Retirement & Tanzania: Tatizo Ni Nini Hasa?

Apr 27, 2006
26,588
10,375
- Wakuu heshima mbele sana, Tanzania ni muda mrefu sasa tumekuwa tukihangaika sana na hii ishu ya mapumziko baada ya utumishi wa siasa na serikali yetu, hii ishu imekuwa mwiba mbaya sana kwetu kitaifa inapofika wakati wa kupumzika wahusika watajaribu kila mbinu kuizunguka hii ishu ili waendelee tu in some capacity.

- Wananchi tumekwua very critical bila kujali circumstances na facts surrounding the ishu, now I am not an apologist wa wakwepaji kupumzika, lakiini je ni kweli tunayo mazingara ya kuridhisha kwa mapumziko kwa wastaafu wetu? Kwa mfano hivi karibuni Rais Kaunda, alisajiliwa na kufundisha shule moja kule Boston kwa miaka miwili, I mean malipo yalikua very poa hata mtumzima hakujali kushika chaki, pia heshima nayo ilikuwa kubwa sana, ninakumbuka sana Waheshimiwa Al-noor Kassum na Mwandosya, walipoamua kwenda kushika chaki jinsi viongozi wengine walivyokuwa wakiwashangaa badala ya kuwaheshimu.

- Now who is at fault watumishi wetu wasiotaka kutoka au taifa wka kushindwa kuwatayarishia mazingira bora ya kutaka ku-retire sio mapema tu, bali hata wakati ukifika? I mean somebody is at fault na siamini kwamba ni watumishi! maana wenzetu Libya hawana haya matatizo, serikali yao ina Social Security nzuri na pia kuna retirement homes, na pia nursing home kwa ajili ya wazee as the results sio rahisi hata kuwakuta wa-Libya majuu wakibangaiza, huwa wanabaki kwao tu!

Respect.

FMEs!
 
Great Topic!

Katika wizara zote, haki ya nani tena usiombee uwe na ndugu awe amefikisha umri wa ku-retire kwenye Wizara ya Elimu! Ma-file yanapotezwa na kupatikana baada ya mwaka au kutokupatikana kabisa. Ofisa Utumishi wa wizara kwa kifupi ni mtu asiyefata maadili ya kazi yake. :(
 
Mkuu FMES, pongezi zangu nyingi sana kwa kuanzisha mjadala huu, umeniwahi tu Mkuu nilikuwa nafikiria kuuanzisha. Kuna baadhi ya nchi sasa hivi retirement ni uamuzi wa mwajiriwa baada ya kuonekana kwamba Wafanyakazi wengi huwa bado wana afya njema na utaalamu wao adimu kuhitajika katika nyanja mbali mbali za uchumi. Kinachonishangaza pamoja na kutokuwa na umri maalum wa retirement bado wafanyakazi wengi wana retire wakiwa na nguvu zao na wachache huamua kuendelea kwa kudai maisha ya kutokuwa na cha kufanya ni very boring na yanaweza kabisa kuchangia kufa kwao mapema.

Kwa Tanzania pia nadhani bado kuna nyanja ambazo tuna upungufu mkubwa wa Wataalamu kama Wahandisi, Madaktari, Wahasibu n.k. ambao labda upendeleo maalum ungefanywa ili kwenye zile fani ambazo tunahitaji wataalamu na kuna upungufu mkubwa basi waendelee kufanya kazi hata baada ya kufikisha retirement age. Tunaweza pia kuliingiza sakata la Prof Baregu ambaye wahadhiri wengi pale UDSM walimtetea kwamba bado anahitajika lakini CCM kutokana na mambo ya kisiasa wakaamua kumnyima makusudi mkataba mwingine kwa kisingizio kwamba Serikali hailazimiki kumpa mkataba mfanyakazi ambaye ameshafikisha umri wa kuretire.

Je, kwenye zile nyanja ambazo nimezitaja hapo juu na nyinginezo ambazo kuna upungufu mkubwa wa Wataalam kuna haja ya kuwekwa upendeleo maalum ili watu hawa waendelee kuajiriwa hata baada ya kufikisha umri huo provided kwamba afya yao inawaruhusu kufanya hivyo au sheria iwe ni msumeno bila kujali upungufu mkubwa wa Wataalam tulionao katika baadhi ya fani!?
 
Kwa mishahara ambayo watumishi wa serikali hulipwa, walah kustaafu hakuna maslahi yeyote kwa mtumishi wa umma kustaafu mapema (hata kwa umri), na ndio maana wengi wao huingia kwenye ajira za kuganga njaa ambazo mwisho wake huwa si wa heshima.

