Revolution Nchi za Kiarabu; Ni Mpango wa Matajiri na Wall Street | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Revolution Nchi za Kiarabu; Ni Mpango wa Matajiri na Wall Street

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Haki, Feb 24, 2011.

 1. H

  Haki JF-Expert Member

  #1
  Feb 24, 2011
  Joined: Jan 14, 2009
  Messages: 356
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bush alipoulizwa mwaka 2001 kwamba "Je Saddam Hussein anahusika vipi na 9/11?" Alijibu "Tunakwenda Iraq kwa sababu ni mafuta ya Iraq ndiyo yatakayolipa gharama za vita vya Afghanistan."
  Bush aliweza kuwatajirisha matajiri wakubwa duniani kwa njia ya kupandisha bei za mafuta.

  Sasa hivi vigogo vya Wall Street haviingizi pesa kama zamani alipokuwa baba yao Mzee Bush. Njia pekee iliyobakia ni kuDestabilize MidEast ili bei ya mafuta ipande. Sasa hivi bei ya mafuta ishaanza kupanda duniani. Revolution zinazotokea duniani zimepangwa na vigogo vya Marekani kwa kutumia njia ya Facebook, Twitter.

  Nchi pekee ya Afrika iliyopata "Uhuru" kwa kushabikiwa na Marekani na Wazungu ni South Sudan. Yote kwa sababu South Sudan wanamafuta.

  Swali:Kwanini Anderson Cooper (CNN) haji Arusha au Mwanza kutangaza live maandamano?

  Jibu: Hatuna Mafuta na interest za kubwa za Marekani na EU.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Feb 24, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  interesting.............

  kwahiyo mubarak ni kiongozi mzuri sio?
   
 3. Scientist

  Scientist JF-Expert Member

  #3
  Feb 24, 2011
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  DUh bingwa, inamaana wanachokitafuta ni kuwaridhisha watu wa 'magharibi'? Yaani hujaona tatizo kwa mfano LIBYA raisi kuongoza nchi kwa miaka 42???? Mhh nina wasiwasi na IQ yako!
   
 4. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #4
  Feb 24, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Tatizo ni kwamba siku zote masikini humlaumu tajiri kwa umasikini wake. Ni masikini yule tu anaye tambua kwamba si kulaumu bali bidii ndiyo itamkwamua huwa ndiyo hufanikiwa. Siku zote mtu akiwa wa kulaumu wengine basi kamwe hafiki popote. Na ndilo tatizo la wengi wetu. Hatujiangalii wenyewe.

  Sisemi kwamba Wazungu hawana makosa yao. Wazungu ni wanafiki na huangalia maslahi yao zaidi. Lakini hata sisi tunge kuwa katika nafasi yao tunge fanya vivyo hivyo.

  Mapinduzi ya nchi za Kiarabu ni kwa sababu ya wananchi. Wananchi walisha choshwa na hali yao. Kama wananchi wange kuwa wame ridhika na maisha yao basi kamwe hata mzungu angesema nini wasinge fanya mapinduzi. Nikupe mfano. Kama mtu umemsaliti mkeo kwa kwenda nje ya ndoa mtu aka kushtaki kwa mkeo kuvunjika kwa ndoa utamlaumu nani? Wewe au aliye shtaki? Mimi nitamlaumu msaliti kwani bila kufanya hivyo hata huyo alieenda kushtaki asingekua na cha kusema.
   
 5. N

  Nonda JF-Expert Member

  #5
  Feb 24, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Mkuu.
  Sisi kama wananchi kweli tuna sehemu yetu katika kuchangia matatizo yetu...pia haya ya viongozi kufikiri wao tu ndio wenye kujua kila kitu na haki ya kuongoza watakavyo haikubaliki ..lakini kuna na hili la wababe wa dunia kuingilia nchi nyingi na kuziharibu kwa maslahi yao. Unakumbuka Chavez alimpa Obama kitabu chenye kuonesha USA inavyozivuruga nchi za Amerika Kusini?Ona hii filamu.


