REVEALED: Muhingo Rweyemamu aligushi jina na kujiita Paji Mihami! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

REVEALED: Muhingo Rweyemamu aligushi jina na kujiita Paji Mihami!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by OgwaluMapesa, Aug 26, 2010.

 1. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #1
  Aug 26, 2010
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Habari zilizozipata kutoka kwa wazee wa UWT ni kuwa Muhingo Rweyemamu aliwahi kughushi jina ili kujiendeleza kielimu,jina lake halisi ni paji Mihami,Mpo hapo??
   
 2. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #2
  Aug 26, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,437
  Likes Received: 380
  Trophy Points: 180
  hehehe
  hii ishu ya uraia walah itatutoa knock out wengi sana hapa
   
 3. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #3
  Aug 26, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,848
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  Asante mkuu, hebu tumpekue huyu rasmi kabisa. Mwaga mtama kuku wale. Ikiwezekana mkipata makaratasi yake dondosheni hapa, ziwe ni facts ati.

   
 4. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #4
  Aug 26, 2010
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Na Kizitto Noya, Mwananchi

  WAANDISHI wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) wamefukuzwa kwenye kampeni za kumnadi mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete.

  Ray Naluyaga, ambaye anaandikia gazeti la The Citizen, na Frederick Katulanda wa Mwananchi, walifukuzwa kwa nyakati tofauti kwenye kampeni zilizofanywa katika mikoa ya Geita na Kagera.

  Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba alikanusha chama hicho kutimua waandishi kwenye msafara wa Kikwete akisema anaamini waandishi hao wamefukuzwa na mtu aliyemwita kuwa ni mhuni na si CCM kama chama.

  Waandishi hao walifukuzwa kutokana na chama hicho kueleza kutofurahishwa na habari iliyoripotiwa na gazeti hili juzi ikiwa na kichwa kisemacho "JK ahaha kunusuru mpasuko CCM".

  Akielezea mkasa huo, Naluyaga alisema alifukuzwa Ikulu saa 1:30 asubuhi jana mjini Bukoba ambako msafara wa mgombea huyo ulipokuwa ukijiandaa kwa safari ya kuelekea Wilaya ya Misenyi.

  "Mimi nilifika Ikulu leo (jana) saa1:30 na kukuta waandishi wenzangu wakiwa wamevalia jaketi zilizoandikwa 'Kikwete Press 2010," alisema Naluyaga na kuongeza:

  "Nikaenda kuripoti kwa (Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais) Salva Rweyemamu, lakini yeye akaniambia nimsubiri (mratibu wa habari wa timu ya Kikwete) Muhingo (Rweyemamu) kwa kuwa yeye (Salva) ni mshauri tu wa masuala ya habari."

  Naluyaga alisema baada ya Muhingo, Mhariri Mtendaji wa magazeti ya New Habari Corporation ambaye sasa anafanya uratibu wa kampeni za urais za CCM, kuwasili alimtaka aendelee kusubiri kwa kuwa jina lake limepelekwa Ikulu kujadiliwa kwanza.

  Muhingo, ambaye kampuni yake huzalisha magazeti ya Mtanzania, Rai, Bingwa na The African, pia alikuwepo kwenye timu ya kampeni ya Kikwete mwaka 2005 wakati mwenyekiti huyo wa CCM akiwania kuingia Ikulu kwa mara ya kwanza.

  Katika kampeni za mwaka 2005, Muhingo alimfukuza mwandishi wa Mwananchi baada ya kutofurahishwa na habari alizokuwa akiandika.

  "Msafara unaanza na yeye (Muhingo) akaendelea kuniambia subiri; subiri; subiri. Baadaye akasema suala langu ni gumu hivyo siwezi kwenda na msafara wao," alisema Naluyaga na kubainisha kuwa ndani ya Ikulu hiyo kulikuwa na makada kadhaa wa CCM, akiwamo mwenyekiti Kikwete, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Khamis Kagasheki na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Deodorous Kamala.

  Alisema ingawa Muhingo hakumweleza sababu za jina lake kupelekwa Ikulu kujadiliwa, makada mbalimbali wa CCM walimwambia kuwa tatizo ilikuwa habari iliyoripotiwa na gazeti hili juzi.

