Richmond Tanzania kufutwa rasmi leo

Ochu

JF-Expert Member
May 13, 2008
975
47
Richmond Tanzania kufutwa rasmi leo

*Siku 30 zimekwisha, notisi kutolewa leo

Na Ramadhan Semtawa

KAMPUNI ya Richmond Tanzania Limited inatarajiwa kufutwa rasmi katika orodha ya makampuni iliyo katika Ofisi ya Wakala wa Usajili wa Makampuni na Majina ya Biashara (Brela), kutokana na kushindwa kujibu notisi ya siku 30 ya kujitetea.

Uamuzi huo ni sehemu ya hatua za serikali kutekeleza azimio namba 17 la Bunge, ambalo lilitaka Richmond Development (LLC) ifutwe. Lakini ilibainika baadaye kuwa kampuni hiyo ilikuwa Marekani na iliyopo katika orodha ya Brela ni Richmond Tanzania Limited.

Taarifa kutoka Brela, ambazo zimethibitishwa na Afisa Mtendaji Mkuu, Estariano Mahingila, zinasema Richmond Tanzania LTD, ambayo iliandikiwa notisi ya siku 30 tangu mwezi Julai, hadi sasa haijawasilisha majibu na muda huo sasa umekwisha.

Mahingila alifafanua kuwa Richmond Tanzania LTD, ambayo kashfa ya kupewa zabuni ya ufuaji umeme wa dharura ilisababisha mtikisiko katika serikali ya awamu ya tatu kiasi cha Waziri Mkuu Edward Lowassa kuachia ngazi, imepoteza sifa za kuwa kampuni kutokana na kuwa na mwanahisa mmoja.

Mahingila alifafanua kuwa hatua ya Richmond Tanzania LTD kupoteza sifa kwa kuwa na mwanahisa mmoja kunatokana na Brela kujiridhisha kwamba mwanahisa mwingine, ambaye ni Kampuni ya Richmond Development (LLC) haipo.

Mkuu huyo wa Brela aliweka bayana hilo akisema baada ya Richmond kushindwa kujibu notisi ya siku 30, leo Brela inatoa notisi ya siku 15 ambayo ni kutaarifu upande wa tatu (third part) ambao ni kuona kama kuna watu wamekuwa na uhusiano wa kibiashara na kuwaeleza azma hiyo ya kufutwa usajili.

Mkuu huyo wa Brela aliongeza kwamba taratibu ziko bayana, kwamba ili kampuni iweze kusajiliwa au kuwa hai inapaswa kuwa na wanahisa kwa kiwango kuanzia wawili.

Alisema baada ya kubaini LLC haipo, Richmond Tanzania LTD imebaki na mwanahisa mmoja, hivyo kupoteza sifa za kuwa kampuni.

Kwa msisitizo, Mahingila alisema Brela katika notisi ya awali kwa Richmond Tanzania LTD, ilieleza bayana kupoteza sifa hiyo kutokana na mwanahisa mmoja (LLC) kutokuwepo, hata hivyo, imeshindwa kujibu.

Brela katika kumbukumbu zake inaonyesha kuwa Kampuni ya Richmond Tanzania LTD, ilisajiliwa Julai 13, 2006 ikiwa na wanahisa wawili ambao ni LLC na Naeem Gire.

Katika mchanganuo huo wa hisa, Gire anamiliki hisa 250,000 na LLC ilikuwa inamiliki hisa 750,000 huku ikiwa imeanza na mtaji wa sh 1,260,000,000 (1.2 bilioni).

"Tuliwapa notice ya siku 30, lakini hawajajibu, kwa hiyo sasa tunatoa notisi ya siku 15 kwa ajili ya kuarifu third part (upande mwingine wenye uhusiano na kampuni hiyo), ili kama wana madai au pingamizi wajue kwamba, kampuni tunaifuta," alifafanua Mahingila, na kuongeza:

"Kampuni imepoteza sifa kwa kuwa na mwanahisa mmoja. Tulieleza hilo kwamba baada ya uchunguzi tumeridhika LLC haipo, sasa kwa kawaida wanahisa wanapaswa kuwa wawili.

