Riba kwenye Mabenki ni Jipu kubwa sana

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
36,982
45,886
Kwa wale ambao wanahitaji mikopo au wanaofanya shughuli zao kwa kutegemea facilities za Mabenki kwa kweli hili jipu linahitajika kuangaliwa upya.

Kwa hapa nchini ukiangalia Prime Lending Rates kwa kweli zipo juu sana, zinafikia mpaka 30%. Ni watu wachache sana watakaoweza kufanya biashara na kupata faida.

Mikopo mingi hairejesheki, sijui ni kwa namna gani wataalam wa uchumi watasaidia katika hili,, ila maendeleo yatakua magumu kufikika kwa mwananchi wa kawaida, kama mwananchi huyo atakua hana uwezo wa kukopa na kufanya shughuli za maendeleo.

Wengi wa wakopaji unakuta dhamana zao zinaishia kutumika ili kurealize madeni yao kwa mabenki.

Magufuli ana mtihani mwingine kuhakikisha kweli hili linafanyiwa kazi maana ni jipu.
 
Ni hatari mno. Watu wanalipa zaidi ya 50% interest baada ya deni kuisha. What a business? Kwa nini usijambe kuendelea, lazima. Hapo hapo ukichukua tu mkopo vyura wa benki hawa hapa waanza kuzikwapua kama speed ya mwanga. Zikiisha haoooo!! wanaanza kukuambia baada ya miezi 6 unaruhusiwa kukopa tena, thubutu!! Utakufa maskini hivi hivi!!
 
matajiri kina manji, dewji wao wanakopa nssf kwa riba za bure kabisa..

maskini unakopeshwa ka milion 10 bank kwa riba mara mbili yake.... why na mfanyakazi wa kawaida asikopeshwe na nssf au ppf??

mi nilichojifunza ni kukopa saccoss tu za maofisini bank zote majanga tu riba zao
 
Mabenki yamezidisha sana, ingawa wanaweza kudai kwamba ni sababu ya Inflation na risk premium, lakin mm naona kama bado yanatuumiza sababu kama ni cost of borrowing ni kama hawana kabisa, wafanyakaz na wenye kipato cha kawaida wanajiwekea savings zao bila hata return yoyote ya kueleweka.
 
Halafu sisilkii waziri wala mbunge yeyote kulikemea Hilo,au kwa vile ni ya kwaooo...
 
Kwa Bank kama ACCESS BANK ni shida na jipu kubwa Africa Mashariki na duniani kwa ujumla, wana riba kubwa isiyoelezeka na wanakupa mkopo kiukaini sana lakini watu wana filisiwa mali zao haraka pasipo hata kufuata sheria, unajikuta unalipa mpaka mtaji wako wa biashara jwa jinsi riba ya mkopo ilivyokuwa kubwa na ya kutisha
Kama hujakopa nakushauri uende japo NMB na sio private banks hususan Access Bank ni wanyama sirudii tena kukopa
 
Ni kweli kabisa lakini hatuna ujanja maana kupata mtaji kwa kilimo ni ngumu sana,duh nilikopa ACCESS Bank hadi namaliza mkopo nikiwa naongea peke yangu barabarani bora NMB na CRDB
mwenzangu nami, mie gari na makabati yaliondoka, karibia nirudi kwenye umaskini, mpaka hapo nimeogopa mkopa yapata miaka mitatu sasa, maendeleo nayasikia kwa jirani
 
Siku tatu kabla ya tarehe ya rejesho wanaanza kupiga simu, hawajali muda wanapiga hadi sa nne usiku!! Ukichelewesha rejesho unapigiwa simu kila nusu saa na namba tofauti tofauti, unaweza kufa na presha.


Duc In Altum.
Kuna siku nilimpa faka afisa mikopo wao baada ya kuanza kunipigia nikiwa kwenye sherehe nikamuuliza mbona siku mliyoniwekea mkopo uliingia saa 12jioni je muda huo nilizitoa na kuanza biashara. Mbona nyie siku moja tu mnachonga sana!! Aisee hadi alikata simu
 
Back
Top Bottom