RICHA PWAAAAAAAAA-----Miss World atoka China

Semanao

JF-Expert Member
Jul 25, 2007
208
16
Miss China Zhang Zilin pichani juu ameibuka mshindi wa Shindano la Miss
World lilomalizika hivi punde Sanya China, ambapo Mwakilishi kutoka Tanzania
Richa Adhia alitolewa kwenye mchakato huo kwenye kwenye hatua za kwanza kabisa
bila kugusa mzunguko wa pili..

Habari zaidi http://haki-hakingowi.blogspot.com/
 
Miss World leo, Lundenga lawamani

na Janelisa William

HUKU fainali za kumsaka Mrembo wa Dunia ‘Miss World' zikifanyika leo mjini Sanya, China, mwakilishi wa Tanzania katika shindano hilo, Richa Adhia ameitupia lawama Kamati ya Miss Tanzania kwa kushindwa kumtumia DVD, hivyo kumkosesha taji la Beauty with Purpose.
Alisema kukosekana kwa DVD hiyo iliyokuwa ikionyesha kazi za kijamii alizofanya akiwa Miss Tanzania, kukamnyima alama muhimu ambazo zingemsaidia katika kuwania taji hilo, hali ambayo imemvunja moyo.

Alipoulizwa kwa simu ni vipi hakuondoka na DVD, Radhia alisema hadi anaondoka, Kamati ya Miss Tanzania ilikuwa bado haijakamilisha kutengeneza DVD hizo, hivyo akaelezwa atangulie, watazituma.

Radhia alisema, siku chache kabla ya shindano hilo la Beauty with Purpose, alipowasiliana na Kamati ya Miss Tanzania, akaelezwa kuwa kwa bahati mbaya, wameituma DVD hiyo Uingereza.

"Hii imenivunja moyo, nilipowasiliana na Mratibu wa Kamati ya Urembo Tanzania, Hashimu Lundenga, akanieleza amekosea kutuma DVD, kwani badala ya kutuma Sanya China, akatuma Uingereza," alisema.

Mrembo huyo pia amelalamika kitendo cha kamati hiyo kumtelekeza kwani mbali ya mama yake aliyemsindikiza katika shindano hilo, hakuna mwingine aliyekuwa amemsapoti.

Wakati hali ikiwa hivyo, mrembo huyo wa Tanzania pamoja na wenzake zaidi ya 100, leo atakuwa akiwania taji la dunia, Miss World 2007 katika shindano ambalo mwaka huu, kwa Tanzania limekosa msisimko.

Shindano hilo litakalofanyika katika Ukumbi wa Beauty of Crown Theatre, linatarajiwa kuwa la ushindani mkubwa kwani kila mshiriki atakuwa akitaka kulitwaa taji hilo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Miss World, Julia Morley kwa upande wake amesema mrembo atakayetwaa taji hilo leo, atatembelea nchi zote zilizo na washiriki ikiwemo Tanzania katika kuhamasisha jamii kujikinga na ukimwi.

Warembo wengine waliowahi kuiwakilisha Tanzania katika shindano hilo na miaka yao katika mabano, ni Aina Maeda (1994), Emily Adolph (1995), Shose Senare (1996), Saida Kessy (1997), Basila Mwanukuzi (1998) na Hoyce Temu (1999).

Wengine ni Jacqueline Ntuyabaliwe (2000), Happiness Magese (2001), Angela Damas (2002), Sylvia Bahame (2003), Faraja Kotta (2004), Nancy Sumari aliyepata mafanikio kwa kuwa bora Afrika ‘Miss World Africa' mwaka 2005 huku wa mwisho akiwa ni Wema Sepetu.
 
hebu wa tz tuanze kuwa serious...china na uingereza wapi na wapi??au kuna mji waitwa sanya huko uk.??
 
n besides..hiyo kamati ya miss tz kwanini haijwahi kubadilishwa toka miaka ileee??hata ka ni biashara huria lakini they are using jina la nchi internationally....watu hao hao tuuuu
 
n besides..hiyo kamati ya miss tz kwanini haijwahi kubadilishwa toka miaka ileee??hata ka ni biashara huria lakini they are using jina la nchi internationally....watu hao hao tuuuu

Nafikiri Lundenga alinunua haki zote za kuendesha hayo mashindano ya Umiss hadi Afe.
 
hata rangi imemuangusha pia wanajua tz weusi anakuja anatokea mdosi walishangaa kidogo tehe!
 