"Notisi tutatoa Jumatatu (leo) na baada ya hapo kama hakuna pingamizi kutoka upande huo, basi tutaifuta mara moja."

Sakata la Richmond lilitikisa nchi hasa wakati wa mkutano wa 10 wa Bunge la mwezi Februari, baada ya Kamati Teule ya Bunge kuwasilisha ripoti yake ya uchunguzi kuhusu kashfa hiyo.

Baada ya kamati hiyo kutoa majibu na kuja na mapendekezo 16, Bunge liliijadili na kutoa mapendekezo zaidi ya saba ambayo yalifanywa kama maazimio 23 na Bunge lilitoa miezi sita kwa serikali iweze kuyatekeleza.

Hata hivyo, katika mkutano wa 14 wa Bunge uliomalizika, pamoja na mapendekezo mengine Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alisema Richmond Tanzania LTD ilipewa notisi ya siku 30 na Brela ambazo zilikuwa hazijakwisha.

Pinda alifafanua kwamba, RDC haikusajiliwa Brela na kuongeza kwamba, hata hivyo, serikali ilitoa maelekezo kwa wakala huyo iifute Richmond T (LTD).

Kuhusu kama RDC ilighushi nyaraka na kupata zabuni hiyo, alisema jinai huchunguzwa na polisi na kwamba tayari jeshi hilo linachunguza kuona kama wamiliki walifanya kosa hilo la jinai kupata zabuni.

Sakata la upungufu wa umeme lilitikisa nchi kuanzia Juni mwaka 2006, miezi michache baada ya serikali ya awamu ya nne kuingia madarakani na juhudi za kulitatua ilisababisha kutafutwa kwa kampuni ambayo ingeweza kufua umeme wa dharura.

Mpango huo ndio uliozaa kashfa ya Richmond baada ya kampuni hiyo kupewa zabuni katika mazingira tatanishi.


source: mwananchi
 
Richmond kupewa siku 15 ifutwe




WAKALA wa Usajili na Makampuni na Majina ya Biashara (BRELA) inakusudia kutoa notisi ya siku 15 kwa wenye pingamizi dhidi ya kufutwa kwa kampuni ya Richmond.

Hatua hiyo imekuja baada ya kampuni hiyo kushindwa kujibu notisi ya siku 30 waliyopewa na BRELA ya kuifuta.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Brela, Bw. Estariano Mahingila, alisema jana Dar es Salaam kuwa notisi hiyo ya siku 15 inatarajiwa kutolewa siku yoyote kuanzia sasa.

Bw. Mahingila alisema tangu kampuni hiyo iandikiwe notisi ya siku 30 ya kujitetea tangu Julai mwaka huu hadi sasa, haijawasilisha majibu na muda huo, sasa umekwisha.

Alisema Richmond imepoteza sifa kwa kuwa na mwanahisa mmoja kunatokana na BRELA kujiridhisha, kwamba mwanahisa mwingine ambaye ni Kampuni ya Richmond Development (LLC) haipo.

"Baada ya kumalizika kwa siku 30 tangu BRELA itoe notisi kwa Richmond na kushindwa kuijibu, sasa tunatarajia siku yoyote kutoa notisi ya siku 15 ya kutaarifu upande wa tatu, ili kama kuna watu wamekuwa na uhusiano wa kibiashara na kuwaeleza azma hiyo hiyo ya kufutiwa usajili," alisema

Alisema taratibu zote ziko bayana, kwamba ili kampuni iweze kusajiliwa au kuwa hai, inapaswa kuwa na wanahisa kwa kiwango kuanzia wawili.

Bw. Mahingila alisema baada ya kubaini LLC haipo, Richmond Tanzania Ltd imebaki na mwanahisa mmoja, hivyo kupoteza sifa za kuwa kampuni na kwamba katika notisi ya awali kwa kampuni hiyo, ilieleza bayana kupoteza sifa hiyo kutokana na mwanahisa mmoja LLC kutokuwapo, hata hivyo imeshindwa kujibu.

