kibaravumba
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 6,635
- 7,005
Pamoja na mikoa mingine kuwa na kilimo chote cha korosho, chakula kama mpunga, mahindi, ufuta, alizeti n.k. hivi vyote ni bure tu kwani havilimwi Dar!
Tunaona migodi mikubwa ya dhahabu Geita, Bulyanhu, Buzwagi, North Mara, Tanzanite Mirerani, migodi ya makaa ya mawe, Mwadui diamond, gesi ya mtwara; vyote hivi si kitu ukiviweka pamoja bado ni kama tone tu ukilinganisha na uzalishaji wa Dar!
Michango ya wafanyakazi wa serikali na sekta binafsi kwa nchi nzima ni kidogo sana ukiichukua yote kwa pamoja ukilinganisha na zinazokusanywa Dar! Hili limenitisha!
Mifugo mingi kama ng'ombe, Mbuzi, kuku n.k. Mbuga za wanyama, utalii, samaki wa ziwa Victoria, mbona inaniwia vigumu kuelewa?
Zile tochi zote na faini za magari huku mikoani, nchi yenye watu milioni 50, faini hizi ni kidogo ukilinganisha na inayolipwa na watu wanaokadiriwa kuwa milioni sita tu wa Dar!
Hii lugha sijaielewa kabisa na kwa ujinga wangu nimeogopa sana kwa umaskini mkubwa uliopo mikoani, licha ya raslimali nyingi zilizoko huku.
Mwenye kunifafanulia naomba anisaidie. Kumbe inawezekana Dar hawapendelewi kimaendeleo, ni haki yao iwapo 80% ya mapato ya Serikali yanatoka Dar.