   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #6
  Feb 24, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mkuu Nonda kama nilivyo sema sija bisha involvement ya West nakubali. Ila viongozi wana changia kiasi kikubwa. Kama ume sikiliza video yote jamaa kasema kwamba hela zina benefit makampuni ya kizungu na familia chache za kitajiri kwenye nchi hizo masikini. Hizo familia chache ni zipi kama sio za viongozi (na baadhi ya wafanya biashara?)? Kumbe tunajua na tunaendelea kukubali kuwa exploited? Kumbe tuna jua hii misaada siyo misaada lakini kila siku tuna tembeza bakuli?
   
 7. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #7
  Feb 24, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kama kweli waafrika tunataka kuendelea tuamke, hii biashara ya kutafuta mchawi kila kukicha wakati matatizo yetu tunayasababisha sisi wenyewe haitotufikisha popote!!!! Mtu kama ben Ally wa tunisia, na yeye tuseme kuwa ni njama za magharibi... tuachane kabisa na mawazo ya ki***zi ili tuweze kuendelea!!!!
   
 8. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #8
  Feb 24, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Ebu lete reference ya Bush akiongea hayo maneno? unaonekana kupoteza kumbukumbu ya hawa jamaa wanao lalamikiwa na wananchni yao, yaani hujui kuwa kinacho waponza ni dharau yao kwa wanachni ya chini? kujilimbikizia mali nyingi na kujisahau kiasi cha kufikia kuwa madaraka ni yake yeye na familia yake tu
   
 9. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #9
  Feb 24, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,112
  Likes Received: 461
  Trophy Points: 180
  Unachoongea si kweli labda kwa ushabiki tu!

  Ukweli ni kwamba population ya hizi nchi imebadilika na vijana wengi wanapenda uhuru badala ya hawa madicteta kuwatawala. Hakuna mtu duniani asiyependa democrasia!!. Kama ni mafuta wazingeanzia Tunisia na Egypt!! wangeanzia Saudi Arabia. Pili mimi naishi hapa Houston,TX kwa miaka 13 na kuna kampuni za mafuta kuliko sehemu yeyote duniani hapa lakini ukweli ni kwamba bei ya mafuta ikipanda sana haisaidii hii nchi kwasababu inapunguza mzunguko wa pesa hivyo kusema kwamba bei ikiwa juu sana ni nzuri kwa marekani si kweli hata Wall Street stock hazijapanda bali zimeshuka kwa 3%. Vilevile bei ikishuka sana si vizuri kwasababu kuna kampuni nyingi hapa hivyo kwa kiwango cha $80 kwa baro ni poa. Ni lazima tuelewe Africa nzima kuna mwamko wa vijana waliochoka madicteta na walarushwa hata Tanzania wapo na hawa vijana iko siku watachukua nchi. Hata Ghadafi yupo kwenye wakati mgumu never say never democrasia itashinda tu in a long run!!
   
 10. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #10
  Feb 24, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  udini
   
 11. H

  Haki JF-Expert Member

  #11
  Feb 24, 2011
  Joined: Jan 14, 2009
  Messages: 356
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wewe kwamba hizi population za nchi za kiarabu zimebadilika. Lakini mbona hatuoni mapinduzi Uganda, Zimbabwe? Je hamna vijana? Kwanini focus ya West ipo kwenye mtandao wa Mafuta tu? Kumbuka Egypt ni key point ya kusafirisha mafuta through suez canal.
  Mbona hatumuoni Anderson Cooper (CNN) Mwanza au Arusha?

  Soma head ya article, ni vigogo wa nchi ndiyo wanaopata faida ya mafuta yanapopanda bei.
  Unaposema mafuta yakipanda bei, Wall Street hainufaki siyo kweli. Kumbuka ni Supply na demand. Makampuni ya mafuta yanatajirika kwa sababu, wananunua mafuta wakati supply inapokuwa high and price inakuwa low. Wanachofanya ni kuexcess inventory.
  Baada ya hapo wanachofanya ni kuangalia Headlines za fujo, vita kutoka MidEast ili wapandishe bei.
  Kumbuka Katrina, makampuni ya mafuta yalitajirika kwa kupandisha bei kwa njia ya kupandisha bei bila ya sababu. Matokeo yake, kulikuwa na Congress hearing in USA kuhusu hiyo scam ambapo makapuni ya mafuta yalikiri kupandisha bei ya mafuta bila ya sababu.
   