Kitu cha muhimu ni kwa serikali kuzalisha ajira za kutosha, ili vijana wachanga wawe na nafasi ya kufanya kazi na kuitumikia nchi yao, na wale walio staafu waweze kuendelea na kazi japo kwa nusu muongo. Vinginevyo, tutapoteza watu wenye teknolojia ya juu kwani kwa kipindi ambacho watu hutakiwa kustaafu ndipo kipindi wanachohitajika sana kutokana na ujuzi na uzoefu wao wa muda mrefu kuhitajika na jamii, na hapo hujikuta wakishindania kazi na vijana wachanga.
 
retirement haipaswi kuwa jukumu la serikali
serikali inatakiwa iweke mfumo mzuri wa pension ambapo utamuezesha mstaafu kuishi kwa kutumia pensio yake

mtu anapo staafu yeye ndio anatakiwa aamue nini cha kufanya na sio serikali, watu wengi wakistaafu unakuta wanataka kufanya vitu tofauti na vile walivyokuwa wanavifanya au kufanya vitu kama vile walivyokuwa wanavifanya kwa charity

kuhusu kaunda alienda kufundisha huko boston ili kukimbia kesi zilizokuwa zinamkabili, anapesa ya kutosha watoto wake waliyoiba kwenye migodi. angekuwa anafundisha university zambia ningemuuona patriotic.

kwa ajili mambo ya kustaafu bado ni machanga TZ unakuta watu wengi bado hawajajiaanda kuustaafu, usisahau hichi ni kizazi cha kwanza kustaafu
 
Hapa hapa kwenye hili jukwaa mlikuwa mnasema wazee/vikongwe waendelee kugombea kwenye siasa then mnabadilika mnasema wawekewe mazingara mazuri unafiki mtupu. Kuna walio na mazingara mazuri kuwapita mawaziri wakuu wa zamani au mafao wanayopata wabunge baada ya miaka mitano?

Lets be serious na sio kuwamba ngozi. Wabunge wanalipwa 46 million baada ya 5 yrs approx £23,000.00 kwa kazi ya kusinzia bungeni bila kujali maslahi ya walipa kodi.
 
Kama ni social security iwe kwa watz wote, hadi yule babu wa kule kijijini. Itakuwa ni kukosa shukrani kufikiria wafanyakazi tu. Kila mtu amechangia ktk mapato ya nchi kwa namna moja au nyingine. Wanasiasa na sisi wafanyakazi tuna kawaida ya kujisahau as if keki ya taifa ni yetu sisi wenyewe tu... this is wrong and immoral
 
retirement haipaswi kuwa jukumu la serikali
serikali inatakiwa iweke mfumo mzuri wa pension ambapo utamuezesha mstaafu kuishi kwa kutumia pensio yake

mtu anapo staafu yeye ndio anatakiwa aamue nini cha kufanya na sio serikali, watu wengi wakistaafu unakuta wanataka kufanya vitu tofauti na vile walivyokuwa wanavifanya au kufanya vitu kama vile walivyokuwa wanavifanya kwa charity

kuhusu kaunda alienda kufundisha huko boston ili kukimbia kesi zilizokuwa zinamkabili, anapesa ya kutosha watoto wake waliyoiba kwenye migodi. angekuwa anafundisha university zambia ningemuuona patriotic.

kwa ajili mambo ya kustaafu bado ni machanga TZ unakuta watu wengi bado hawajajiaanda kuustaafu, usisahau hichi ni kizazi cha kwanza kustaafu
Unajua kuna baadhi ya kazi ambazo ukizifanya unapoenda mtaani, huwezi kufungua kaofisi kako ukasema unaendeleza kazi ile ile.Hata hivyo naona tunakosa mipangilio mizuri au tunafanya makusudi ili kusiwepo succession plan nzuri kwenye kazi za umma ndio maana watu wanaweka mazingira ya kudumu kufanya kazi amnazo mara nyingine hata hawana uwezo wa kuzimudu kutokana na changes zinazoendelea hapa na pale.
 
- Nilianzisha hii topic kwa kutegemea solutions, sasa huwezi pata solution kabla ya kukubali kwamba tuna tatizo, yes tunalo tatizo sasa tunaweza kuendelea kurusha rusha maneno yasiyo na tija kwa taifa, au kukubali na kutafuta solutions,

- Binafsi ninaishi karibu sana na Mzee mmoja aliyewahi kuwa Katibu wa Mwalimu, huyu hakuwa mwizi wala fisadi, amejaribu sana kuishi on pension lakini it too little kwamba it is a big joke, sasa wale wanaomfuata kwenye position yake si wanamuona anavyohangaika, mawili either wawe mafisadi au walilie kutoondoka kwenye power!

