REVEALED: Muhingo Rweyemamu aligushi jina na kujiita Paji Mihami! | Page 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

REVEALED: Muhingo Rweyemamu aligushi jina na kujiita Paji Mihami!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by OgwaluMapesa, Aug 26, 2010.

 1. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #1
  Aug 26, 2010
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Habari zilizozipata kutoka kwa wazee wa UWT ni kuwa Muhingo Rweyemamu aliwahi kughushi jina ili kujiendeleza kielimu,jina lake halisi ni paji Mihami,Mpo hapo??
   
 2. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #21
  Aug 26, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 4,026
  Likes Received: 462
  Trophy Points: 180
  Jamani wachawi wala nyama za watu wanaanza kujitokeza! ?
  Hivi tulifahamu kuwa magazeti ya New Habari ni ya RA na ukitumikia hapo hata kama hakuna intergrity unapanda na kwenda mbele, what is happening to our sense of direction?
  Mtu anayetumika kwa makusudi yasiyofaa lakini mradi mkono uende kinywani, huo ni kuuza utu wako.
  Sasa cha kusikitisha ni kuwa huyo Muhingo kastukiwa na wenziwe, nafikiri hapa there is more water flowing over the river than it is actually ackowledged.
   
 3. m

  mapambano JF-Expert Member

  #22
  Aug 27, 2010
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waandishi wa habari Tanzania nao wamo, wengi wao ni njaa zinawasumbua na kutofahamu kazi zao vizuri...Kwa mfano, Shigongo, ni kati ya watu waliofanikiwa kwa ujanja ujanja kupitia kasoro za system nzima ya hii nchi, leo hii hawa watu wanaonekana ni watu wakuigwa mfano. Leo ni mwandishi wa habari, kesho ni mgombea... Magezeti/waandishi wanaingia katika siasa kwa sababu ya rudhuku wanazozipata na kusahau kazi zao.
  Tuna vilaza wajanja wengi kwenye maofisi yetu sasa, mambo yanayojitokeza sasa, kugushi VYETI, FAKE DEGREES, MAJINA nk. Hawa walitakiwa wawe magereza!
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #23
  Aug 27, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,759
  Trophy Points: 280
  .
  Mchukia Fisadi, kwanza naheshimu msimamo wako, ila pia nakuomba na kukusihi sana tutenganishe facts na falacies, facts ni kitu ambacho kipo, huwezi kupinga au kubisha, kama baada ya mchana, lazima usiku utaingia, au haa upende vipi usiku udumu milele, lazima kutakucha. Falacy ni hisia na mtu ambazo zio lazima ziwe based kwenye facts.

  Hivyo mtu kama ni kichwa, its a fact, haijalishi anamtumikia nani, atabaki kuwa kichwa and that is a fact, ndio maana nikasema namkubali jamaa kama kichwa, japo anatumika kwa fisadi papa, kama ninavyomkubali Jacton ambaye pia ni kichwa na ni mtumishi mwaminifu wa fisadi papa, kama vile vichwa kwenye payroll ya nyangumi, kule nako kuna mlolongo mrefu wa vilaza wake.

  Adolf Hitler aliwaangamiza Mazayuni kwa vile ni vichwa, ila pia imethibitika, waliobuni concetration chembers, ni hao hao Mazayuni waliokuwa wakimtumikia Hitler kwa uaminifu mkubwa. Pamoja na madhambi yote aliyowafanyia na kuwaangamiza kadri alivyoweza, hawa jamaa wamebakia kuwa vichwa karibu duniani kote, ukiondoa Bara Asia, na huwezi amini, kuna uwezekano, hata waliobuni September 11 kule US ni Mazayuni, japo mtekelezaji ni Osoma ndio maana siku hiyo inasemekana hakuna aliyeripoti kazini. Hivyo hoja ya nani anamtumikia nani, haina nguvu.

