Results processing template (Ms Excel) - Primary schools Tsh 10,000/=

Njuka II

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2019
Messages
201
Points
250

Njuka II

JF-Expert Member
Joined Feb 25, 2019
201 250
Natumaini kuwa sote ni wazima wa afya
Bila kupoteza muda, niende moja kwa moja kwenye mada. Mimi ni mtaalamu wa Microsoft Excel, Leo nimekuja na template ambayo kazi yake ni kuchakata matokeo ya wanafunzi wa shule ya msingi.

Hii template ina uwezo wa kuchukua wanafunzi 400 na ina worksheets tatu, kila worksheet ina kazi yake, nitazielezea moja moja.

1. Worksheet 1 (setting)

Hii ni worksheet ambayo mwalimu atakuwa anafanya setting za madaraja (grades).

Pia katika hii worksheet kuna sehemu mwalimu ataset alama ya ufaulu (pass mark) ambayo itakuwa inalinganishwa na wastani alioupata mwanafunzi, nitaielezea vizuri dhumuni la kuweka hii passmark katika worksheet inayofuata.

2. Worksheet 2 ( Score sheet )

Hii ni worksheet ambayo mwalimu atakuwa anajaza majina pamoja na alama (marks) za wanafunzi wake.

Mwalimu atajaza alama tu, grades zitajijaza zenyewe kulingana na setting ulizofanya kwenye worksheet 1.
Pia mwalimu atajaza jina la shule yake , tarehe, na darasa (Haya maelezo yatatumika katika worksheet zingine).

Worksheet hii itamsaidia mwalimu kuwajua wanafunzi waliofaulu (Pass), wanafunzi waliofeli (Fail), wanafunzi ambayo wamefanya mitihani nusu au kutofanya kabisa (Incomplete).

Wanafunzi wote ambao watakuwa wamevuka alama ya ufaulu (pass mark) ambayo uliijaza kwenye setting watakuwa na highlight nyeupe, wanafunzi ambao watakuwa hawajafikisha alama ya ufaulu watakuwa na highlight ya kijivu(grey), wanafunzi ambao watakuwa wamefanya mitihani ambayo idadi yake haifiki tano au kutofanya kabisa watakuwa na highlight ya blue bahari.
NB: Nimeweka key za highlights zote hapo juu (Angalia picha ya score sheet nitakayoweka hapo chini)

3. Worksheet 3 (Student's Report)

Hii ni worksheet ambayo kazi yake ni kutengeneza report za wanafunzi wote ambao mwalimu aliwaandika kwenye sheet ya kurekodi marks (score sheet).

Inaonesha nafasi (position) kwa kila mwanafunzi utakayemchagua kwenye list (drop down list, ambayo itadisplay pale utakaposelect cell yenye jina la mwanafunzi)
Worksheet hii mwalimu haruhusiwi kuandika chochote zaidi ya kuchagua jina la mwanafunzi tu, cells zote zilizopo kwenye hii worksheet zinajijaza zenyewe na pia nimezilock ili kulinda formula nilizoziandika.

Bei ya hii template ni Tsh 10,000/= na hakuna malipo za ziada, utaitumia hii template katika Maisha yako yote.

Njuka II
Expert in Microsoft Excel
Email: ebusiness.excel@gmail.com
Dar es salaam,
Friday 13-09-2019


Let's see together the power of Microsoft Excel.
 

Njuka II

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2019
Messages
201
Points
250

Njuka II

JF-Expert Member
Joined Feb 25, 2019
201 250
Ukiwa na hii template utaweza kuprint report zaidi ya 150 ndani ya lisaa limoja. Hakuna haja ya kufanya page setup, zote nimeshaziset hivyo utachagua jina la mwanafunzi unayetaka kuona /kuprint report yake kisha utabonyeza Ctrl+P kupata report husika
 

Mamtolo

Senior Member
Joined
Feb 27, 2018
Messages
122
Points
250

Mamtolo

Senior Member
Joined Feb 27, 2018
122 250
Ukiwa na hii template utaweza kuprint report zaidi ya 150 ndani ya lisaa limoja. Hakuna haja ya kufanya page setup, zote nimeshaziset hivyo utachagua jina la mwanafunzi unayetaka kuona /kuprint report yake kisha utabonyeza Ctrl+P kupata report husika
Huna template ya sekondari mkuu
 

Njuka II

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2019
Messages
201
Points
250

Njuka II

JF-Expert Member
Joined Feb 25, 2019
201 250
Huna template ya sekondari mkuu
Template ya O- level hii hapa

 

Njuka II

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2019
Messages
201
Points
250

Njuka II

JF-Expert Member
Joined Feb 25, 2019
201 250
Ktk templates zangu huwezi kukutana na changamoto ya kuharibika kwa file kutokana na bahati mbaya ya kuandika kitu kwenye cell zenye formula. Cells zote ambazo zina formula huwa nazilock, hivyo mtu hawezi kuharibu/kufuta formula iwe ni bahati mbaya au makusudi. Mtumiaji wa template ataweza kuandika sehemu ambazo anatakiwa kuandikwa
 

66KV

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2014
Messages
247
Points
250

66KV

JF-Expert Member
Joined May 16, 2014
247 250
Ktk templates zangu huwezi kukutana na changamoto ya kuharibika kwa file kutokana na bahati mbaya ya kuandika kitu kwenye cell zenye formula. Cells zote ambazo zina formula huwa nazilock, hivyo mtu hawezi kuharibu/kufuta formula iwe ni bahati mbaya au makusudi. Mtumiaji wa template ataweza kuandika sehemu ambazo anatakiwa kuandikwa
Unaendesha mafunzo ya excel pia?
 

Forum statistics

Threads 1,343,414
Members 515,033
Posts 32,783,933
Top