- System ya Social Security inatengenezwa na walipa kodi, ambao wanachangia kidogo kidogo hela zao zinazokatwa kwenye mishara yao na kuwa-invested kwenye Financial Instituions ili kuongezeka, ni vigumu sana kumsaidia through this sytem mwananchi ambaye hajachangia anything, kwa hiyo walipa kodi ndio lazima wafikiriwe kwanza!

- Taifa letu lazima lianze sasa kujadili haya ya retirement as a national ishu, one time nilienda kule Hazina kufuatilia pension ya ndugu yangu aliyefariki akiwa serikalini, yaani sina hamu na niliyoyaona kule, hasa jinsi mafaili yalivyokuwa "Yamehifadhiwa" it was a very serious joke, ilichukua kama two months kuweza kufikia lilipokuwa hilo faili. Inasikitisha sana!

Respect.

FMEs!
 
Mkuu we should think of working first before we retire. Kama decision makers wanaona kuwa they can make themeselves good retiring environment by embezzling, they will not care about others. Mzee Apio alikula kuku sana na kubadilisha vimwana sana alipokuwa utumishi kutokana na hela za kifisadi, lakini alipotoka kwenye kiti kilichokuwa kinampa hizo njia alikuwa malamikaji mkubwa sana wa sera alizotetea kwa nguvu alipokuw kwenye kiti. Hii issue sio mpya, imeongelewa sana, lakini huwezi kuingea kwa watu ambao ofisi ni opportunity ya kuiba, hawawezi kujali kabisa.
Let us get other things going first, watu wapate ajira nzuri na wafanaye kazi kweli, mishahara ya maana, tukiwa na income ya kutosha, na kufanya uwekezaji wa kutosha kwenye social welfare tutafika huko. Sasa hivi hata uwekezaji kwenye social welfare ni almost sifuri, kutokana na kwengine ambako pesa za kuwekeza huko zinatakiwa kutoka kuwa ovyo.
 
- Wakuu heshima mbele sana, Tanzania ni muda mrefu sasa tumekuwa tukihangaika sana na hii ishu ya mapumziko baada ya utumishi wa siasa na serikali yetu, hii ishu imekuwa mwiba mbaya sana kwetu kitaifa inapofika wakati wa kupumzika wahusika watajaribu kila mbinu kuizunguka hii ishu ili waendelee tu in some capacity.

- Wananchi tumekwua very critical bila kujali circumstances na facts surrounding the ishu, now I am not an apologist wa wakwepaji kupumzika, lakiini je ni kweli tunayo mazingara ya kuridhisha kwa mapumziko kwa wastaafu wetu? Kwa mfano hivi karibuni Rais Kaunda, alisajiliwa na kufundisha shule moja kule Boston kwa miaka miwili, I mean malipo yalikua very poa hata mtumzima hakujali kushika chaki, pia heshima nayo ilikuwa kubwa sana, ninakumbuka sana Waheshimiwa Al-noor Kassum na Mwandosya, walipoamua kwenda kushika chaki jinsi viongozi wengine walivyokuwa wakiwashangaa badala ya kuwaheshimu.

- Now who is at fault watumishi wetu wasiotaka kutoka au taifa wka kushindwa kuwatayarishia mazingira bora ya kutaka ku-retire sio mapema tu, bali hata wakati ukifika? I mean somebody is at fault na siamini kwamba ni watumishi! maana wenzetu Libya hawana haya matatizo, serikali yao ina Social Security nzuri na pia kuna retirement homes, na pia nursing home kwa ajili ya wazee as the results sio rahisi hata kuwakuta wa-Libya majuu wakibangaiza, huwa wanabaki kwao tu!

Respect.

FMEs!

Mkuu system ina matatizo ila nataka kuzungumzia kitu kimoja maana nataka kupingana na wewe kidogo. Ulisema hutaki kuwa laumu watumishi. Nakubali siyo watumishi wote wapo at fault lakini baadhi wana makosa na hii naongelea from personal experience ya watu nilio waona.

Unakuta mkuu mtu alikua balozi kwa miaka mingi au alikua serikalini na nafasi nzuri lakini ana staafu bila chochote. At the same time unakuta mtu aliye kuwa na cheo kidogo au cha kati ana staafu na kabanda kake na viji miradi vywa kuweza kumsogeza siku za uzeeni. Do you get my point hapo?

I think pamoja na kwamba the system is at fault lakini pia watumishi wengi hawana utamaduni mzuri wa kuweka akiba na kujiandaa kwa ajili ya kustaafu. Mtu akipata vijisenti kidogo tu ana tumbua utafikiri huko mbeleni ataendelea kupata kipato hicho hicho.

So sikubaliani na kuwaondoa kabisa watumishi wenyewe as part of the problem japo si wote.
 
Back
Top Bottom