RFA, si nyimbo zote za kuchezwa mchana

Jacobus

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
4,674
1,685
Nitumie fursa hii kushauri Vyombo vyetu vya Habari kuchuja nyimbo. Leo ni mara ya pili RFA kuucheza wimbo ambao maneno yake si ya hadhi ya radio kama hii kuucheza. Kama ni lazima, basi zichezwe usiku kuanzia saa sita.

Wimbo huu unaimbwa na mdada akikumbuka raha anayoipata akiwa kitanda cha sita kwa sita na njemba wake mpaka kufika kileleni.

Kwa kuwa Mamlaka ipo lakini ni kama inasubiri mhemko wa kisiasa basi ombi langu nyimbo aina hiyo kuchezwa usiku na si mchana.
 
Alie imba huo wimbo katumia luga gani? Kama kiswahili hapo nitatizo ila kama ni kimombo haina shida kabisa
 
Inaonekana unachuki tu na RFA, mbona WCB na clouds wanapiga nyimbo za matusi lakini hujadema?
 
Nitumie fursa hii kushauri vyombo vyetu vya habari kuchuja nyimbo. Leo ni mara ya pili RFA kuucheza wimbo ambao maneno yake si ya hadhi ya radio kama hii kuucheza. Kama ni lazima, basi zichezwe usiku kuanzia saa sita.

Wimbo huu unaimbwa na mdada akikumbuka raha anayoipata akiwa kitanda cha sita kwa sita na njemba wake mpaka kufika kileleni.
Kwa kuwa mamlaka ipo lakini ni kama inasubiri mhemko wa kisiasa basi ombi langu nyimbo aina hiyo kuchezwa usiku na si mchana.

Nyimbo gani hiyo mkuu?
 
Ushauri mzuri kabisa kuna baadhi ya nyimbo ni aibu kuzisikiliza mchana ,wamamuziki wa USA/UK mara nyingi huwa wanatoa Radio /Clean/Edited Versions kwa ajili ya Radio Only na Dirty Vsersion zinakuwa kwenye LP/EP/Albums tu,Nashangaa Bongo nyimbo matusi tupu zinapigwa redioni ,nakipongeza chombo kimoja tu cha East Africa Radio huwezi kusikia nyimbo za matusi ,sehemu yenye neno la tusi huwa wanamute/edit.
 
Inaonekana unachuki tu na RFA, mbona WCB na clouds wanapiga nyimbo za matusi lakini hujadema?
Sio chuki mkuu tena pana nyimbo nyingi tu ukizisikiliza ni aibu tupu ndo maana nimetumia RFA kuwakilisha 'media' zote hapa nchini.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom