Richmond nyingine yazimwa Tanesco | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Richmond nyingine yazimwa Tanesco

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Halisi, Dec 22, 2009.

 1. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145


  Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 22nd December 2009

  MCHAKATO wa kutafuta wazabuni kwa ajili ya kununua mitambo miwili ya kuzalisha umeme wa jumla ya megawati 160 itakayowekwa Dar es Salaam na Mwanza, imebidi urudiwe baada ya kubainika kwamba tathmini iliyofanywa haikuzingatia vigezo muhimu.

  Mitambo hiyo inayotarajiwa kununuliwa na ambayo serikali imetoa miezi mitatu kwa mchakato wa kuinunua uwe umekamilika, ni megawati 100 utakaowekwa Dar es Salaam na wa megawati 60 utakaokuwa Mwanza.

  Miongoni mwa vigezo ambavyo havikuzingatiwa, ni kile ambacho Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja alisema ni kutojumuishwa kwa ukamilifu gharama za uendeshaji, kwa mtambo wa megawati 60, ambazo kwa wastani ni kubwa.

  “Pamoja na maelezo na ufafanuzi uliopatikana kwa barua na kupitia vikao kadhaa wizarani, ilikubalika kuwa tathmini ya Tanesco (Shirika la Umeme Tanzania) haikuzingatia vigezo vingine muhimu vya zabuni,” Ngeleja alisema jana Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari.

  Alisema uamuzi wa kurudia mchakato wa zabuni huo, umeepusha pia mwanya wa kuingiza mambo mengine ambayo hayakustahili katika kufanikisha suala hilo.

  Mwaka 2006, wakati wa ukame nchini, serikali iliagiza mitambo ya dharura ya kufua umeme nchini, ambayo baadaye ilikuja kugundulika kuwepo na ukiukwaji wa taratibu katika uingizwaji wake na kuzaa kile ambacho kwa sasa ni maarufu kama sakata la Richmond, moja ya kampuni zilizoshinda zabuni za kuleta mitambo hiyo.

  Ngeleja ambaye hata hivyo alisisitiza kwamba siyo uzembe wa Tanesco, alisema kwa kuzingatia umuhimu wa kupatikana mitambo hiyo haraka, shirika limeshauriwa kutumia vipengele muafaka chini ya Sheria ya Ununuzi wa Umma ya 2004 kuanza mchakato mara moja na kupata mkandarasi ndani ya miezi mitatu kuanzia sasa.

  Alisema, “Serikali imeamua ni busara zabuni kurudiwa kwa kuwataka wazabuni wote waliofuzu kwenye mchujo na kuthibitika kuwa wana uwezo wawasilishe takwimu za kuwezesha kufanyika thathmini ya gharama za ununuzi wa mitambo, ujenzi na uendeshaji.”

  Akielezea kilichojiri katika zabuni hiyo ya awali ambayo haikupitishwa, Ngeleja alisema kwa kuzingatia gharama za uendeshaji wa mitambo ya uzalishaji umeme, Tanesco iliishauri serikali ifikirie na kufadhili ununuzi wa mitambo hiyo ya Mwanza na Dar es Salaam.

  Serikali ilikubali kulipia gharama za kuinunua. Aprili 21, mwaka huu, ilitangazwa zabuni kupitia magazeti huku makisio ya Tanesco kuhusu gharama za miradi hiyo ikiwa takribani Sh bilioni 267.

  Tarehe ya mwisho ya kurudisha makabrasha ya zabuni Tanesco, ilikuwa Juni 6, mwaka huu, lakini muda ukaongezwa hadi Julai 3, ili kutoa muda wa kutosha kwa wazabuni kukamilisha makabrasha husika.

  Ngeleja alisema wazabuni 30 walinunua makabrasha ya zabuni kwa ajili ya mitambo ya Dar es Salaam na wazabuni 28 kwa ajili ya mitambo ya Mwanza.

  “Hata hivyo waliorudisha makabrasha yaliyokamilika kujazwa walifikia watano kwa mitambo ya Dar es Salaam ya megawati 100 na wanne kwa mitambo ya megawati 60,” alisema na kuongeza kuwa matokeo ya tathmini ya zabuni yaliwasilishwa wizarani Septemba 10, mwaka huu.

