Kana-Ka-Nsungu
JF-Expert Member
- Oct 4, 2007
- 2,257
- 349
Wataalamu wa maswumbwi wamelibatiza pambano hili la ubingwa wa dunia uzito wa junior welterweight kati ya Ricky Hatton (43-0,31 KOs) na Floyd Mayweather(38-0,24 KOs) kwa jina la "UNDEFEATED". Nimeusubiri sana mpambano huu na thanks God, tarehe 8 December ndio hiyo inakaribia tujue mbabe nani. Unadhani nani atashinda? na mshindi atashinda vipi na kwa nini? Binafsi naamini style ya Ricky ya "pressure- pressure" toka mwanzo hadi mwisho na physical stenght yake itakua tatizo kwa Floyd. Mayweather ana ngumi za chapchap na ni mwepesi sana kuliko Ricky, lakini sina hakika kama amewahi kuzichapa na mtu yeyote mwenye style kama ya Ricky. Sioni uwezekano wa Mayweather kum knock out Hatton kwa kuwa sio "power puncher" kama Kotsya Tszyu ambaye alijaribu na kushindwa. Siamini speed ya Mayweather itamfikisha mbali kama anavyotaka katika mpambano huu, Hatton atakuja na style ambayo itampunguza kasi, itamchosha na mwishowe atammaliza. Hatton is like a bull. As you can probably imagine by now, I choose Hatton to win by late TKO. What is your opinion and prediction on this?