  Kitu ambacho nakubaliana na wewe, ni ile concept ya 'ganda la mua la jana, chungu aona kivuno', hivyo kiwango nani ni kichwa na nani sio kichwa ni relative. Yule ambaye mimi naweza kumuona kichwa, kwa mtazamo wa mwingine, ni kilaza wa kutupwa, na yule wengine wanaowaona kama vilaza, ni vichwa funika bovu kwa wengine ni vichwa tukuka.
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #24
  Aug 27, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,759
  Trophy Points: 280
  mapambano, kuweka records clear, siyo kila anayeandika ni mwandishi wa habari, kwa kumbukumbu zangu, Shigongo siyo mwandishi wa habari, bali ni mmiliki wa Global Publishers kama alivyo Mengi na Dialo, wao sio waandishi wao ni wamiliki. Ila Shigongo ni mwandishi mwenye kipaji cha kuandika.

  Kwa wafuatiliaji, mtakubaliana na mimi, kuwa Shigongo hakufanikiwa kwa ujanja ujanja, alianzia mbali kwa kujituma na anaendelea kujituma na nikimuangalia, bado ana very bright future japo binafsi sikubaliani na mauza uza na mauchafu ya magazeti yake ambayo siku hizi magazeti ya udaku yamebatizwa jina la 'magazeti pendwa', na huwezi amini, kwenye ubao wa magazeti pake UDSM kwa wasomi, ni magazeti ya udaku ndio hutangulia kumalizika kwenye ubao, huku serious papers zikidoda na kulala.
   
 6. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #25
  Aug 27, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 23,115
  Likes Received: 6,757
  Trophy Points: 280
  Kumaharibia vipi?....kama kafoji watu wakae kimya....hicho kitumbua unachokitetea kakipata halali....kama ni cha dhuluma wacha kiingie matope
   
 7. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #26
  Aug 27, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,759
  Trophy Points: 280
  .
  Lole, hawa wachawi wala nyama za watu sio tunaanza kujitokeza, tupo, tulikuwepo na tutaendelea kuwepo kwa sababu tuu, sio kila mmoja wetu anaweza to call a spade a spade, ila kwa waliosoma riwaya ya 'An enemy of the people', anasema 'The strongest man in the world, is the one who stands alone' hivyo kwenye hao wachawi, count me in.

  Kama Mtu kutumika kwa makusudi yasiyofaa lakini mradi mkono uende kinywani, huo ni kuuza utu wako, wako wengi wemeuza utu wao na amini nakuambia ni mtindo huu ndio umemuingiza JK ikulu, na ndio huu huu utaendelea kutumika kwenye kampeni na pia ndio moja ya oparative mechanisim ya TISS, kutumika vibaya kuhakikisha wasiofaa wanaendelea kututawala ili hao wasiofaa waendelee kuula na mikono yao iende kinywani. Hiyo yote haya hayaondoi fact za uwezo binafsi wa mtu, ukioachana na paper works ambayo siyo issue.
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #27
  Aug 27, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,759
  Trophy Points: 280
  Safari_ni_Safari, sitaki nionekane kama mtetezi wa forgery, bali mleta habari ameileta ikiwa haijakamilika hivyo kuonekana kama majungu fulani.
  Kupata kitumbua kihalali ni issue moja na dhuluma ni nyingine, jee waliongia magogoni kwa njia hizo hizo ni halali au?.

  Ila pia kuna wapambanaji na wapiganaji wa aina mbili, wale wanaopigania maslahi ya taifa, na wale wanaopigania nafsi zao, hata kama wetu wetu tunapigania maslahi ya taifa, tusiwazushie hawa wachumia tumbo, waacheni ama waendelee kujilia vyao, ama kuendekeza njaa zao bila kuwazingizia.

  Hoja zozote za forgery, lazima ziambatane na facts.
   
 9. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #28
  Aug 27, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,759
  Trophy Points: 280
  ,
  Chakaza, sio lazima ndio yeye awe Salva, bali ukikaa karibu na wafalme, nawe ni lazima utanukia japo manukato ya kifalme, kiumri kamanda huyu, mchana umeshapita, anaelekea jioni, hivyo siyo vibaya akapata fursa ya kuandaa kitanda kabla giza halijaingia, tena afadhali yeye kajiwahi mapeni, kwenye hii fani ya uandishi, wengi wao hukumbuka shuka kumekucha.
   
 10. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #29
  Aug 27, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,759
  Trophy Points: 280
  MawazoMatatu, kuwaita makanjanja, waandishi wa ukweli, sio kuwatendea haki, hata kama hatukubaliani na wamiliki wao. Wapo baadhi ya wamiliki ambao vyombo vyao viko mtari wa mbele kwenye vita dhidi ya ufisadi lakini nao wana yao, kama ulibahatika kuusoma ule waraka wa Sakina, nadhani kweli hili utanielewa.