  "Wengine walisema kampuni ya Mwananchi ni hatari sana kwa sababu ni kampuni binafsi inafanya kazi zake bila upendeleo. Lakini kama issue (suala) ni kampuni binafsi, mbona kulikuwa na waandishi wengi wa kampuni binafsi," alihoji Naluyaga.

  Lakini jana Muhingo alikanusha kumfukuza Naluyaga akisema "Atakuwa amekwambia uongo. Kwa nini nimfukuze mwandishi? After all (zaidi ya yote) tunahitaji coverage (taarifa zitoke)".

  Muhingo alieleza kuwa ni kweli alimwacha Naluyaga Ikulu ndogo ya mjini Bukoba, lakini si kwa sababu hakutaka aripoti matukio ya kampeni za CCM bali ni kwa sababu ya uhaba wa magari ya kusafiria.

  "Tulitegemea tuwe na magari mawili ya waandishi, lakini tukapata moja tu na mimi nilikuwa na waandishi kumi niliotoka nao Dar es Salaam sasa katika mazingira hayo, unamchukua aliyeanzia Bukoba ama, unaendelea na wale ulioanza nao Dar es Salaam,"alihoji Muhingo.

  Awali Katulanda alisema alidokezwa suala la kufukuzwa kwa waandishi wa Mwananchi juzi na Muhingo majira ya saa 4:00 asubuhi wakati Kikwete alipokuwa anahutubia kwenye Uwanja wa Katoro mjini Geita.

  Alisema siku hiyo mara baada ya Kikwete kupanda jukwaani na kuanza kuhutubia, aliitwa na Muhingo, anayeshughulikia mambo ya habari.

  "Akaniambia twende huku. Nikamuuliza wapi? Akasema twende. Akanipeleka mahala ambako nisingeweza kumsikiliza Kikwete anavyozungumza na kuniuliza:
  "Kwa nini umeandika habari hiyo? Wewe huoni unatuharibia? Kuna vitu vingi vya kuandika ikiwamo wilaya mpya kuanzishwa mwezi Januari, lakini bado uliona hiyo ndio habari. Mimi ni mtu muhimu hata huko Mwananchi; jina langu limo kwenye usajili wa gazeti lenu na nitakufukuza kwenye msafara wetu," alieleza Katulanda akimnukuu Muhingo.

  Katulanda alisema maswali hayo yaliibua mvutano kati yake na Muhingo hasa pale aliposisitiza kuwa anaamini alichoandika ndicho wananchi wanachopaswa kujua.

  Katulanda alisema kuwa Muhingo alidai habari iliyoripotiwa na gazeti hili juzi kwamba Kikwete alitumia mkutano wa kampeni kwenye Jimbo la Buchosa kutuliza wimbi la mpasuko unaoonekana kukikumba chama hicho tawala baada ya kumalizika kwa kura za maoni za kuteua wagombea ubunge na udiwani zilizosababisha wanachama wengi kukimbilia upinzani.

  Akizungumza na Mwananchi, Makamba alisema: "Ili uamuzi uwe wa chama lazima ufikiwe na Kamati Kuu, Nec au uamuzi afanye katibu mkuu. Vikao hivi havikufanyika kokote na mimi (katibu mkuu) sijaagiza mtu awafukuze waandishi. Fuatilia vizuri habari yako, utagundua tu kwamba yupo mhuni amekosana nao akaamua kuwafukuza."

  Mhariri Mtendaji wa magazeti ya MCL, Theophil Makunga alieleza kusikitishwa na kitendo cha mratibu wa habari wa kampeni za CCM kuwafukuza waandishi wake, akisema kuwa kampuni haikutegemea kitendo hicho kufanywa na CCM.

  "Sishangai sana kwani hata mwaka 2005 walimfukuza mwandishi wetu maeneo ya Ngara. Lakini nasikitika na sikutegemea hilo kufanywa na chama makini kama CCM," alisema Makunga na kuongeza.

