Richmond mtihani mgumu kwa Pinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Richmond mtihani mgumu kwa Pinda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jun 22, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jun 22, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,094
  Trophy Points: 280
  Richmond mtihani mgumu kwa Pinda
  Monday, 22 June 2009 07:44
  *Nyumba za Serikali donda jipya
  *Mikataba ya TICTS,TRL yafukuta
  *Wabunge sasa wachoshwa misamiati
  *Wadai kuna mazingaombwe, usanii

  Na John Daniel, Dodoma
  Majira

  WAKATI Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, anawasilisha bajeti ya ofisi yake leo, wabunge wamesema hawana maswali kwa hilo bali wanamsubiri atakapowasilisha utekelezaji wa Serikali juu ya maazimio ya Bunge kuhusu sakata la Richmond.

  Sambamba na hilo, wabunge hao wamesema pia wanangoja kusikia majibu yasiyo na utata kutoka kwa Kiongozi huyo wa Shughuli za Serikali Bungeni kuhusu hoja za uuzaji holela nyumba za Serikali, mkataba tete wa Kampuni ya Kupakua Mizigo Bandarini(TICTS) na ule wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL).

  Wabunge hao ambao walizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, wamesema hoja hizo zinaisumbua Serikali na hata kukiweka chama tawala CCM kwenye wakati mgumu.


  Mmoja wa wabunge hao alisema wananchi wamekuwa wakihoji masuala hayo lakini majibu yanayotolewa na viongozi, hayatoshelezi hivyo wanachohitaji sasa ni kusikia kutoka kwa Bw. Pinda muafaka wa kudumu wa hoja hizo. Taarifa ya Richmond inatarajiwa kuwasilishwa bungeni mwezi ujao.

  "Mimi hadi nawaogopa wananchi wangu, nikirudi jimboni naulizwa, Richmond mmefikia wapi, nasema linafanyiwa kazi taarifa itatolewa wananiuliza lini? Natafuna maneno. Sasa Waziri Mkuu hili alitolee ufafanuzi nisije nikapoteza jimbo wale watu wana akili sana, wanafuatilia mambo na wanataka kujua matokeo" alisema Mbunge mmoja wa Kanda ya Ziwa na kuomba kuhifadhiwa jina.

  Mbunge huyo alizidi kueleza "Najiuliza haya ni mazingaombwe au usanii? Tuliambiwa Richmond wanalipwa mamilioni kwa siku, juzi Waziri anasimama anasema hawajalipwa hata senti tano nini hii! Ukweli uko wapi?" Alihoji Mbunge huyo na kusisitiza kuwa Waziri Mkuu lazima aweke wazi suala hilo.

  Aliongeza kuwa uuzwaji holela wa nyumba za Serikali ambao umelalamikiwa na wananchi wengi nao ni shughuli nyingine nzito ambayo Bw. Pinda anapaswa kuutolea ufafanuzi.

  Mbunge huyo alidai kuwa hadi sasa Serikali haijatoa majibu ya kuridhisha kwa Watanzania kuhusu hatua hiyo na wengi wao wanaamini kuwa nyumba zao ziliporwa kwa kutumia ujanja.


  " Nakwambia Watanzania wa leo ni tofauti na wa jana, mimi nimekwenda jimboni kwangu nikawekwa kitimoto, wakaniuliza Mheshimiwa (anataja jina lake) hivi kweli walionunua nyumba za Seriali walikuwa hawajajenga au hawana uwezo wa kujenga au wanataka kupora tu ? Sisi tunakuagiza hizo nyumba zirudi, mkishindwa kurudisha usirudi hapa kutuomba kura?" Alisema.

  Mbunge mwingine kutoka Kanda ya Kaskazini ambaye amekuwa miongoni mwa vinara wa kupinga ufisadi alisema, Waziri Mkuu lazima aweke wazi suala la mkataba wa TICTS inayodaiwa kuwa moja ya sababu za kudorora kwa ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam.

  Pia alisema Bw. Pinda anapaswa kuweka wazi suala la kusuasua kwa Kampuni ya TRL chini ya wawekezaji RITES kutoka nchini India na ikibidi, mkataba huo uvunjwe kwa maslahi ya Watanzania.