Jamani mimi nimeona mashindano ya Miss World kutoka ughaibuni, Miss Sweden alikuwa hana DVD alikuwa na picha 1 tu lakini aliingia top 5 ya Beauty with a Purpose na aliingia top 5 ya mashindano na kunyakua taji la Queen of Europe! Richa aache visingizio! Kama angepeleka hata picha angeingia kama wangeona alichokifanya kinafaa kwani Miss Sweden alikuwa na newspaper clipping 1 tu!
Mi simtetei Lundenga lakini mrembo Richa anajihami tu! Akubali kushindwa asitafute visingizio.
 
Kama kawaida kwa Tanzania Mchawi hakosi. The whoel sytem is C. R. A. P. Lundenga na mamluki wake wnachaofanya ni kukusanya pesa tu nothing else bora mwaka upite. Na kwa mshindani mdosi naye aache visingizio DVD ziantumia muda gani kutengeneza? Was she serious? Amekaaa siku ngapi SANYA JUUU!!! teh teh tehe(China sio kwa Sadala). Ina maana jana tu ndiyo anakumbuka kupiga simu snunui hiyo mbovu. Arudi Tanzania, Hatuna Hiana si wa kwanza na labda hatokuwa wa mwisho!!
 
Discrimination against people of different origins will not help us.
They are Tanzanians like us. She was born and raised in Tanzania. Her parents at the same time. Today results was what we want since sh wont miss Tanzania title, why we Tanzanian we behave like this. If the case is her origin i think all of use our origin will be questionable.
I am feeling ashamed for being called Tanzanian.
 
Jamani hapa hakuna discrimination! Let us stop using it as an excuse! Lundenga aliwaambia watanzania kwamba walimchagua Richa kwa sababu 'amefanana nao' na ana uwezo wa kuleta crown! So her selection already was based on race! Mimi lazima niwatetee watanzania wote. Suala la race alianza kulitetea Lundenga the wrong way! He should have just said she deserved it.
So, baada ya kutoa utetezi huu, usemi ukawa ngojeni aende Richa atafanya mambo. Lundenga aliwaponda mpaka mamiss Tanzania waliopita akisema hakuna aliyefanya kazi ya kijamii kama Richa. Sasa anaposhindwa na watz wakimponda Lundenga na mrembo wake kama kawaida tena wanataka kutumia disguise ya discrimination! NO!
Face the music, haya ni mashindano tu lakini you have to accept some things including defeat.
Mi naamini it's the way Lundenga and company handled the whole issue, vinginevyo watanzania hawana matatizo na Richa. Mbona alituwakilisha Miss Earth mwaka 2006 na hakuna aliyemsema vibaya?
 
The girl is not beatiful period.

At the end of the day it is still a beauty contest and along with all the other stuff (personality, confidence etc) you have to be beautiful. Compare Richa to most of the other girls and she doesn't even come close in terms of beauty. It's got nothing to do with her race if she was a beautiful Tanzanian of Indian origin, of european origin, of chinese origin i would be happy.

However the bottom line is we picked a girl who is not beautiful to represent us in what is essentially a beauty contest. She had no chance from the begining
 
Thanks Alpha! Alafu kinachonikera ni hao wapambe wanaosema eti mzuri kwa sababu kafanana nao au ana ngozi nyeupe na hawaoni ya kuwa they are beng racist like this! Ni inferiority complex zetu tu! Mbona Flaviana Matata kaenda black and bald and beautiful to Miss Universe na kafika mbali kwani alishika namba 6 in the universe? Tuache kasumba. Let us choose the best girl despite of skin color na tuache kuabudu ngozi nyeupe na nywele zilizonyooka!
But then what does Lundenga know?
 
yaaani jus bcz ni mhindi ndo wanataka tukubali kuwa ni mzuri....jus bcz ma miss world kadhaa waliopita washawahi toka india....ok now ametoka china so miss tz wa mwakani tumtafute mchina mmojawapo kati ya hao waliomigrate kinyemela kwa wingi bongo yetuu awe miss tz!!!
mie kilio changu ni kwanini hao kina Lundenga na Patel n company ni hao hao tuu??hawawezi badilishwaa??au ndo u life time bnez ka Fidel Castro Cuba kuleee??
 
Niliangalia hilo shindano juzi through TV, wallah naapa sikubahatika kuiona hiyo sura ya mhindi,kulikua hakuna uwakilishi wa Tanzania pale,sometimes nilikuwa nikimuona miss Ghana najua ndo miss wetu.