  "Hata hivyo bado ninawahakikishia wasomaji wa magazeti yetu kwamba tutafanya kila liwezekanalo kuwaletea habari zote zinazohusu kampeni zote, zikiwemo kampeni za CCM," alisema. MCL inachapisha magazeti ya Mwananchi, Mwananchi Jumapili, The Citizen, Sunday Citizen na Mwanaspoti.

  Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM, John Chiligati alisema hana taarifa ya tukio hilo na akalitaka gazeti hili liwasiliane na mratibu wa kampeni za chama hicho, Abdurhaman Kinana au Katibu Mkuu, Yusuf Makamba kwa maelezo zaidi.

  Jana kutwa nzima, Kinana hakupatikana kuzungumzia suala hilo.

  Habari inayoelezwa kulalamikiwa na CCM iliripotiwa na gazeti hili juzi kwamba Kikwete alitumia jukwaa la kampeni kunusuru mpasuko wa wanachama wanaohamia vyama vya upinzani kupinga matokeo ya kura za maoni za kupata wagombea ubunge na udiwani, akiwataka waige mfano wake wa uvumilivu.

  Kikwete alisema hayo alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Tarafa ya Nyehunge.

  Alisema wanachama walioshindwa hawana budi kutulia na kuwapigia kampeni wagombea waliopita kupeperusha bendera ya chama hicho ili kishinde uchaguzi.

  Alikuwa ameshtushwa na kitendo cha mbunge wa zamani wa Jimbo la Busega, Dk Raphael Chegeni kutoonekana katika msafara ulioenda kumlaki alipowasili na pia kutoonekana kwenye mkutano wa hadhara kwenye jimbo hilo ambalo makada wanne wa CCM wamefungua kesi kumpinga mgombea wa CCM, Dk Charles Tizeba.

  Kikwete alisema kuwa walioshindwa hawana budi kuiga mfano wake kwa kuwa baada ya kushindwa na Benjamin Mkapa mwaka 1995 kuwania tiketi ya CCM ya kugombea urais, alivumilia na mwaka 2005 akapata nafasi hiyo kwa ushindi wa kishindo.

  Kikwete aliongoza awamu ya kwanza ya kura za maoni za kutafuta mgombea urais wa CCM mwaka 1995, lakini katika awamu ya pili aliangushwa na Benjamin Mkapa ambaye baadaye alishinda uchaguzi na kuwa rais wa serikali ya awamu ya tatu.

  Kikwete aliingia tena kwenye kinyang'anyiro cha kutafuta urais kwa tiketi ya CCM na kushinda kwa kishindo kwenye kura za maoni za chama hicho mwaka 2005.

  Chanzo: Mwananchi

  Duhu!! Paji Mihami a.k.a Muhingo Rweyemamu Report ya Veting ya Ma DC 2006 ilimuhumbua
   
 5. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #5
  Aug 26, 2010
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Duhu!! Paji Mihami a.k.a Muhingo Rweyemamu Report ya Veting ya Ma DC 2006 ilimuhumbua [​IMG] [​IMG] Reply W
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Aug 26, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,762
  Trophy Points: 280
  OgwaluMapesa, hizi ni tuhuma tuu, kama usipozijengea hoja za kutosha, zitaishia kuwa majungu tuu ya kutaka kumuharibia Muhingo, haswa baada ya kuitwa tena kwenye timu ya kuratibu media kwenye kampeni ya JK.

  Alifanya kazi hiyo kwa umahiri mkubwa mwaka 2005 huku Salva akisimami pale editorial, sisi wengine tukitegemea, baada ya kazi nzuri, ataitwa jikoni, kumbe la, aliyeitwa ni Salva, kama Muhingo karudi tena, kwa hakika safari hii ni zamu yake, sasa usitake kumletea majungu, ili kukitia mchanga kitumbua chake.

  Binafsi namfahamu Muhingo, ni kichwa cha ukweli, japo anamtumikia fisadi papa, lakini viko vichwa vingi tuu kwenye payroll hiyo akiwamo Jacton, sambamba pia viko vichwa kibao kenye payroll ya nyangumi.