  Akizungumzia hotuba ya leo ya Bw. Pinda, Mbunge wa Viti Maalum Bi. Stela Manyanya (CCM) alisema anaamini itakuwa nzuri lakini akaonya kwamba mkakati wa 'Kilimo Kwanza' lazima uweke bayana .

  "Kikubwa zaidi ninachotegemea katika hotuba ya Waziri Mkuu ni kutueleza ni jinsi gani 'Kilimo Kwanza' kitatekelezwa, naamini yeye ataainisha kwa majina vijiji, kata na wilaya zitakazopokea matrekta na jinsi mradi huo ukavyotekelezwa.

  "Hatutarajii kubaki na mpango bila dira kamili ya utekelezaji kisha ikifika mwakani tuje tuambiwe mara fedha zilichelewa, mara kulikuwa na hili hapana, naamini Waziri Mkuu kama Kiongozi wa shughuli za Serikali atatueleza na kutaja moja kwa moja vijiji vitakavyonufaika ili usimamizi uwe mzuri na ufuatiliaji uwe rahisi,"alisema Bi. Manyanya.

  Alipoulizwa matarajo yake kuhusu masuala mtambuka kama vile ufisadi alisema "Unajua ufisadi unatakiwa utazamwe kwa eneo pana sana, ukizingatia hayo ninayosema hapawezi kuwepo ufisadi, yaani ukaweka wazi miradi, nani atanufaika, na trekta zitatolewa ngapi, ni rahisi kufuatia na mkono wa fisadi hauwezi kuingia kwa kuwa kila kitu kipo wazi na wananchi watajua,"alisema.

  Kwa upande wake Mbunge wa Maswa, Bw. John Shibuda, (CCM) alisema anaamini Waziri Mkuu atatoa dira kamili kuhusu utekelezaji wa 'Kilimo Kwanza' kwa kuwa yeye ndiye 'mmliki'wa Wizara zote ndio maana anaitwa Waziri Mkuu.

  "Najua atatoa dira kamili inayoondoa ukungu na mgando wa mawazo usioleta maendeleo katika wizara zote lakini hasa kilimo, yeye ameonea msingi wake wa utawala wake ajenge juu ya 'Kilimo Kwanza' safi kabisa, sasa naamini atatueleza dira hiyo itatekelezwa vipi kwa vitendo na kuondoa misamiati mingi ya muda mrefu,"alisema Bw. Shibuda.
   
 2. W

  WildCard JF-Expert Member

  #2
  Jun 22, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Watabwabwaja na kupayuka kama walivyofanya kwenye hotuba ya bajeti halafu makadirio ya ofisi ya WM yatapita bila kupingwa. Magazeti yanaandika hivi ili yauzike tu. Tunalijua kweli Bunge letu TUKUFU.
   
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  Jun 22, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,323
  Likes Received: 1,788
  Trophy Points: 280
  Napata shaka na utukufu wa bunge kama yaliyopo ni kuongea ili ionekane wako makini kweli halafu mwisho wa siku business as usual. Utukufu ni cheo kikubwa zaidi ya yale yanayofanyika
   
 4. W

  WildCard JF-Expert Member

  #4
  Jun 22, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Nimeliita hivo kuepusha JF yetu isije ikaumizwa na "POWERS AND PRIVILEGES" za Bunge letu TUKUFU.
   
 5. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #5
  Jun 22, 2009
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  wakuu kuna lipi tunalolitaka toka Richmond? Ni history tena jamani. Pengine Dr. Mwakyembe amalizie story aliyoiacha. Nawasilisha
   
 6. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #6
  Jun 22, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,604
  Trophy Points: 280
  Rich monduli inazimwa kimtindo....yale mapendekezo yote 21 jiii..............siasa kwenye utendaji...ni tz tuu hakuna nchi nyingine
   
 7. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #7
  Jun 22, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,581
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  WildCard, nakubaliana na wewe kabisa, tusitegemee kipya kutoka kwa wabunge wetu.
   
 8. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #8
  Jun 22, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Toka lini wabunge wanaogopa kutajwa majina yao? Hivyo vitu kwa nini wasivisema Bungeni, hadharani?

  Gazeti jongo, wabunge waongo, hakuna wa kuwa hold hawa watu accountable... darn!
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Jun 22, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Kama ilivyokuwa hakuna wa kuku hold wewe accountable na uzushi wako wa Dkt. Masau....mzushi uliyekubuhu wewe...
   
Loading...