  Baada ya kutafakari ripoti ya Tanesco, Ngeleje alisema Oktoba 4, mwaka huu, wizara iliomba ufafanuzi kutoka shirika hilo kuhusu masuala kadhaa hasa gharama za uendeshaji zikiwemo mafuta na vipuri kwa umri wa mitambo unaokisiwa kuwa wa miaka 30.

  Kwa upande wa mitambo ya Dar es Salaam, alisema zabuni ya Tanesco ilielekeza kuhitajika mitambo ya megawati 100 ya kutumia gesi asili, lakini mzabuni aliyependekezwa angeleta mitambo yenye uwezo wa megawati 130, kiasi ambacho hakikuwa katika makadirio ya bajeti, jambo lililochangia pia zabuni kurudiwa.

  Alipoulizwa na waandishi wa habari iwapo kulikuwa na uzembe ndani ya Tanesco kiasi cha kushindwa kubaini kasoro hizo, Ngeleja alisema ni upungufu wa kawaida.

  Aidha, alisisitiza mitambo hiyo italetwa mara moja baada ya kipindi hicho cha miezi mitatu kilichotolewa.

  Alisema haitasubiri kuleta mitambo yote kwa pamoja; badala yake, itakayokuwa imekamilika hata ikiwa michache italetwa mara moja.

  Uamuzi wa kuleta mitambo hiyo ya megawati 160, ulitokana na tathmini iliyofanywa na Tanesco mwanzoni mwa mwaka huu kuhusu hali ya uzalishaji wa umeme nchini. Ilithibitika kuwa mfumo wa uzalishaji umeme haukidhi mahitaji na kwamba unahitaji megawati zisizopungua 160 haraka iwezekanavyo.

  Katika hatua nyingine, Waziri Ngeleja aliwaambia waandishi wa habari kwamba hali ya upatikanaji wa bidhaa za petroli unaridhisha na usambazaji wake unaendelea vizuri.
  Ilianza hivi:

  A new Richmond is coming...


  THISDAY REPORTER
  Dar es Salaam

  CERTAIN businessmen-cum-politicians implicated in the infamous Richmond deal are now chasing up two brand-new contracts worth more than $100m (approx. 140bn/-) from the state-run Tanzania Electric Supply Company (TANESCO) for the construction of power generating plants in Dar es Salaam and Mwanza, THISDAY can reveal today.

  The two separate energy contracts involve the procurement of a 100-megawatts, gas-fired power plant at Ubungo in Dar es Salaam, and the purchase of a 60MW power plant in Nyakato, Mwanza, which will run on heavy fuel oil.

  Government officials have confirmed that the same people said to be behind the 2006 Richmond scandal are now well-positioned to be awarded the contracts using a different company name.

  TANESCO received bids for both projects in June this year, but the tender process has since been shrouded in apparent secrecy and controversy.

  It is understood that the group of Richmond-tainted businessmen-cum-politicians, working as a syndicate of sorts, submitted bids for the two contracts under another company name, ostensibly in an attempt to hide the identities of the real owners of the firm.

  The 'syndicate' is said to be using the same network of government officials who facilitated the Richmond deal, to ensure it stays ahead in the race to land the latest contracts.

  "A new Richmond is coming...," a senior government official familiar with the latest TANESCO tenders told THISDAY.

  According to government insiders, the bids submitted by the 'syndicate' for the contracts were inflated by more than $30m (approx. 40bn/-).

  "These people received inside information on the tenders, and submitted bids for both. In fact, there are reports going around that both contracts have already been awarded to the same people who were behind the Richmond scandal," said the senior government official.

  The 'syndicate' is said to have been doing lots of behind-the-scenes maneuvering since early this year to land the new contracts.

  "These people have the audacity and dastardly courage to repeat the same methods of fraud, misrepresentation of facts, bribery and what-have-you that they deployed to secure the Richmond contract, this time around as well," said the government official.