 12. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #12
  Feb 24, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Wewe ni Muhuni wa mtaani tu unaye ganga njaa kwa lolote na chochote.
  Tuondolee udhia wako hapa.

   
 13. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #13
  Feb 24, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mkuu Haki nadhani ume soma hizo source zako bila kuchaganua mwenyewe. Una dai nchi za magharibi ndizo zime engineer mapinduzi ya nchia kama Tunisia, Egypt na sasa Libya. Ila una sahau kitu kimoja. Mubaraka alikua ally mkubwa wa Marekani na hata Israel. Na walikua wana jaribu kuta futa njia za kumuokoa behind closed doors na ndiyo maana in public walikuwa wana toa kauli neural bila kuonyesha wazi wazi kama wana support wananchi au Mubarak. Je una semaje juu ya hilo?
   
 14. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #14
  Feb 24, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Haki ni mlevi wa kahawa vijiweni ni vema tumpuuze.

   
 15. n

  niweze JF-Expert Member

  #15
  Feb 24, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  I think you got this wrong. I know there are some opportunists in the middle of all these revolutions but people are crying hard for democratic reforms and better lives. I can't see the proof in your words. Americans themselves don't like what they see and especially in Egypt. Lets support people who are seeking better lives because the time is here and we can't stop this moment. This is for Tanzanians too, lets walk up and enjoy the aromas of freedom.
   
 16. N

  Nonda JF-Expert Member

  #16
  Feb 24, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Mkuu.
  Mimi pia sikubisha kitu katika uliyoyasema.Wala sijawatetea viongozi wetu. Lakini nimeweka hiyo video ili tujue pia kuwa jamaa wababe huwa hawapendi kutuona tunautulivu na tunapiga hatua, wakipata mwanya wanaingia kuvurua ili wavune shamba la bibi...pia nimesema sisi kama wananchi tunaulea uovu wa viongozi wetu kwa muda mrefu bila ya kuwachukua hatua.
   
 17. M

  MushyNoel Senior Member

  #17
  Feb 24, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 104
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  Haki,

  Kaka nimependa thread yako . Naelewa sana janja ya hawa mazungu ( kama nyerere alivyopenda kuwaita ) .Walikutana wakatumia societies zao kutengeneza mfumo wa kifedha duniani . Wakaweka IMF ili maslai yao yaendelee kudumu .Ni kwa maslai yao tu wanasimama kidete .But the close we come to understand them,the close we will figure another way out of them.
   
 18. bona

  bona JF-Expert Member

  #18
  Feb 24, 2011
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  nchi nyingi za kiarabu zilikua zinapumbazwa kua magharibi ni wabaya na anti-islam kiasi viongizi wao walikua wanatumia opportunity hiyo kuwakandamiza wananchi wao na kujilimbikizia mali lakini sasa hali imefika pabaya uelewa umeongezeka na kigezo chao sasa haki hold water dhidi ya umaskini wa wanachi walio nao! ili liwe fundishpo jamani kwa wale watanzania wenzetu waliokua wanadhan kua nchi za kiarabu ni matajiri sana wananchi wake wote wako na hali nzuri kumbe ni kinyume kabisa umaskini uko mkali tu na watu sasa slogan ya kutokufuat mifumo ya west kua ina haribu uislam hai hold water mbele ya njaa!
   
 19. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #19
  Feb 24, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Unataka kusema waarabu hawana akili kuliko wazungu? Kwa kiasi kikubwa kama unaweza kudanganywa ina maana anayekudanganya kakuzidi maarifa.
   
 20. n

  nyantella JF-Expert Member

  #20
  Feb 24, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Hapo kwenye red ndugu ma brother/sister, soon they will be here!!!! Si unakumbuka Tz kuna Uranium ya kumwaga? watakuja tu. Tutaanza kuuana then wao kiulaini watakuja kutuamulia ugomvi wetu at our own cost! mbona zamani hukusikiaga hizi vurugu za sasa? just think of it.
   
Loading...