Ridhiwan Kikwete avamiwa na vijana wa CHADEMA ashindwa kufanya kampeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ridhiwan Kikwete avamiwa na vijana wa CHADEMA ashindwa kufanya kampeni

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by PayGod, Sep 29, 2010.

 1. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #1
  Sep 29, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Na FRANCIS GODWIN (MZEE WA MATUKIO)

  [​IMG]
  Msafara wa mtoto wa Rais Jakaya Kikwete Bw Ridhiwan Kikwete ukiondoka katika shule ya msingi Ipogolo baada ya kikao chao cha vijana shule hapo kushindikana leo
  [​IMG]
  Mkuu wa shule ya msingi Ipogolo Aman Mkeremi akiomba msamaha kwa wafuasi wa Chadema kwa hatua yake ya kuruhusu CCM kufanya kampeni shuleni

  [​IMG]
  Darasalililoandaliwa kwa ajili ya kampeni za CCM hili hapa

  [​IMG]
  Mwanafunzi wa shule ya msingi Ipogolo akiwa nje ya ofisi baada ya walimu kujifungia ndani

  MTOTO wa mgombea urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Jakaya mrisho Kikwete ,Ridhiwan Kikwete leo ameonja joto la jiwe katika ziara zake za kampeni ndani ya CCM baada ya kutimuliwa mbio zaidi ya mara moja wakati akitaka kufanya kampeni za CCM katika taasisi za umma.

  Ridhiwani ambaye ni mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya baraza kuu la umoja wa vijana wa chama cha mapindunzi (UVCCM) Taifa akiwa na viongozi akiwemo aliyekuwa mshindi wa kura za maoni jimbo la Iringa mjini Frederick Mwakalebela na washiriki wengine wa kura za maoni kama Jescar Msambatavangu walifika katika shule ya msingi Ipogolo wakitaka kukutana na vijana wa eneo hilo ili mjumbe huyo aweze kumuunganisha mgombea ubunge wa jimbo hilo Monica Mbega na Mwakalebela japo mkakati huo uligonga ukuta.


  Kabla ya msafara wa Ridhiwan kufika shuleni hapo kwa ajili ya kikao chake cha ndani ya vijana wa CCM kwa lengo la kuvunja makundi ndani ya chama hicho ,aliyekuwa mmoja kati ya wana CCM 12 walioingia katika kinyang'anyiro cha ubunge jimbo hilo Msambatavangu alipita mitaani kujaribu kuwaomba vijana kwenda kumsikiliza mtoto huyo wa Rais Kikwete japo waligoma kwa madai kuwa hawadanganyiki na ujio wake.


  Hata hivyo baada ya vijana hao wa vijiweni kugoma kwenda katika shule hiyo kwa ajili ya kutana na mjumbe huyo kwenye chumba cha darasa la pili katika shule hiyo ya msingi Ipogolo bado msafara huo uliweza kufika katika eneo hilo kwa ajili ya mkutano japo idadi ya vijana waliokuwa wamefika ilikuwa ni kama vijana 10 pekee.
   
 2. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #2
  Sep 29, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Dah Safi sana wanyaluuuu, pale Ipogoro napafahamu sana tuu, ule uwanja wa shule ya Msingi Ipogolo nishapiga sana boli pale 1991 - 1995 na timu yetu ya Ruaha shooting wakat huo ikiwa ligi daraja la tatu.

  Hii inaonesha wazi kabisa sasa mwisho wa CCM ndo huooo. halafu huyu ridhwani asituyeyushe nchi yetu siyo ya kifalme, haturithishani uongozi.

  Naona dogo ana mamlaka makubwa sana sasa hivi, asitufanye sie mabwege, tunaona yote anayoyafanya.
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Sep 29, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,136
  Trophy Points: 280
  Tanzania will never accommodate "dynasty" politics
   
 4. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #4
  Sep 29, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  yule dogo ni mpuuzi sana hakana akili kabisa

  safi sana
   
 5. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #5
  Sep 29, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  mzee wa matukio safi sana kwa kuleta matukio kama haya

  sijui alielekea wapi baaday ahii dharuba
   
 6. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #6
  Sep 29, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  aaaah head tichaaaaaaaa unanipa raha sana ...kwa hali hiyo bado unaona chichiemu ni baba na wanakuboreshea maisha..hahaaaa.God Forbid
   
