Rev. Mtikila ashida kesi ya kuruhusu mgombea binafsi Mahakama ya Afrika

ANC-KWA ZULU NATAL

JF-Expert Member
Jun 5, 2013
325
37
Arusha. Mwanasiasa mkongwe nchini Christopher Mtikila ameshinda kesi aliyofungua Mahakama ya Haki za Binadamu ya Afrika (AfCHPR) mjini Arusha akidai Tanzania inakiuka demokrasia inapozuia wagombea binafsi.

Katika hukumu iliyosomwa leo jioni, mahakama imesisitiza kuwa kwa kulazimisha viongozi watoke vyama vya siasa, Tanzania inawanyima wananchi wake fursa huru ya kushiriki kwenye uongozi.

Mchungaji Mtikila, ambaye ana historia ndefu ya kukwaruzana na serikali ya Chama Cha Mapinduzi, alifungua shauri mahakama ya Afrika mwaka 2011 baada ya jitihada zake za kupindua mabadiliko ya kikatiba yaliyofuta ugombea binafsi kugonga mwamba kwenye mahakama za kitaifa

Chanzo: Mwananchi
 
REV. CHRISTOPHER MTIKILA WINS THE CASE AGAINST THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

Arusha, 14 June 2013 - On Friday, 14 June 2013, the African Court on Human and Peoples' Rights ruled in favor of Reverend Christopher Mtikila against the United Republic of Tanzania, in the matter of Tanganyika Law Society and The Legal and Human Rights Centre and Reverend Christopher Mtikila v. The United Republic of Tanzania. The case concerned violation of basic political and civil rights, in particular Articles 2, 10 and 13 (1) of the African Charter on Human and Peoples' Rights, Articles 3, 22, 25 and 26 of the International Covenant on Civil and Political Rights and Articles 1, 7, 20 and 21 (1) of the Universal Declaration of Human Rights. In fact, the Applicants alleged that the Government of the United Republic of Tanzania had violated the democratic principles and the political rights of its citizens by enacting the Eighth Constitutional Amendment of 1992 and the Eleventh Constitutional Amendment Act No 34 of 1994 which prohibit independent candidates from standing for or contesting the Presidential, Parliamentary and Local Government elections, since the current Constitution provided that a candidate had to be a member of and/or be sponsored by a political party.

In its defense, the Respondent, the Government of Tanzania argued that the prohibition of independent candidates was a way of avoiding absolute and uncontrolled liberty, which would lead to anarchy and disorder; that the prohibition was necessary for good governance and unity. It sustained that the prohibition on independent candidates for positions of government leadership was necessary for national security, defense, public order, public peace and morality or to avoid tribalism. After examining both parties' submissions, the Court found that there is nothing in the Respondent's arguments to show that there are reasons for restrictions on the exercise of the right to participate freely in the government of the country. In any event, the restriction on the exercise of the right through the prohibition on independent candidacy is not proportionate to the alleged aim of fostering national unity and solidarity. The Court therefore found a violation of the right to participate freely in the government of one's country since for a Tanzanian individual to participate in Presidential, Parliamentary or Local Government elections in Tanzania, one must belong to a political party.

Tanzanians are thus prevented from freely participating in the government of their Country directly or through freely chosen representatives. The Court by majority ruled that the Government of the United Republic of Tanzania has violated Articles 2, 3, 10 and 13(1) of the Charter. Therefore, the Court directed the United Republic of Tanzania to take constitutional, legislative and all other necessary measures within a reasonable time to remedy the violations found by the Court and to inform the Court of the measures taken. With regards to compensation, the Court granted, in accordance with Rule 63 of the Rules of Court, leave to Reverend Christopher Mtikila to file submissions on his request for reparations within thirty (30) days hereof and the Respondent to reply thereto within thirty (30) days of the receipt of the 2nd Applicant's submissions.

Source :
Rev. Christopher Mtikila wins the Case against the United Republic of Tanzania
 
mbona mara ya mwisho majaji walimshauri asubiri kwanza mchakato wa katiba mpya ambayo waliamilio labda swala hilo lingekuwepo na ndivyo ilivyo kwenye rasimu hii.mi mi naona kesi hiyo imekuwa overtaken by event.
 
Ushindi kwa demokrasia na kanuni za siasa shirikishi kwa wote.
Ushindi kwa wanaojali kanuni za msingi za kikatiba.
Ushindi kwa wanaoamini katika masuala zaidi ya vyama.

This is a no brainer for anyone following the first principles embedded in our constitution.

Next stop, watu wote wanaoruhusiwa kupigia kura wagombea urais waruhusiwe kupata nafasi ya kugombea urais. Miaka ya kuweza kugombea urais ishushwe mpaka 18.
 
mbona mara ya mwisho majaji walimshauri asubiri kwanza mchakato wa katiba mpya ambayo waliamilio labda swala hilo lingekuwepo na ndivyo ilivyo kwenye rasimu hii.mi mi naona kesi hiyo imekuwa overtaken by event.
Kwa kuwa alikuwa amesha fungua kesi huko ilikuwa ni lazima ifike mwisho. Usisahau pia kuwa kuwepo kwenye draft ya katiba sio final. Kwenye mchakato swala la mgombea binafsi linaweza kupigwa chini kwa sababu linamwelekeo wa kuiathiri zaidi CCM endapo mmoja kati ya wale wanaoamini kuwa ni watu wa watu akipigwa chini kwenye mapendekezo ya mwisho lazima ataenda kugombea kama mgombea binafsi. Kwa kufanya hivyo ataondoka na wale wote wanaomshabikia
 
