riba ya kukopa iliyopangwa na Benki Kuu ni asilimia nane

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,222
1,670
"Meghji alia riba benki zinaumiza wakopaji"

'Mfano hata sisi wabunge hapa tunashindwa kupata mikopo hiyo wakati tunajulikana tunaishi wapi, tunafanya nini na tunalipwa nini lakini bado ni matatizo,je hao wananchi inakuwaje?'

Dodoma. Waziri wa zamani wa Fedha, ZakhiaMeghji, ameitaka Serikalikudhibiti benki ili ziache kuwatoza riba kubwa ya mikopo wananchi wa Tanzania.
Meghji, ambaye ni Mbunge wa Kuteuliwa, alisema riba ya kukopa iliyopangwa na Benki Kuu ni asilimia nane lakini benki hizo zimekuwa zikitoza riba ya asilimia 19.
Hata hivyo, gazeti hili linafahamu kiwango chariba kinachotozwa na mikopo kwa sasa hufikiahadi asilimia 30 katika baadhi ya benki.
Akichangia hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Wizara ya Fedha kwa mwaka 2013/14 bungeni jana, Meghji alisema kwa mwenendo huo benki haziwezi kuwakomboa Watanzania kiuchumi. “Hata Gavana wa Benki Kuu anajua kuwa tunakopa fedha kwa benki kubwa kwa riba ya asilimia nane, lakini benki hizo zinakopesha kwa riba ya asilimia 19, hali hii inawapa shida wananchi na hasa wale wenye kipato cha chini,” alisema Meghji. Meghji, ambaye aliondolewa kwenye nafasi ya Waziri wa Fedha mwaka 2008, alilalamikia pia urasimu katika utoaji mikopo akitoa mfano baadhi ya benki kutaka makazi ya wakopaji huku wakisingizia wanataka vitambulisho vya taifa.
“Mfano hata sisi wabunge hapa tunashindwa kupata mikopo hiyo wakati tunajulikana tunaishi wapi, tunafanya nini na tunalipwa nini lakini bado ni matatizo, je hao wananchi inakuwaje?” alihoji. Naye Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi) alilia na benki akieleza kuwa haziwasadii Watanzania na akazituhumu kuwa zinajihusisha na kutorosha fedha nchini.
Kafulila alisema licha ya Tanzania kuwa na benki zaidi ya 50 lakini huduma za kibenki haziwafikii kikamilifu Watanzania walio wengi. “Hizi benki hazipo kwa ajili ya kumsaidia mwananchi….zipo kibiashara zaidi na ndiyomaana wanatoza riba kubwa hali inayomnyimamwananchi fursa ya kukua na badala yake wanaokopa wanazifanyia kazi benki,” alisema Kafulila. Pia aliitaka Serikali ipeleke bungeni majina ya watu wote waliokopapesa katika Benki ya NBC ili wajulikane na walazimishwe kuzilipa.
“Zaidi ya shilingi 60 bilioni zimekopwa na wafanyabiashara wakubwa….wapo tu na hakuna mwenye nia ya kulipa, tunataka majina ya watu wote waliokopakatika benki hiyo yaletwe hapa bungeni,” alisema.
Ununuzi wa magari
Mapema akiwasilisha bungeni makadirio ya matumizi ya wizara yake,Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa alisema,Serikali itafuta ununuzi holela wa magari kwa taasisi zake mbalimbali, pia kupunguza muda kwa wastaafu kupata pensheni zao kutoka miezi sita hadi miezi mitatu.
Alisema taasisi zote za Serikali zitapaswa kununua magari kupitia Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini, (GPSA), kwa kuwa eneo la ununuzi wa magari linatumia fedha nyingi.
“Ununuzi wa magari ni eneo linalotumia fedha nyingi za umma na kutokana na hilo, Serikali imeona kuna umuhimu wa kuweka utaratibu bora utakaowezesha kupata thamani ya fedha katika ununuzi pamoja na matumizi ya magari yake.

CHANZO: MWANANCHI
 
Huyo Meghji si alikuwa waziri wa fedha alikuwa halijui hilo tatizo wakati limeimbwa miaka yote lakini sielewi kwanini tunaruhusu benki zote zijazane dar wakati umefika tulazimishe ili benki zioperate atleast ziwe na matawi mikoa kuanzia 5
 
Nadhani 8% ni lowest possible lending interest ambayo BOT wameweka. The market rate can be higher than that. Kumbuka riba inategemea na mahitaji ya mikopo, kumbuka riba ni bei ya mkopo, so, muuzaji wa mkopo ana uhuru wa kuuza kwa bei anayotaka ila hawezi kwenda chini ya 8%. Ni simple economic facts
 
na pia huwa wanatoa riba wakiondoa inflation rate sasa wewe ndio ujiongeze sasa kulingana na inflation iliyopo..
 
Riba ni tatizo sana sana na hii inasababishwa na serikali kukopa fedha nyingi.

Serikali ipunguze kuchukua pesa ila riba ishuke.
 
Riba ni tatizo sana sana na hii inasababishwa na serikali kukopa fedha nyingi.

Serikali ipunguze kuchukua pesa ila riba ishuke.

Mkuu pamoja na hilo lakini ukweli unabaki pale pale kwamba there is little competition between lending/financial institutions, wanajipangia tu wanavyotaka, ukitaka ukakope, hutaki unaache wenzako wanataenda kukopa!
 
Ye alifanya nn wakati alivyokuwa waziri? Afu angefafanua hiyo 8% ni lowest or highest interest inayotakiwa kutozwa. Back to the topic katika kuset interest kuna vitu ving sana vinaangaliwa eg inflation,level of risk etc. Katika hizi taasis risk ya kupoteza hela ni kubwa sana ndo maana mabenk yanaweka interest kubwa na hii ni kutoka na system mbovu ya serikal yetu yakutokuweka utambulisho wa mwananchi. Mteja anaweza kopa benk x kwa kutumia voter's id baada ya mwez anahama anaenda benk y anatumia driving licence tena baada ya miaka miwili anaenda kukopa sehemu nyingine kwa kutumia chet cha kuzaliwa na cha makazi. Ona huyu mtu mwisho wa siku ukimtafuta humpati maana kila alikoenda amejitambulisha tofauti. Serikali ifanye haraka kuandaa id zile za utaifa maana huwezi kuwa na zaid ya moja na hiyo ndo itumike kwenye hiz lending institutions pamoja na kuanzisha credit reference burea ili kusaidia kumpata defaulter wakati akikimbilia benk nyingine. Hapo interest zitashuka maana benk zitakuwa na uhakika wa kupata fedha zao hata kama faida itakuwa ndogo. Mfano kenya
 
Nadhani 8% ni lowest possible lending interest ambayo BOT wameweka. The market rate can be higher than that. Kumbuka riba inategemea na mahitaji ya mikopo, kumbuka riba ni bei ya mkopo, so, muuzaji wa mkopo ana uhuru wa kuuza kwa bei anayotaka ila hawezi kwenda chini ya 8%. Ni simple economic facts

nice economist
 
Back
Top Bottom