 7. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #7
  Sep 29, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  la msingi ni kumuondoa huyu kiwete ooops! kikwete pale ikulu maana anaweza kuigeuza ikulu ndo familia yake ilipo

  hana maana kabisa huyu mzee na tuna bahati huyu mtoto sio mwanajeshi maana gafla mngesikia ndo mkuu wa majeshi
   
 8. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #8
  Sep 29, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  watoto wetu tunataka wasome yeye ni nani anakwenda huyu riziwani

  nyambafu kabisa.

  kikwete ndo ataibomoa ccm. kikwete,riziwani na salma ni watu wa ovyo sana. huwezi kumtuma mwanao aende kuvunja makundi.kwani wakati kiwete anapita iringa kukampeni hakuliona hili?
   
 9. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #9
  Sep 29, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Vijana wetu wameonyesha kukomaa. Riziwani ni nani nchi hii?
   
 10. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #10
  Sep 29, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,202
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280
  Undai bado anauota utawala wa kifalme. Halafu bana mtu akiwa wa upande huu wa mama mdogo huwa hata akiwa kasoma haelimiki. Haka kaundai kanawalazimisha watendaji wa serikali kuvunja sheria na kanuni za uchaguzi maana kanaota kako juu ya sheria. Sasa kamekutana na watanzania ambao hawadanganyiki.
   
 11. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #11
  Sep 29, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Safi sana hao wanataka kuanzisha mbinu za uchakachuaji wa kura, safari hii hawaambulii kitu
   
 12. Sidanganyiki10

  Sidanganyiki10 Member

  #12
  Sep 29, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 93
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mbona hii habari ni kama haijakamilika!Kama ni kweli vijana wa Iringa wanastahili pongezi.Kwa kweli hatuhitaji vi family trinity kutuongezea umasikini.
   
 13. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #13
  Sep 29, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  Mtoto wa rais ana akili ndogo.
   
 14. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #14
  Sep 29, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  Kila kitu kinachiohusu kuvamia munakihusisha na Chama chetu Chadema. Acheni upunguani.

  Huyo Rizwani kavamiwa na Watanzania.

  Acheni uzushi wenu.
   
 15. u

  urasa JF-Expert Member

  #15
  Sep 29, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  angalia magari ya msafala wake yalivyo ya kifahari,then linganisha na hali ya mwl mkuu na mazingira ya kujifunzia ya shule hiyo,hili ni somo kwa walimu na watanzania kwa ujumla hii familia inaendekeza anasa na si kujali kero za wa tz
   
 16. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #16
  Sep 29, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  kwa nini hawakumvunja taya bawazazi huyu? yeye anatanua na mashangingi ya ikulu wakati wenzake wanashindia ulanzi
   
 17. KAZIMOTO

  KAZIMOTO JF-Expert Member

  #17
  Sep 29, 2010
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 1,073
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni mtoto wa Rais
   
 18. KAZIMOTO

  KAZIMOTO JF-Expert Member

  #18
  Sep 29, 2010
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 1,073
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kampeni za Ridhwan zinawauma sana chadema. kama hazina manufaa kelele zote za nini?
   
 19. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #19
  Sep 29, 2010
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  source bwana!!!! Habari kama hazina rejea hutupwa kapuni!!!!
   
 20. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #20
  Sep 29, 2010
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Wanyalu mmeonyesha spirit ya Chief Mkwavinyika wakati anawakataa wakoloni, hasa alipomdondosha kamanda wa wajerumani Emil Von Zelewisky pale Lipuli.... Naskia raha naona kama ukombozi wa nchi yetu umekaribia vile..... Kazi nzuri my brothers and sisters... nilidhani mtatia aibu kama akina Mwakifulefule, Mwakyusa, Mwandosya, Mwankusye, Malakasyuka, Mwamfupe, Mwamsojo, Mwampulule, Mwakisole, Mwamjinga, Mwampumbavu.... hawa jamaa wanyakyusa wameushangaza ulimwengu kwa kumpa Riizi wani uchief wa wanyakyusa, eti riizi wani ni malafyale kule kwao, lakini wanyalu mmesimama kidete na kulinda uhuru wa kabila lenu na kazi nzuri ya Mkwawa pale lipuli...
   
Loading...