  Under tender number PA/001/09/HQ/W/016, TANESCO invited bids for the "supply, installation, testing and commissioning" of the emergency,gas-based 100MW power generation plant in Dar es Salaam, on a turn-key basis.

  A turn-key project is a type of project that is constructed by a developer and sold or turned over to a buyer (in this case, TANESCO) in a ready-to-use condition.

  On the other hand, tender number PA/001/09/HQ/W/018 involves the supply, installation, testing and commissioning of a 60MW power plant in Nyakato, Mwanza, that will use dual-heavy fuel oil for power generation. The proposed Mwanza power plant is also a turn-key project.

  According to our government sources, the bid winner(s) for both projects was expected to be picked on the basis of experience, technical capacity, fulfillment of tender requirements, and other such aspects.

  “But the word is now out that the one company already awarded both contracts...has never worked in Tanzania before, nor does it have any power generation experience in the whole of Sub-Saharan Africa," the sources said.

  Contacted for comment, the Minister for Energy and Minerals, William Ngeleja, asserted that the TANESCO tender board is still in the process of assessing bids from various companies for the two tenders, and no formal decision has been made so far on the bid winner or winners.

  “It's too early to comment on this matter now because the tender process is still in the early stages...," the minister told THISDAY.

  The official deadline for submission of bids for the two tenders expired on June 5 this year, meaning that TANESCO has been processing the bids for almost six months now.
  Source: THISDAY, November 30, 2009

   
 2. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #2
  Dec 22, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Nini kinawazuia kuwataja wote walio-submit tenda na wale ambao tenda zao zimekubaliwa ? Wakati wa kufungua tenda vyote hivi vinasomwa wazi. Na wale ambao tenda zao zimekataliwa ziwekwe wazi. Hakuna haja ya siri.

  Amandla.......
   
 3. b

  bigilankana Senior Member

  #3
  Dec 22, 2009
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 143
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mzabuni ambaye Ngeleja alimtaka ameenguliwa. Hii kitu ni kama ile ya vitambulisho vya Taifa na Ngeleja hapa kawa kama Masha. Mwandishi ameripoti kama kasuku bila kuhoji kwa ndani.
  Wizara haina mamlaka na zabuni ya taasisi iliyo chini yake katika mchakato na hawana mamlaka ya kuagiza zabuni kurudiwa isipokuwa PPRA.

  Muhimu kujua mzabuni wa Ngeleja alikuwa nani?
   
 4. b

  bigilankana Senior Member

  #4
  Dec 22, 2009
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 143
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sources familiar with the tenders say five companies submitted proposals for the construction and sale to TANESCO of the 100MW power plant in Dar es Salaam; Aaneen Power Cooperating of Canada, Jacobsen Elektro (Norway), Wartsila (Finland), Kolon & Samsung (South Korea), and China National (China).

  China National apparently submitted the highest project cost proposal of $149.5 million (approx. 200bn/-), while Jacobsen Elektro proposed the second-highest project costs at 95,711,730 euros (approx. 193bn/-).

  Aaneen Power Cooperating submitted a bid of 94.95 million euros (approx. 191.7bn/-), followed by Kolon & Samsung's bid of around 133bn/-. Wartsila's proposed project cost is 62.5 million euros (approx. 126bn/-)

  On the other hand, according to the sources, four bidders submitted proposals for the 60MW power plant slated for Mwanza. They are Germany's MAN Diesel with a bid of 77.6 million euros (approx. 156.6bn/-); Wartsila again with 49.8 million euros (approx. 100bn/-); Egypt's UNATRAC with 67,681,467 euros (approx. 136.6bn/-); and Semco Maritime/Rolls Royce Marine of Norway with a bid of approximately 102bn/-.

  Hapo juu kuna kampuni ambayo Ngeleja kahongwa au kaahidiwa kuhongwa na imetupwa nje ya zabuni. Kuwarudisha wote ni mtindo aliotaka kutumia Masha kwenye Vitambulisho na waandishi wa habari wakashughulika vya kutosha akashindwa. Katika hili pia Vyombo vya habari makini kama Raiamwema vifuatilie ili kumzuia huyu bwana mdogo kuturudisha Richmond.