  Mode, imekuwa ni tabia, wakati wa kampeni ndio kipindi cha kuchafuana, nashauri zikija thread kama hii, mleta thread kama kama hana facts, fungilia mbali, unless ikae kwenye tetesi, na tena aulize swali kwa mwenye taarifa zaidi, vinginevyo itakuwa ni kuendekeza majungu.
   
 7. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #7
  Aug 26, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,683
  Likes Received: 171
  Trophy Points: 160
  Pasco, ninachokubaliana na wewe ni zile tuhuma zisizo na ushahidi kutupiliwa mbali kapuni. Maana zinashusha credibility yetu.

  Lakini hili la kuwa Mhingo na takataka zilizo kwa RA kuwa ni vichwa mimi nasema hapana. Ni vichwa wazi kabisaaaaaa. Maana vichwa visivyozaa matunda ya kuliwa bali vinazaa mitunda iliyojaa ukakasi si vichwa kabisa!

  Wakina mama wanakufa kwa kukosa huduma, wanalala juu ya vitanda vya ajabu ajabu kwenye vituo vya afya, hamna dawa wala huduma stahiki,Wazee pia wanadanganywa kuwa wanapewa huduma za afya bure kumbe uongo, shule zimekuwa ni story hata huwezi kusimulia, maji hayo ndio tena basi, Mkapa alipobuni ule mradi wa maji kwenda Shy basi kwingine wabaki kusikia majisifu ya jinsi sasa maji isivyokuwa shida tena, na hii mijitu inashabikia alafu unasema kuwa ni vichwa??????? Hapa napingana na wewe kabisaaaaa. Wala huwezi kunishawishi kwa vyovyote vile. Hawa ni vichwa wazi. Ni vilaza tu kama wengine. Elimu isiyo na manufaa ni sawa na elimu ya mtu ambaye hakwenda shule.
   
 8. Makanyaga

  Makanyaga JF-Expert Member

  #8
  Aug 26, 2010
  Joined: Sep 28, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Huyu anagombea au alikuwa mgombea jimbo gani ? Nimesoma kichwa cha habari tu nikashindwa kusoma maelezo yenu sababu najua fika kuwa sasa hivi ukishasikia mtu aidha anasemekana si raia au amefanya forgery ya whatever, ujue huyo alikuwa mgombea ubunge kupitia kura za maoni, na most likely kutoka chama kikubwa cha siasa!
   
 9. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #9
  Aug 26, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,408
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Hili hapa si suala la uraia, ni suala la kughushi jina. Kumbuka alighushi (doctored) picha ya Dr Salim in Mwananchi newspaper back in 2005! Mwizi hua haachi tabia kamwe!!!!
   
 10. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #10
  Aug 26, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 24,958
  Likes Received: 25,232
  Trophy Points: 280
  Pasco hapo katika red sikuelewi, Ni zamu yake kuwa nini katika utawala ujao? Kuwa Mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu? Nani wa kumpa?
   
 11. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #11
  Aug 26, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 36,391
  Likes Received: 7,943
  Trophy Points: 280
  Hold on, hold on, whoa, whoa, whoa

  Waandishi wa habari wamevaa jackets zimeandikwa nini ?

  Ati 'Kikwete Press 2010"

  Hivi jamani mnaona waandishi wa habari ambao wanawaandikia habari wananchi kutoka magazeti yanayojitegemea ni halali kuvaa majaketi yenye haya maneno ?

  Hivi hawa CCM wanataka kufanya mind control kwamba wanaown hii press?

  Idea nzima ya waandishi wa habari kuwa approved na Ikulu inanuka censorship na control.

  Wengine watasema idea nzima ya Ikulu ku control hizi attachment inanuka. Rais anatakiwa kuwa accessible na waandishi wa habari wote, watakaojilipia gharama zao wenyewe na hivyo kutohatarisha objectivity.

  Hizi habari za kuanza kupitishwa Ikulu na kuanza kulipiwa malazi na usafiri kutoka mfuko wa Ikulu zinaharibu objectivity ya waandishi wa habari.
   
 12. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #12
  Aug 26, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,490
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Kiranga,'
  Kumbe umeliona hilo? Kikwete Press 2010, yaani utadhani Kikwete ni World Cup vile unapata kitambulisho maalumu ku-cover the event.
   
