Revealing: Nani wametoa vibali vya kuishi/kufanya kazi kwa watu hawa?

Danniair

JF-Expert Member
Feb 18, 2011
360
66
Wana JF,

Imefika wakati sisi wenye nchi tuseme ni akina nani, (tuwataje kwa majina pamoja na mambo mengine wanaofanya haya):

-Wanawanyima wazawa ajira na kuwapa wageni (hasa waasia) na wapi walipo. mf. masonara waasia weusi waliofungiwa mtaa wa Indira Ghandhi tujue ni nani (M-tz) kawapa kibali cha kufanya kazi hizo.

-Wachina wanaofanya kazi cha kuchoma magrill badala ya wazawa mf.kampuni ya Hu Tuo iliyoko Msasani. Je, sisi hatuwezi kazi hizo au tumalize madigirii yetu na kwenda kuajiliwa huko kwani nyumba karibia zote zinazojengwa Dar grill zinatengenezwa na wachina. Vile vile frem karibia zote ktkt mwa jiji zinarembeshwa na wachina!!!!!

- Wachina wanaosukuma mikokoteni nani kawaleta humu Tz kufanya hayo? Tunawajua: Jf tuwekeeni nafasi maalumu tuwataje hawa wa-Tz wenzetu wapenda rushwa huku wakituangamiza kwa kuwathamini wageni na kudhalilisha wazawa. Hawa wa-tz wasio na utu wenye kuangalia mifuko yao wakiisahau jamii yao nyuma.

-Waasia waliojificha huko viwandani keko/chang'ombe (nasikia sijawaona).

-Wakenya na waganda eti kwa kuwa wanajua kiingereza kutupita.

-Wachimba madini yetu, mf. nasikia huko Morogoro kuwa wanaojiita wamisionari lakini usiku ni wachimba madini yetu. Tuwataje kwa majina ili kumsaidia rais na kuzilinda mali zetu.

- n.k, n.k, n.k...
 
Thanx very much, binafsi mimi naishi nao naona kama hawa waasia wamekuwa juu sana ktk hili. La ajabu kila mmoja ana polisi wake wa kumwita mara wanapogombana. Ukipita pale Golden Plaza utaona uchungu sana. Wao wamo ndani waafrika wamekaa NJE marangoni.

Vivyo hivyo maduka mengi tu. Ukienda ktk baadhi ya ofisi za serikali utawakuta wameanza nako. Lakini hawataki jeshi, polisi, ualimu vijijini au udaktari vijijini.

Nenda migahawa ya kichina, kule utawakuta hata sex servants wa kichina-Mgahawa Tangren (kule iliko nyumba ya rais maeneo ya moroko kuelekea victoria na kawe. Nadhani mtaa unaitwa UNUNIO au..Uuu, sikumbuki vizuri)
 
Nenda k'koo kaone wachina wanavyofanya kazi za wazawa mpaka kupiga picha za paspot na kuuza vyombo na mapazia.

Haya ndo matokeo ya serikali dhaifu.

Serikali imara ingeweka vigezo vya kumruhusu mgeni kuja kuwekeza nchini, mfano awe na mtaji usio pungua 100m kiasi kwamba anaweza kuajiri wabongo. Hii ni kuacha nafasi ya uwekezaji wa mdogomdogo kwa wabongo wenyewe wenye mitaji midogo ya vikoba, Saccos, NMB, Access Bank, Kiinua mgongo, nk.
 
Hili ni tatizo kubwa sana katika nchi yetu kwasasa,sijui hawa magamba wawalioni? Wizara ya kazi na Ajira wapo wapi? au ndiyo hiyo 10%? Nadhani kuna haja yakulifanyia kazi hili jambo hata kwa nguvu ya Umma maana naona tuliowapa uongozi wanatupeleka msobemsobe!

Hapa Morogoro kuna hivi viwanda vya Tumbaku kuan wazungu hapo wanajiita "Maexpert" hili neno Expert lina maana zifuatazo Skilled,Skillful,Professional,Knowledgeable na hizi ziwe skills ambazo watz hatuna,Sasa utakuta Mzungu alikuwa Plumber then anakuja humu anhongahonga huko idara ya kazi na uhamiaji anafanya kazi kama Meneja wakati hata ABC za management hana,sasa huu ni udhaifu wa serikaili dhaifu na viongozi dhaifu wa Magamba.

Hili ni janga la uhakika,ipo siku litalipuka tu!
 
Nashangaa sana kuwakuta kariakoo nao wakibeba mabokis

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Wabongo kazi za kujiajiri hatuwezi wengi tukishapata ka-degree kamoja kutwa kucha na bahasha unatafuta kazi za kuajiriwa.Kwani kabla hao wachina na wahindi hawajaja kwanini nyie wabongo msizifanye hizo shughuli.?