  PPRA waulizwe kama uamuzi wa wizara ni sahihi?
   
 5. b

  bigilankana Senior Member

  #5
  Dec 22, 2009
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 143
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Re-float tender, Tanesco told[​IMG]The minister of Energy and Minerals, Mr William Ngeleja, addresses reporters in Dar es Salaam yesterday on power tender issues. Right is his deputy Mr Adam Malima.By Tumsifu Sanga

  The Government has ordered the Tanzania Electricity Supply Company (Tanesco), to re-float tenders for production of 100MW for Dar es Salaam and 60MW for mwanza.

  The minister for Energy and Minerals, Mr William Ngeleja, told reporters in Dar es Salaam yesterday that the decision was reached after it was established that analysis done by Tanesco after receiving some tenders, were nor done properly.

  He said after receiving the go ahead from the Government, Tanesco floated tenders for the production of 160MW and several companies applied.

  However, he said, an analysis on the 60MW power plant for Mwanza, Tanesco overlooked a key aspect of running cost, which are huge and could impact on the implementation of the project if it is not included from the initial stages.

  He said the Government has ordered Tanesco to contact those who had applied and were pre-qualified to present fresh data indicating their ability to purchase, install and maintain the generators.

  "It has been established that analysis done by Tanesco experts did not look into all important aspects of the tenders," he said.

  Mr Ngeleja said Tanesco was required to take into consideration the running cost for Mwanza generators whose capacity is to produce 60MW.

  He said Tanesco was also supposed to verify that the bidder was capable of installing generators with life span of 30 years.

  He said public utility firm had estimated to use $80 million for the 60MW plant and $120 million for the Dar es Salaam 100MW generators, making the total cost of the two generators $200 million or about Sh267 billion.

  Mr Ngeleja told reporters that some 30 companies took documents for the Dar es Salaam tender and 28 others showed interest for the Mwanza power plant.

  However, those who returned tender documents were five for Dar generators and four for the Mwanza plant.

  Mr Ngeleja urged Tanesco to expedite the process and adhere to the 2004 Public Procurement Act.

  He said the Government agreed to the two tenders early this year after Tanesco own analysis indicated that there was a need for 160MW to supplement the current power production.

  kuna kitu hapa kinafichwa katika hii zabuni. Ama serikali inataka wachelewe ili kununua dowans maana miradi hii ilikuwa ni ya haraka kama tulivyoambiwa. Au kama nilivyosema awali kampuni yao imekosa.

  Tittle kutokana na habar za nyuma za thisday na kulikoni iwe NGELEJA ALILIA RICHMOND yake.

  Maana kusema imezimwa ni kana kwamba ngeleja ndio kazima wakati yeye ndio anataka mzabuni wake.

  Hii ni Masha style
   
 6. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #6
  Dec 22, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Swali ni kuwa kama vyote hivi vilikuwemo katika matakwa ya tenda. Na kama havikuweko, kwa nini havikuweko? Kwani ilikuwa tenda ya kununua vitunguu! Hatuwezi kuhamisha magoli katikati ya mechi.

  Amandla.....
   
 7. b

  bigilankana Senior Member

  #7
  Dec 22, 2009
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 143
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapo sasa. na watanzania na hasa waandishi wanaandika walichoambiwa tu na ngeleja
   
 8. H

  Hume JF-Expert Member

  #8
  Dec 22, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 338
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  Miongoni mwa makosa waliyotuhumiwa nayo Lowassa na Karamagi ni kuingilia utaratibu wa zabuni ya Tanesco.
  Hivi ngeleja haoni kwamba anafuata mkondo uliowaondoa wenzie?
   
 9. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #9
  Dec 22, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Pamoja na kupinga kusogeza magoli katikati ya mechi lakini ni muhimu mwaliko wa tenda uangaliwe kama uliandaliwa kukidhi maslahi ya taifa letu. Maswali aliyouliza waziri ni ya muhimu lakini yalitakiwa kuulizwa kabla ya tenda kutangazwa. Na kama haikuwa hivyo basi tenda irudiwe.

  Amandla........
   
Loading...