Richmond case study: Je, Waziri Mkuu Majaliwa atavuka kikwazo cha Lowassa kwa ma-V 8 haya?

Kabende Msakila

JF-Expert Member
Oct 7, 2020
579
1,000
PM hawezi kukwaa kisiki - kama ni hivyo basi OR itawajibika sababu KM Utumishi, Waziri Mkuchika hawataweza kukwepa - baada ya uteuzi yapaswa wafanye Mafunzo ya ndani kwa wateuliwa ili kuwekana sawa - hayo hayakufanyika - KM Tamisemi na Waziri wake Jafo nao hawakuwajibika

Hili limepita
Tunaweza kuyauza nje wapo watu wanaweza kununua au kuuuzia asasi za kiraia ishu ya matunguli sio ishu sana
 
MoseKing

JF-Expert Member
Jul 5, 2017
1,677
2,000
Nawashangaa wanaomuona PM Majaliwa Kassim kuwa ni mchapakazi. Majaliwa ni zao la viongozi madikteta wasiopenda kukosolewa au kushauriwa. Madikteta hawa hachaguwa watu wepesi na wasio na uwezo wa kuchambua mambo ili kutekeleza maamuzi yao kwa watawaliwa.

Majaliwa ni kama DODOKI, mwenye nalo akililoweka linanyonya maji, akilikamua linatowa maji. Hana mawazo wala maamuzi yake. Mifano 4 hii hapa;
1. Suala la FARU JOHN alidanganywa na yule Naibu Waziri na Mbunge wa Loliondo naye akalipuka
2. Alimuwashia moto Asia Abdallah yule DC wa Kilolo tukajuwa atatumbuliwa, hakuna kilichotokea hadi leo
3. Alileta wananunuzi wa korosho na JPM akamtupilia nao mbali
4. Daraja la barabara ya Dodoma- Moro lilipobomilewa aliamuru yule Mhandisi atolewe Morogoro. Hakutolewa
Mkuu nchi hii sasa hivi ukiwa Unazurula unapiga kelele mnooooo na kufokafoka kwenye media ndio unaonekana unachapa kazi balaa.

Ndio maana kuna watu wanamwona Jaffo aka mzee wa Nyungu anafaa kuwa Rais 🤣🤣🤣
 
Oct 27, 2020
65
125
DED anahujumu uchumi utaombaje kitu ambacho unajua ni haramu kwako ? VXR unajua sio hadhi yako kuwa nayo ww ukaomba hili ni kosa, alie idhinisha unaweza kuta alipewa Document ambazo ziko general na vitu vingi akapitisha kumbe kuna mzoga ndani yake
Happy ndipo pa kumkatilia ili kuonyesha unafanya kazi kwa weredi
 
mliberali

JF-Expert Member
Jul 13, 2012
9,133
2,000
Balozi wa USA Mark Green kipindi cha Richmond aimbia dunia kuwa kilichomponza Lowassa ni kuonekana ni tishio kwa wanaotazamiwa kumrithi Kikwete (alipaniwa).

Hapa kuna mtu anayeonekana kuwa frontline kumrithi Magufuli kwa uwezo, utendaji, dini, ukanda na umri, Kassim Majaliwa anazunguka zongo linalomuandama la magari ya kufru yaliyopitishwa chini ya ofisi zake, yalipitishwaje na mtu anayeonekana yupo makini sana walioko chini yake wanamnyooshea kidole.

Akihojiwa na tume ya Dkt. Mwakyembe na baadae bungeni aliyekuwa naibu waziri wa nishati na madini wa wakati huo Ibrahim Msabaha anasema "Naona mimi nitakuwa mbuzi wa kafara kwa hili " maDED wote wanasema ihojiwe ofisi ya waziri mkuu wao wasiwe mbuzi wa kafara.

Kama umemsiliza waziri mkuu kule Mwanza anaona kuwa wenye makosa ni walioitisha ombi la ununuzi wa magari hivyo wawajibike baada ya uchunguzi, walioagiza wanasema shida sio wao kuomba maana ombi lina kukubaliwa na kukataliwa hivyo aliyelipokea na kuidhisha ndie mchawi hapa na huyu si mwingine ni ofisi ya waziri mkuu.

"Tulifuata utaratibu wa ununuzi wa umma kuanzia kwenye kamati ya halmashauri, baraza la madiwani, wizara ya ujenzi na baadae ofisi ya waziri mkuu" DED wa Geita anaongea kwa kujiamini kuwa kwa nini walipewa na aliyetoa anasema kwanini waliomba, kuna utata hapa.

Watanzania hawataki kujua mambo ya nani aliomba na nani alitoa wanataka kufahamu kwanini pesa zao million 400 zote zinunue gari la mtu mmoja tu huku wakiwa na matatizo chungu mzima.