Suala la mgombea binafsi sio stori tena
sasa mtu kama una nia ya uongozi sio lazima ujikombe . Unawaachia wananchi waamue
 
Uhuru wa mgombea binafsi ulikuwa unaruhusiwa kwa tafsiri ya kisheria ya katiba ya sasa. Lakini kwa kuwa CCM siku zote inaendeshwa na ufedhuli wa kisiasa kwa kuangalia inaathirika vipi na kila uhuru uliopo kwenye katiba, waliweka kizuizi kingine ndani ya katiba kuminya uhuru huo.

Kwa vile CCM inapofika kwenye haki za raia ni dhulumati mkubwa, hukumu hii bado ni muhimu sana. Japo rasimu ya katiba inatoa mapendekezo ya kuwepo wagombea binafsi, bado CCM kutokana na kujengeka katika misingi ya dhuluma dhidi ya haki za Raia, inaweza kuipindua rasimu hiyo, na kugomea pendekezo hilo.

Nchi hii hakuna mzimu mbaya kuizidi CCM unapoongelea haki za raia. Ni afadhali iendelee kuoneshwa kila upande jinsi CCM na serikali yake vilivyojengeka kwa misingi ya dhuluma dhidi ya haki za raia.

mbona mara ya mwisho majaji walimshauri asubiri kwanza mchakato wa katiba mpya ambayo waliamilio labda swala hilo lingekuwepo na ndivyo ilivyo kwenye rasimu hii.mi mi naona kesi hiyo imekuwa overtaken by event.
 
mbona mara ya mwisho majaji walimshauri asubiri kwanza mchakato wa katiba mpya ambayo waliamilio labda swala hilo lingekuwepo na ndivyo ilivyo kwenye rasimu hii.mi mi naona kesi hiyo imekuwa overtaken by event.

Kwa kuwa shauri hili lilikuwepo toka mwaka 2011,

Na kwa kuwa mapendekezo yaliyopo kwenye Rasimu ya kwanza ya Katiba mpya si lazima yote yawepo kwenye Katiba kamili ya mwisho,

Na kwa kuwa viongozi wa CCM wameonyesha nia ya kujaribu kunyofoa mambo wasiyoyapenda kwenye rasimu hii ya kwanza, hasa yale yanayoleta haki kwa wananchi (mfano Wagombea binafsi na Serikali tatu yaani kuwepo pia Serikali ya Tanganyika),

Basi kuna haja kabisa ya kupongeza uamuzi huu wa Mahakama ya haki za binadamu ya Afrika, na pia kumpongeza Mch Mtikila kwa kulipigania jambo hili tokea mwaka 1995.
 
mbona mara ya mwisho majaji walimshauri asubiri kwanza mchakato wa katiba mpya ambayo waliamilio labda swala hilo lingekuwepo na ndivyo ilivyo kwenye rasimu hii.mi mi naona kesi hiyo imekuwa overtaken by event.
mheshimiwa rasimu ya katiba sio sheria!!
 
mbona mara ya mwisho majaji walimshauri asubiri kwanza mchakato wa katiba mpya ambayo waliamilio labda swala hilo lingekuwepo na ndivyo ilivyo kwenye rasimu hii.mi mi naona kesi hiyo imekuwa overtaken by event.

Pamoja na maelezo mengine yaliyokwisha kutolewa na wengine hapo juu kuhusu swala hili, ila napenda kuongeza pia kwamba- kwa "Mtikila" kutangazwa kuwa "Mshindi" dhidi ya "Serikali" ina maana "Serikali" itawanyibika kulipa "Gharama" zote za Kesi!! Pia swala la "Mgombea binafsi" sio tena "Swala la Mjadala", bali linapaswa "Ipso facto" kuingizwa kwenye "Katiba Mpya"!!!
 
'
.... .. the Respondent, the Government of Tanzania argued that the prohibition of independent candidates was a way of avoiding absolute and uncontrolled liberty, which would lead to anarchy and disorder......

Anarchy and disordert is brought by the sitting president and his henchmen.
 
Usisahau kuwa ile ni rasimu siyo katiba kamili. Inaweza kukataliwa. Dawa ya haya yote ni kwenda mahakamani tu si vinginevyo. Mtikila alikuwa sahihi kabisa. Yeye ndiye kai overtake rasimu ya katiba mpya.
 
Kumbukumbu zangu zinaonyesha kuwa mahakama za Tanzania zilishatoa hukumu ya mgombea binafsi. Na hukumu hii ilikuwa binding.

Je, nipo sahihi kutokana na hizo kumbukumbu au nilipitwa na kitu?

Je, hukumu gani ni lazima serikali izitekeleze? (Mfano hatujawahi kusikia mfungwa kahukumiwa kisha serikali kumkalia kimya kama vile hakuhukumiwa.).

Kwenye kesi hii maarufu, ni upi msimamo wa kisheria? Serikali ipo in jeopardy of the law au ni mimi tu sielewi?

Nawasilisha na naomba mwenye maelezo anielimishe.
 
Back
Top Bottom