  Jamani iwe kweli alifoji au hakufoji, mlengwa hapa sio kanjanja, na pili uwezo wa kazi ya uandishi, anao, tatizo labda liwe ni kumtumikia kafiri, apate mradi wake, kwani wako waandishi wangapi ni vibaraka?., jamani hizi njaa hizi, zitatuponza!.
   
 11. R

  Ramos JF-Expert Member

  #30
  Aug 27, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nimefurahishwa sana na kitendo cha Muhingo kumfukuza huyo mwandishi wa Mwananchi. Hii ni kwa sababu kwa kufanya hivyo ametuwezesha kujua mengi, kumbe waandishi wa vyombo vya habari vya 'kujitegemea' wanavishwa jezi na ikulu! Kumbe wanalipiwa usafiri! Inawezekana hata Per DM wanalipwa!

  Sasa haya tungeyajuaje kama asingefukuzwa? Actually inawezekana hata safari za kabla ya hapo huyo jamaa 'alijumuishwa' katika msafara, sasa akaharibu alipoandika lile la JK kuhaha kuondoa mpasuo CCM. Kumbe angeweza akaonywa tu bila kufukuzwa na akaendelea 'kujumuishwa' na akakaa kimya.

  Ndo maana magazeti mengine yote naona yameamua kufumbia macho ishu za muhimu kwenye hizo kampeni za JK. Hata Tz Daima, naona wanakomalia tu suala la kufukiwa wachimbaji wadogo (ni muhimu of coz) na habari toka kwa Slaa, hakuna kabisa mwenendo wa kampeni za JK. Ina maana nao 'wamejumuishwa"?

  Naomba JF nayo ipeleke mwandishi wake ambaye tutamsihi asikubali 'kujumuishwa'.

  Baada ya kutimuliwa Mwananchi, najua ikulu haitafanya makosa kwani hata leo wamekanusha sana. Najua baada ya mda mwandishi wa Mwananchi atatafutwa, atapelekwa baa, atakatiwa kiasi, ataambiwa yameisha, actually wewe ni mtu muhimu sana na tunaomba kesho tuwe pamoja kwenye 'msafara', atakabidhiwa kitop cha "kikwete Press 2010" (kama alichokuwa nacho kabla hajaandika ile stori nadhani, naye atakuwa mmoja wao...
   
 12. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #31
  Aug 27, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,801
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Mkuu, Pasco. Ninavyofahamu mimi ni kuwa sifa mojawapo, kama sio kuu, ya mtu kuwa kichwa ni uwezo wake wa kuchanganua mambo, kujua baya na zuri na kusimama mahali ambapo watu wakikuangalia hawawezi kuhoji 'Ukichwa' wako. Sasa hivi Tanzania haisemwi lakini niwazi kuwa tumejitenga kwenye kambi mbili kubwa za Wasiopenda jinsi nchi yetu inavyoendeshwa na Wanaoona sawa tu ilimradi mikono yao na inakwenda kinywani. Mafisadi na Walalahoi. You are either with them or with Us.You cant eat your cake and have it. Kama mtu unashindwa kuchanganua mambo na kujua baya na zuri, kati ya kufa na Mafisadi ama kufa na walalahoi, ni upi basi 'Ukichwa' wako? Huo wa kuongozwa na tumbo linavyotaka??? 'Ukichwa' ni zaidi ya madarasa na Vitabu ulivyosoma. Ni Upeo wako wa kuchanganua mambo.
   
 13. e

  enterpreneur New Member

  #32
  Aug 27, 2010
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii siyo kweli. Mimi namjua sana huyo Bwana Muhingo. Upande wa kielimu amekuwa akiyatumia majina hayo mawili yaani Muhingo Rweyemamu. Naujue kwamba huyu ni NSHOMERE upto University of Tumaini with vast experience as an editor. Wakora Bojo
   
 14. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #33
  Aug 27, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,328
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Duh tunakoelekea utasikia oyaaa utotoni ulikua waitwa Soda Nitakutapika, wewe sio raia
   
 15. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #34
  Sep 3, 2017
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,568
  Likes Received: 1,740
  Trophy Points: 280
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...