RFA hii ni aibu kwenu

njaakalihatari

JF-Expert Member
Feb 12, 2019
4,084
8,663
Saa 12.22 jioni dw ujerumani iko hewani kupitia rfa mtangazaji anasoma sms za wasikilizaji. Kuna sms moja kutoka tanzania ikauliza: mbona wizara ya afaya inasema tuepuke mikusanyiko halafu serikali hiyohiyo inakusanya mamia ya watu kuzindua miradi?

Wakati sms inaendelea kusomwa ghafla jamaa wa ilemelea mwanza wakakata matangazo na kuweka ji-song la christian bella.

Aibu sana sana tu mngeacha sms isomwe hadi mwisho tu!
 
Tupeleke lawana zinapotakiwa kwenda napo ni TCRA, kulingana na sheria za sasa redio ndio inahusika/ inawajibika na chochote kitakachosemwa kwenye redio yao..

Na huu mwendo wa kupigana faini / na kosa ni according la wenyewe wakiamua kama ni kosa au hapana..., unadhani nini kitatokea
 
si waache tu basi kujiunga na DW au BBC? au wanalipwa na hayo mashirika?mbona kipindi cha kikwete kulikuwa hakuna censorship ya kiasi hiki?yaani hata hiyo sms ilikuwa na madhara gani sasa?
Mkuu zama zimebadilika
 
Bora wao wanakata, kuna radio zingne zikuiz hawarushi kbs matangazo ya dw
 
Ya RFA mzee baba anaita uzalendo. Ya hiyo SMS mzee baba anaita kukosa uzalendo.

Hivyo RFA wamekuwa wazalendo kweri kweri.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Haya mambo zamani tukiwacheka watu wa mataifa mengine kutawaliwa ki communist. Tulidhani Sisi tupo salama kumbe zamu yetu ilikuwa bado.

Tunaambiwa uzalendo , sijui ndiyo hayo ya kujatiana matangazo ?! . Kama kipindi cha uchaguzi kiliboa vibaya sana !!
 
Iliamuliwa kila chombo cha habari kinachojiunga na matangazo ya nje, viwe na mtu maalum kutoka TCRA. Huwenda ndo anafanya kazi yake aliyoagizwa.
 
Uwe unajiunga na radio za nje wa zile za IPP
DW mchana Capital Radio au Radio Tumaini
BBC jioni Radio One

Rfa mafala
 
si waache tu basi kujiunga na DW au BBC? au wanalipwa na hayo mashirika?mbona kipindi cha kikwete kulikuwa hakuna censorship ya kiasi hiki?yaani hata hiyo sms ilikuwa na madhara gani sasa?
Nyakati za Jiwe hizi a.k.a mtukufu
 
Saa 12.22 jioni dw ujerumani iko hewani kupitia rfa mtangazaji anasoma sms za wasikilizaji. Kuna sms moja kutoka tanzania ikauliza: mbona wizara ya afaya inasema tuepuke mikusanyiko halafu serikali hiyohiyo inakusanya mamia ya watu kuzindua miradi?

Wakati sms inaendelea kusomwa ghafla jamaa wa ilemelea mwanza wakakata matangazo na kuweka ji-song la christian bella.

Aibu sana sana tu mngeacha sms isomwe hadi mwisho tu!
Mbona RFA ilishafeli siku nyingi?

Sent from my vivo 1904 using JamiiForums mobile app
 
RFA wapo Sawa, mleta mada unaweza kusikiliza DW moja kwa moja kupitia masafa yao au kupitia Facebook.
Hatutaki matangazo ya Corona
 
Tupeleke lawana zinapotakiwa kwenda napo ni TCRA, kulingana na sheria za sasa redio ndio inahusika/ inawajibika na chochote kitakachosemwa kwenye redio yao..

Na huu mwendo wa kupigana faini / na kosa ni according la wenyewe wakiamua kama ni kosa au hapana..., unadhani nini kitatokea
Basi wasiwe wanarusha live ila wahariri kwanza ndio warushe baadaye..maana wanajitia aibu mno
 
Back
Top Bottom