Alisema baada ya notisi hiyo ya siku 15 kutolewa kama kutakuwa hakuna pingamizi kutoka upande huo, Richmond itafutwa.

Bw. Mahingila alisema kwamba hajasema kuwa kampuni ya Richmond inafutwa jana kama ambavyo chombo kimoja cha habari kimeripoti bali alisema kuwa watatoa notisi ya siku 15 kwa ajili ya kuarifu upande mwingine wenye uhusiano na kampuni hiyo, ili kama wana madai au pingamizi watoe kabla ya kuchukuliwa kwa uamuzi wa kufutwa.

Katika kumbukumbu za BRELA, inaonesha kuwa Richmond ilisajiliwa Julai 13, 2006 ikiwa na wanahisa wawili ambao ni LLC na Naeem Gire, ambapo Gire anamiliki hisa 250,000 na LLC hisa 750,000 huku ikiwa imeanza na mtaji wa sh. bilioni 1.2.
 
richmond kupewa siku 15 ifutwe




wakala wa usajili na makampuni na majina ya biashara (brela) inakusudia kutoa notisi ya siku 15 kwa wenye pingamizi dhidi ya kufutwa kwa kampuni ya richmond.

Hatua hiyo imekuja baada ya kampuni hiyo kushindwa kujibu notisi ya siku 30 waliyopewa na brela ya kuifuta.

Ofisa mtendaji mkuu wa brela, bw. Estariano mahingila, alisema jana dar es salaam kuwa notisi hiyo ya siku 15 inatarajiwa kutolewa siku yoyote kuanzia sasa.

Bw. Mahingila alisema tangu kampuni hiyo iandikiwe notisi ya siku 30 ya kujitetea tangu julai mwaka huu hadi sasa, haijawasilisha majibu na muda huo, sasa umekwisha.

Alisema richmond imepoteza sifa kwa kuwa na mwanahisa mmoja kunatokana na brela kujiridhisha, kwamba mwanahisa mwingine ambaye ni kampuni ya richmond development (llc) haipo.

"baada ya kumalizika kwa siku 30 tangu brela itoe notisi kwa richmond na kushindwa kuijibu, sasa tunatarajia siku yoyote kutoa notisi ya siku 15 ya kutaarifu upande wa tatu, ili kama kuna watu wamekuwa na uhusiano wa kibiashara na kuwaeleza azma hiyo hiyo ya kufutiwa usajili," alisema

alisema taratibu zote ziko bayana, kwamba ili kampuni iweze kusajiliwa au kuwa hai, inapaswa kuwa na wanahisa kwa kiwango kuanzia wawili.

Bw. Mahingila alisema baada ya kubaini llc haipo, richmond tanzania ltd imebaki na mwanahisa mmoja, hivyo kupoteza sifa za kuwa kampuni na kwamba katika notisi ya awali kwa kampuni hiyo, ilieleza bayana kupoteza sifa hiyo kutokana na mwanahisa mmoja llc kutokuwapo, hata hivyo imeshindwa kujibu.

Alisema baada ya notisi hiyo ya siku 15 kutolewa kama kutakuwa hakuna pingamizi kutoka upande huo, richmond itafutwa.

Bw. Mahingila alisema kwamba hajasema kuwa kampuni ya richmond inafutwa jana kama ambavyo chombo kimoja cha habari kimeripoti bali alisema kuwa watatoa notisi ya siku 15 kwa ajili ya kuarifu upande mwingine wenye uhusiano na kampuni hiyo, ili kama wana madai au pingamizi watoe kabla ya kuchukuliwa kwa uamuzi wa kufutwa.

Katika kumbukumbu za brela, inaonesha kuwa richmond ilisajiliwa julai 13, 2006 ikiwa na wanahisa wawili ambao ni llc na naeem gire, ambapo gire anamiliki hisa 250,000 na llc hisa 750,000 huku ikiwa imeanza na mtaji wa sh. Bilioni 1.2.
nonesense sasa mtu kesha vuna ndio mnamfuta kwanza ndio mnazidi kumpa kwani anual tax return hawezi kurudisha wala corporation tax yaani watu utadhani wanfanya makusudi vile
 
Back
Top Bottom