Tafuta frem na wewe fungua uwape ushindani kama unaweza. WACHA KULALAMIKA WACHINA WANATOA HUDUMA NZURI SANA.
 
Wachina kuwagusa inakuwa ngumu sana maana sera yao ni kutapakaa duniani maana kule kwao wapo wengi.

Hivi juzi tu China imesaini mabilioni ya mikopo kwa nchi za Africa sasa sijui kama wanashikika kirahisi hawa.
 
HR Manager wa NIC BANK TANZANIA LIMITED (Mhindi na certificate ya usecretary), pia kuna Muchiri (Mkenya) ni wabaguzi kinyama. Kila kukicha wahindi wanaajiriwa kwa mishahara minono ila Mtanzania anakula clerk wages hata kama una Masters.
 
Danniair

Funguka mkuu, hapa JF una nafasi ya kutosha, nafsi uliyotumia kuandika hii post ni tosha kabisa kushusha majina!
 
Last edited by a moderator:
Nenda k'koo kaone wachina wanavyofanya kazi za wazawa mpaka kupiga picha za paspot na kuuza vyombo na mapazia.

Haya ndo matokeo ya serikali dhaifu.

Serikali imara ingeweka vigezo vya kumruhusu mgeni kuja kuwekeza nchini, mfano awe na mtaji usio pungua 100m kiasi kwamba anaweza kuajiri wabongo. Hii ni kuacha nafasi ya uwekezaji wa mdogomdogo kwa wabongo wenyewe wenye mitaji midogo ya vikoba, Saccos, NMB, Access Bank, Kiinua mgongo, nk.

demand supply theory ndo inamajibu ya hiki mukinenancho, wazawa tumelala mno, tunafanya kazi hovyohovyo, wacha waje watuchangamshe.
 
POLISI na UHAMIAJI wapo macho na hawajashindwa kuwatambua hao wahamiaji haramu, lkn sote tunajua kwa nini hawawakamati - kwa kua wamefanya ndio maduka yao ya kuchukua pesa na kila Polisi/Uhamiaji ana wachina wake, wahindi wake, nk.

Sio Polisi tu, pia siasa za makabila na udini Tanzania hapunguza nguvu ya pamoja na tunaona siri na raha kufanya biashara ama kumfanyia kazi Mchina ama Mhindi. Matokeo ni Wachina na Wahindi kuwin kirahisi.

Watu makini wenye Uongozi ndani ya CCM hawana vichwa vyenye uwezo wa kubadirisha hii hali maana walishaharibiwa na mfumo wa CCM yenyewe.
 
Watanzania kwa kulalamika tumezidi, nyie mmeshindwa kubeba maboksi kariakoo, wachina wameona dili na wanabeba ayo maboksi mnaanza kulalamika.

Watanzania wengi hasa wenye degree hupenda kulalamika na kuzurula miaka na miaka kuomba kazi, wengi wanataka wakae ofisini, wachina na waindi ni mahustler,watafutaj awachagui kazi kama sisi watanzania,tunaopenda kulalamika ovyo,mim niliona kwa macho yangu wachina wakiuza ice cream barabaran dar na wanauza sana kwa sababu ya hali ya ewa ya joto la Dar.

Vijana wa kitanzania tunapenda starehe na usharobaro umezidi na ndio unatuponza na kusababisha kuanza kuchagua kazi sababu ya kupata degree.

Hakuna kingine tunafikiria zaidi ya kuzurula kwa maofis ya watu kuomba kazi na wadada wetu kujiraisisha kwa wanaume wapate hela, tunapenda vitu vywa bwerere (bure), wengi tunapenda kulelewa tu.

Kwa serikali nayo inatakiwa kabla aijatoa kibali cha mgeni kufanya kazi lazima ifatilia ni kazi gani mtu anataka kufanya kulingana na sheria ambazo zipo kama zinaruhusu ni sawa tu.

Mwisho vijana tuache kulalamika tutoe stress zetu kwa kufanya kazi na kuwa wabunifu.
 
Uwepo wa wageni kwenye soko la ajira na biashara unatoa mwanya kwa wazawa kujifunza tabia mpya na kujiongezea uwezo wakushindana.
Cha kujiuliza ni je, iwaje mtu asafiri maili kibao aje nchini kwako na kujifunza lugha yako na mitaa yako halafu akushinde kupata kazi au kuuza mahindi aliyolima mjomba wako? Where is our weakness? - hapo ndio tujikite kupashughulikia.
 
Nchi iko kwenye AUTOPILOT tutegemee nini zaidi? JK yuko kanada anapanda mikokoteni ya farasi
 
Back
Top Bottom