 13. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #13
  Aug 26, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,683
  Likes Received: 171
  Trophy Points: 160
  Vilaza wa habari wako kazini. Wanadhalilishwa na kujidhalilisha wao wenyewe. Shida ni kupata bahasha hakuna kingine.

  Hii imewashusha hadhi ya uandishi wa Tanzania sana.

  Ndio sababu leo mtu akija na story ambayo ni investigative anaonekana wa ajabu ajabu vile kwa wenzie. Wengi utasoma habari zao zikinukuu " Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi wa mkoa maalum" huwezi kusikia story waliyoianzisha na kuileta ikiwa hot. Wanasubiri kila siku kuitwa kuwa kuna hili na lile pale makao makuu ya polisi au kuna hili na lile pale maelezo.

  Inaniboa sana nyie waandishi wa kibongo.
   
 14. M

  MWANASHERIA Member

  #14
  Aug 26, 2010
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  jamani mnyonge mnyongeni, ila haki yake mpeni, muhingo rweyemamu ni mwandishi mahili sana,ila tu system ndo ipo corupt, kama mkuu wake amesema mwondoe huyo unategemea nini?

  lakini pia suala la kuforge picha, mbona salim mwenyewe hakubisha kuhusu ile picha, japo ilimharibia salim lakini ni ukweli kua mdogo ni mwanajeshi wa yemen, na hilo je mnalionaje?

  kisheria muhingo was very wrong hata kama ametumwa, kumfukuza mwandishi wa habari kwenye mkutano wa kampeni.
   
 15. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #15
  Aug 26, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 36,391
  Likes Received: 7,943
  Trophy Points: 280
  Huu ndio ukondoo tusioutaka, mkuu akimwambia abong'oe atabong'oa ? Wapi principles ?

  Katika jamii inayotaka kuendelea, mtu anatakiwa kujiamini kwamba anaweza kubadili mfumo.

  Katika jamii isiyoweza kuendelea, mtu anaruhusiwa kutoa visingizio vyovyote na kusema viko nje ya uwezo wake. Ndiyo maana hatukomi kusingizia vitu, system, bosi, mvua, mungu, matatizo, shetani, wakoloni, maadui wa nje, etc.

  Ukiangalia kwa sana utaona ni ubinafsi na woga tu.
   
 16. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #16
  Aug 26, 2010
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 987
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  siamini kwamba ili uweze kutoa habari unahitaji kibali... yaani kwenda Geita au popote pale ni lazima upate kibali cha mwendesha kampeni, sijawahi kuona. au wanamaanisha kwamba wananyimwa posho/perdiem za kwendea kwenye kampeni za CCM.
  uhuru wa habari hakuna... na kama ukitumia perdiem ya CCM lazima utaandika habari kufurahisha CCM...
   
 17. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #17
  Aug 26, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,470
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Wanahabari wengi humu nchini ni malofa, hilo ndio tatizo.
   
 18. MawazoMatatu

  MawazoMatatu JF-Expert Member

  #18
  Aug 26, 2010
  Joined: Sep 6, 2008
  Messages: 505
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Umesahau ile barua ya Salva kwenda kwa fisadi Papa kuwa amemtosa baada ya kumfanikishia kununua Habari Cop ? Hiyo ndio ilikua chanzo nafkiri baada ya Salva kunusa kuwa angechaguliwa Muhingo badala yake nafkili this time watamchukua...kula kwa zamu.!
  Yaani mkuu hapa ndio sikuelewi yani unasupport ukanjanja? Mbona vichwa kama kina Jenerali hawana haja ya ku kiss a## na wanaendesha maisha yao kwa raha tu..! Ukiona hivyo jua sio kichwa
  Hili naafiki..!
   
 19. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #19
  Aug 26, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,834
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  ... simuungi mkono muhingo [ingawa one had to do that job anyway, na pia siwezi kumuita mahiri kama kazi yake anaifanya with evil deed]

  lakini nadhani Ogwalu needs to sort this one isije ikawa ni kamba style
   
 20. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #20
  Aug 26, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 133
  Nimesikia mpaka wa Tzdaima yumo humo kwa Kikwete hii vp?
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...