Rais anaonekana yuko wa wananchi wanaolia pesa zao kufujwa na kutaka waliohusika wawajibishwe, waliohusika wanarushiana mpira.

Kwa kuwa hofu kuwa Majaliwa anaandaliwa hakuna anayeweza kumhoji na badala yake yeye ndio anahoji (hapa kuna utata).

Maadui wa Majaliwa kisiasa wanaojipanga kuelekea 2025 wanakesha wanachochea kuni ili kitumbua kiiingie mchaga.

My take; Ule msemo wa kuwa waziri mkuu wa Tanzania hawezi kuwa Rais unaweza ukajitokeza hapa tena!

USSR
Nyie maccm mnaandika upuuzi
Magufuli kamunua midege Nani kamtuma,

Katuibia tri 2.4 kamunua wapinzani mlikuwa kimya

Kawatapeli EU hela za korona mko kimya

Eti majaliwa kupitisha ununuzi wa v8 ndo mnaita ufisadi

Majinga nyie
 
RAISI AJAE

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
2,164
2,000
Comrade huelewi nini hapo??Pale jiwe aliposema pm hana gurantee ndipo safari ya kumtemesha upm ilianza!!!HAPA kitengo kimesuka mpango wa kumuondoa pm kwa skendo bila yeye mwenyewe kujua mtego!!!namna pekee pm angeugomea mpango huu wa ufujaji pesa angekuwa salama!we subiri bunge liketi na kina Gwajima wapewe maiki waanzishe mpira uone tiktaka!!!!MKAPA ANAONDOKA NA PM WAKE MPENDWA!!!
 
mud-oil-chafu

JF-Expert Member
Dec 27, 2020
309
500
Yote Tisa kumi game tough ,,,mafuta ya kula yamepanda Toka 3500 had 5000 ndan ya miez minne mjn iringa,na mkate yamepanda Toka 2000 had 2500 kwa wiki mbili ongezeko la 25%,,,,still you are discussing about Nani kamla mwanangu na fisi mnawaona,,,,focus🤕🤕🤕
 
katoros

JF-Expert Member
Feb 12, 2020
428
500
Balozi wa USA Mark Green kipindi cha Richmond aimbia dunia kuwa kilichomponza Lowassa ni kuonekana ni tishio kwa wanaotazamiwa kumrithi Kikwete (alipaniwa).

Hapa kuna mtu anayeonekana kuwa frontline kumrithi Magufuli kwa uwezo, utendaji, dini, ukanda na umri, Kassim Majaliwa anazunguka zongo linalomuandama la magari ya kufru yaliyopitishwa chini ya ofisi zake, yalipitishwaje na mtu anayeonekana yupo makini sana walioko chini yake wanamnyooshea kidole.

Akihojiwa na tume ya Dkt. Mwakyembe na baadae bungeni aliyekuwa naibu waziri wa nishati na madini wa wakati huo Ibrahim Msabaha anasema "Naona mimi nitakuwa mbuzi wa kafara kwa hili " maDED wote wanasema ihojiwe ofisi ya waziri mkuu wao wasiwe mbuzi wa kafara.

Kama umemsiliza waziri mkuu kule Mwanza anaona kuwa wenye makosa ni walioitisha ombi la ununuzi wa magari hivyo wawajibike baada ya uchunguzi, walioagiza wanasema shida sio wao kuomba maana ombi lina kukubaliwa na kukataliwa hivyo aliyelipokea na kuidhisha ndie mchawi hapa na huyu si mwingine ni ofisi ya waziri mkuu.

"Tulifuata utaratibu wa ununuzi wa umma kuanzia kwenye kamati ya halmashauri, baraza la madiwani, wizara ya ujenzi na baadae ofisi ya waziri mkuu" DED wa Geita anaongea kwa kujiamini kuwa kwa nini walipewa na aliyetoa anasema kwanini waliomba, kuna utata hapa.

Watanzania hawataki kujua mambo ya nani aliomba na nani alitoa wanataka kufahamu kwanini pesa zao million 400 zote zinunue gari la mtu mmoja tu huku wakiwa na matatizo chungu mzima.

Rais anaonekana yuko wa wananchi wanaolia pesa zao kufujwa na kutaka waliohusika wawajibishwe, waliohusika wanarushiana mpira.

Kwa kuwa hofu kuwa Majaliwa anaandaliwa hakuna anayeweza kumhoji na badala yake yeye ndio anahoji (hapa kuna utata).

Maadui wa Majaliwa kisiasa wanaojipanga kuelekea 2025 wanakesha wanachochea kuni ili kitumbua kiiingie mchaga.

My take; Ule msemo wa kuwa waziri mkuu wa Tanzania hawezi kuwa Rais unaweza ukajitokeza hapa tena!

USSR
Wataje maadui wa PM angalau wawili
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom