosababisha migogoro itafanyiwa marekebisho.
“Kama kuna watu wamevunja sheria hawatabaki….nasema bora wajisalimishe, waliochukua maeneo ya wazi wayarudishe, kama kuna mtu kapewa kiwanja ajisalimishe,” alisema Prof. Tibaijuka.
Kadhalika waliojitwalia maeneo ya fukwe za bahari, aidha kwa kujenga nyumba zao au chochote kile, Tibaijuka alisema watu hao wako kwa muda tu kwa kuwa sheria haikubali kujenga katika maeneo hayo.
“Walioko kwenye Beach wako kwa muda tu zile ni Public Utilities, zipo kwa ajili ya watu kwenda kufurahi si kwa ajili ya kujimilikisha wao, wataalamu wetu wanajipanga tutafika huko,” alisema Tibaijuka.
Akizungumzia kero na migogoro ya ardhi, na watu kujenga kiholela, alisema watarudisha walinzi wa ardhi katika manispaa ambao walikuwepo katika siku za nyuma kwa kazi ya kulinda ardhi.
“Tutarudisha walinzi wa ardhi, ili kupunguza migogoro ya ardhi, hili limetugharimu sana,” alisema Tibaijuka.
Katika hilo pia alisema migogoro ya ardhi hawawezi kuimaliza wao kama viongozi bila kushirikiana na wananchi.
Alisema wataweka kwenye tovuti ya wizara eneo la kutoa taarifa kama za mtu kuiba eneo au kujitwalia isivyo halali ama kaziba barabara na kero nyingine.
“Tunahitaji jamii itusaidie kuimaliza migogoro ya ardhi ili tuweze kujikita kwenye masuala ya msingi ya teknolojia kama ya kupima.
“Najua kuna kero za msingi, viwanja vimeuzwa, najua miji yetu, kuna ujenzi holela….Dar es Salaam hakuna eneo la kuegesha magari...kwa kipindi hiki hatutalala.
“Ukienda miji ya wenzetu inafurahisha, kuna maeneo ya kucheza mpira kuna maeneo yamepangwa vizuri lakini hata Mwalimu alisema kuna maendeleo ambayo hayahitaji pesa mfano usafi au kuandika majina ya mtaa hili tunaweza kutekeleza ndani ya miaka miwili tutakuwa tumechelewa,” alisema.
Tibaijuka alisema sekta ya ardhi ni sekta muhimu na wao Umoja wa Mataifa walikuwa wakiita agenda kwa sababu ni sekta mtambuka, kwa maana masuala ya ardhi yasipofanyiwa kazi sekta nyingine zinadorora.
Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Patrick Rutabanzibwa, amezungumzia jina lake kuhusishwa kwenye kashfa ya sanya sanya ya viwanja katika maeneo muhimu nchini ikiwahusisha waliokuwa mawaziri pamoja na familia zao akiwemo pia mtoto wa Rais Kikwete, Ridhiwan Kikwete.
Kashfa hizo ziliripotiwa na gazeti moja la kila wiki, ambalo lilidai kuwa katika baadhi ya maeneo nchini, ikiwamo mikoa ya kanda ya Kaskazini, Dar es Salaam na mkoa wa Pwani, inaonyesha kwamba vigogo hao wamekuwa wakijitwalia maeneo kwa kasi ya ajabu; huku wenyeji wa maeneo hayo wakinyimwa.
Katika hilo, Rutabanzibwa alikiri kuwepo kwa mtandao wa kuuza ardhi kwa ushirikiano kati ya watu na wizara na halmashauri.
Alisema jina lake limetajwa, kwa kuwa tu alijitolea kuwashughulikia hao watu kwa kuanza kuwapangua watendaji.
Alisema huo ndio ulikuwa mwanzo wa kuchafuliwa kwenye magazeti ikiwa ni mbinu ya kumuondoa kwenye lengo la kuacha kuwashughulikia.
“Watu waliofanya hujuma tutawashughulikia, mimi binafsi nimelipeleka suala hili kwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) wachunguze wajue ukweli wa hili suala na mimi nitatafuta siku nizungumze,” alisema Rutabanzibwa.
Kwa mujibu wa taarifa za gazeti hilo baadhi ya maeneo yaliyotajwa vigogo wanaotuhumiwa wamekuwa wakinunua kwa fedha taslimu na mfano hili lilitokea mkoani Arusha eneo la Burka ambako siku chache baada ya uchaguzi mkuu, vigogo kadhaa waligawiwa viwanja katika mazingira ya kutatanisha mara baada ya Halmashauri ya Arusha vijijini kutangaza kugawa viwanja kwa ada ya sh 10,000.
Mbali ya Ridhiwan, vigogo wengine wanaodaiwa kugawiwa viwanja Burka ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Phillip Marmo, na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Aggrey Mwanri.
Wengine ni Sophia Simba ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM (UWT) na pia Waziri wa Jinsia na Watoto.
Vigogo wengine ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Benno Ndulu, Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Stephen Kimei, Meneja wa Benki hiyo mkoani Arusha, Chiku Issa Athuman, na aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo, John Ole Saitabau, na Katibu Mkuu wa UWT mkoa wa Arusha, Elly Minja.
Katika orodha hiyo pia wamo wakuu wa mikoa ambao ni Mkuu wa Mkoa wa Singida, Parseko Vicent Kone, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Isdori Leka Shirima, na Mkurugenzi Mtendaji wa jiji la Mwanza, Wilson Kabwe, mbunge wa viti maalumu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ritha Mlaki, na Mbunge wa Singida Vijijini, Lazaro Nyalandu (CCM).
Pia wamo watu wenye majina ambayo yana ubini unaofanana na viongozi maarufu na hao ambao ni Frida Nyalandu ambaye anadaiwa kuwa ni ndugu wa mbunge Lazaro Nyalandu, Innocent Karamagi ambaye uhusiano wake na Nazir Karamagi haukuweza kufahamika mara moja, Andrew Lowassa, Hilary Ngoyai na Evance A. Ngoyai ambao pia uhusiano wao na aliyekuwa Waziri Mkuu Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, haukufahamika mara moja kwa mujibu wa gazeti hilo.
 
Njowepo

Njowepo

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Messages
9,392
Likes
467
Points
180
Njowepo

Njowepo

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2008
9,392 467 180
Chukua Chako Mapema
 

Forum statistics

Threads 1,238,278
Members 475,878
Posts 29,314,610