Hawa BASATA sijui wanampango gani, wanaangalia tu jinsi jina la Tanzania linavyodhalilika lakin wako kimya tu,kwanini kila mwaka ni Lundenga tu? inamaana hakuna watu wengi wanaoweza kufanya hii kazi ni Lundenga tu ndio anaeweza kutafuta mamiss!
 
Ram siyo peke yako nimesoma maoni mengi, wengi wakitaka Lundenga na Prashant Patel wasiendelee na Miss World, lakini haiwwezekani.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba franchise ya Miss World ni ya Lino Agency. Hii ni biashara ni kama ukinunua franchise ya MacDonald's. Ni ya kwako as long unafuata sheria. Na hawakunyang'anyi leseni akina Julia Morley labda ubangaize. Lakini naona Miss World Organization na bibi Julia Morley wameridhika na akina Lundenga kwa hiyo tunalo!
 
Discrimination against people of different origins will not help us.
They are Tanzanians like us. She was born and raised in Tanzania. Her parents at the same time. Today results was what we want since sh wont miss Tanzania title, why we Tanzanian we behave like this. If the case is her origin i think all of use our origin will be questionable.
I am feeling ashamed for being called Tanzanian.

Hell No............!

Sijawahi kuona Mtanzania wa ukweli ukwelii I mean mababu wote hapa hapa aukane utanzania wake even hapa JF wewe ndio wa kwanza.

Tumetukanwa,tumedhalauliwa na hata kuonekana tuna akiri pungufu lkn hamna aliye ukana UTZ wake hapa.

I am begining to think nyie ndio ndugu zake Bint ambao mna passport mbili mbili,mkiona hapa kina waka mnakimbilia kwengine labda Canada kwa mfano kama wale wengine............!

Alafu mbona hi kitu iko wazi kabisa,kwa mfano just now i am from RITA kule kwenye kuandikisha birth & death kwa wale mlioondoka zamani VIZAZI NZ VIFO.
Hawa jamaa zetu Mabaga choli hawataki kujichanganya na sisi wazawa na wanataka huduma zao(wahudumiwe haraka kuliko ss tuliodamka) ziwe faster faster,alafu wakiwa huko majukwaani kwa hao puppets wao wana nadi wao Watanzania tena "DUGU MOJA" na sisi.Mie hesabu hii naikataa tena nakata mpaka kufa.

Jana tu kwa wale walio angalia ITV habari saa mbili usiku ni mashuhuda ya yale ninayo yasema,Kulikua na shughuli kwenye 'skuli' ya kidosi theme yao ni kuwalithisha 'utamaduni' asili yao watoto wao wano soma kwenye shule hiyo,tukaonyesha ngoma zao hasa nachi,sikuona VANGA,Sindimba au hata mdundiko wa watu wote alfu wan sema wao wengine ni wagogo,wazaramo hata wachaga!

Mie nakata hawa watanzania ila ni WAHINDI kwao INDIA huko ASIA ambako tamaduni za huko wana walithisha watoto wao na kama TAMADUNI NDIO UTAIFA kuna nini tena hapo............!!!!!!????
 
yaaani jus bcz ni mhindi ndo wanataka tukubali kuwa ni mzuri....jus bcz ma miss world kadhaa waliopita washawahi toka india....ok now ametoka china so miss tz wa mwakani tumtafute mchina mmojawapo kati ya hao waliomigrate kinyemela kwa wingi bongo yetuu awe miss tz!!!
mie kilio changu ni kwanini hao kina Lundenga na Patel n company ni hao hao tuu??hawawezi badilishwaa??au ndo u life time bnez ka Fidel Castro Cuba kuleee??

Haswaa...!!!!
Si wachina wameshakua wengi hapa bongo.
Wengine wanauza karanga mtaani.
 
Sanda Matuta, I think your anger is misplaced! Mimi sina tatizo na Richa na ninaamini hata watanzania wengi hawana habari naye. Tatizo ni mazingira aliyoshinda hilo taji. Kama kawaida miss Tanzania kulikuwa na utata. Sasa kwa kuwa Richa anaasili ya uhindi hii ikawa ishu. Hapo nyuma ilikuwa ni ishu ya baba mwenye uwezo (Wema SEPETU, Basila MWANAKUZI, n.k.) au miss katoa rushwa ya ngono! Mara chache sana, mshindi alikubalika na jamii, kama ilivyokuwa kwa Nancy na Hoyce.
Sasa naona kiini cha matatizo yote siyo Richa bali Lundenga na kampani. Kama persnally you have your axe to grind na wahindi that is separate from this issue and we should keep it this way, ili wasije wakatafuta sababu kusema eti watanzania ni wabaguzi!
 
Back
Top Bottom