Revealed: Viongozi Jukwaa la Wahariri walimwalika Nchimbi katika maandamano

Ama kweli weye mwana mpotevu. Wewe ndo umethibitishiwa na hao watu hatukatai. Sasa wewe unafikiri kwa kusema hivyo tu inatosha kututhibitishia sisi wenye akili zetui timamu. Lete documentation au any sort of proof kama wafanyavyo wenzako la sivyo mi naita hiyo ni vapour na mara zote hupita na upepo tu

kila kitu hupita kama upepo Tanzania hii,

pia hulazimishwi kukubali, just shake ur head before use
 
Sijapata kusikia mtu akipewa mwaliko wa kwenda msibani! Tena msiba unaomhusu,ulio ndani ya himaya yake.Sidhani kama kuna kitu kama hicho ukizingatia kuwa Nchimbi ni waziri na wizara anayoiongoza ndiyo iliyofanya mafyongo na waandishi wa habari hawakutaka kumwona akiwepo pale akijifanya kuomboleza pamoja nao.

Mfumo mzima wa kiprotocol uliotumika siku waziri alipotimuliwa na kuondoka kwa aibu unaonyesha wazi kabisa kuwa hakualikwa. Ni kwa nini siku hizi misiba,makanisa na vyombo vya habari vinatumika sana na viongozi au watu maarufu katika kutafuta umaarufu au kujulikana zaidi?

Utandawazi umeishatuharibu. Hatuwezi kwenda misibani kama waombolezaji, wala kutafakari zamu zetu za kuwekwa katika nyumba ya milele zitakapofika tutaombolezwaje na kukumbukwa.
 
Meena kweli alikula mlungura , kwani hata nilipo sikia hotuba yake, haikulingana na mtu ambaye anamsiba. tutafika mahali kupata pesa ili wenzetu wafe
 
Kama kweli Comrade Dr. Emmanuel Nchimbi alivamia bila mwaliko uwao wote: formal or informal basi alienda kujidhalilisha na alidhalilika kiasi cha kutosha kwa kukataliwa na kuzomewa na waandishi. Lakini kama Comrade Nchimbi alikuwa na mwaliko uwao wote: formal or informal toka kwa Meena basi Meena atakuwa ni mnafiki wa hali ya juu na huo unafiki utamsuta hadi anakutana na muumba wake. Lakini kama wote wako sahihi nasi mungu awasamehe nami pia nipate rehema za mungu.
 
Meena kweli alikula mlungura , kwani hata nilipo sikia hotuba yake, haikulingana na mtu ambaye anamsiba. tutafika mahali kupata pesa ili wenzetu wafe

Mimi nilibahatika kumuona kupitia TV akiwa anaongea kabla/baada ya Jane Mihanji kuongea. Nilisoma kitu machoni na mikononi mwake, alikuwa akitetema;labda kwa hofu ya kuwa double agent.
 
Waziri dhaifu ndo maana alikubali kualikwa 'kihuni' bila barua.

Ila Tz mawaziri wakishazoea wizara zao wakibadilishwa si flexible.JK bado hajasahau wizara ya mambo ya nje haju kuwa sasa yeye ni rais,huyu naye hajasahu wizara yake iliyokuwa ikimweka katika part usiku na kulikwa na camera.

This time hakujua wameba camera walikuwa busy na issue zao,kanjanja aliyepewa hela akamdanganya kuwa aje atamchomeka ghafla kama surprise.

Hizi tabia hawakujifunza kule arumeru, surprises zao makanisani ziliwatokea puani.Surprises zina wenyewe. kajikuta surprise ya kudhalilisha ikiwa kinyume chake.
 
Vyovyote vile; awe alialikwa au la, KWA AIBU ILE, MIMI NINGEJIUZULU KWANI ALIONYESHWA JINSI ASIVYOKUBALIKA!!!
 
kila kitu hupita kama upepo Tanzania hii,

pia hulazimishwi kukubali, just shake ur head before use

kuishi kwa mazoea ni taabu kubwa iliyo zaidi ya taabu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Hakuna awezaye yote hapa duniani anayeweza kuwaza/kufikiri kwa niaba yangu. Nafikiri kwa kadri ya uwezo wa utashi wangu niliojaaliwa na Mwenyezi Mungu. Najua lipi baya na lipi zuri. Wewe endelea kuwaachia hao unaowaamini wafikirie kwa niaba yako.
 
Sifa , njaa na woga ndio uliomfanya amwalike kama ni kweli. Kwa upande mwingine anatetea zawadi alizopewa kwenye sherehe za waandishi bora.
 
Back
Top Bottom