Restructuring - Jiji la Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Restructuring - Jiji la Dar

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Quemu, Jan 5, 2009.

 1. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2009
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Kama kuna maeneo mawili muhimu ambayo yanaweza kubadilisha mji wa Dar Es Salaam kwa kuleta ladha mpya ya ‘jiji la kisasa’ basi ni maeneo yaliyopo base za majeshi yetu. Ninazungumzia maeneo ya Mgulani na Lugalo.

  Inawezekana wakati blueprint (ramani) ya jiji Dar ilipokuwa drafted, wataalam hawakufikiria kuwa jiji hili linaweza kukuwa zaidi ya mipaka waliyoweka. Au pengine walifikiria hivyo na wakaandaa ‘expandable blueprint’, lakini watawala wetu wakapuuzia au wakakosa means za kui-implement. Vyovyote vile, kutokana na ukuajia wa jiji la Dar, maeneo haya mawili ya jeshi yamemezwa na kuwa ndani ya jiji kabisa.

  Kutokana na hali hii, kuna haja kubwa ya kufanya mpango wa kuyaamisha majeshi yetu kutoka maeneo haya na kuyasogeza nje ya mji. Sababu za kufanya hivyo zinaweza kuwa ziko nyingi, lakini pengine mbili muhimu ni:

  1) Suala la security na privacy za Jeshi kwa ujumla
  2) Suala la majeshi hayo kumiliki maeneo makubwa ndani ya jiji.

  Ningependa kutogusa sababu ya kwanza (sio dhumuni la mada hii). Uvutio wangu huko kwenye sababu ya pili.

  *****************************************************************************************
  Ni maeneo gani haswa nizungumziayo?

  Eneo la jeshi lililopo Mgulani – eneo jeshi hili limeanzia mara tu baada ya kumaliza zile flats kumi zilizopo Keko Bora (zile flats zilizoanzia pale kwenye kona ya kiwanda kilichokuwa cha visu - Tameko), limekwenda mpaka maeneo ya shule ya msingi Mgulani, likaelekea mpaka kwenye junction ya barabara za Sabasaba na Kawawa, na mpaka maeneo ya Uwanja wa Taifa.

  Eneo la jeshi lililopo Lugalo – eneo hili linaanzia mara tu baada ya junction ya barabara za Bagamoyo na barabara ya kwenda Ubungo (Mandela Road?), limekwenda mpaka maeneo ya Kawe, na mpaka Makongo Juu.

  *Maeneo haya niyo orodhesha ni kwa tathmini ya harakaharaka. Kwa hiyo kunaweza kuwa na + or - ya maeneo.
  ******************************************************************************************

  Sasa basi kama tukifanikiwa kuhamisha majeshi haya, basi tunaweza kutanua na kulipendezesha jiji la Dar na kulipa ladha mpya kabisa ya jiji la kisasa.

  Mfano, tukiangalia eneo la Lugalo. Eneo hili, ukijumlisha na maeneo ya Chuo Kikuu, Changanyikeni, na upande wa pili wa Kawe (Tanganyika Packers area) linaweza kabisa kuhamisha focus ya jiji kutoka City Center. Pale panaweza kutengenezwa infrastructure ya nguvu, ambayo itajumuisha office buildings, residential condominiums/apartments, shopping centers, na parks. Yes, panatosha kuweka vitu vyote hivyo na zaidi.

  Sasa tukifanya hivyo hivyo kwa eneo la Mgulani, basi tutazungumzia mengine kabisa kuhusu Dar. Bila ya shaka itatubidi tuweke ‘The New” kabla ya jina "Dar Es Salaam."
   
  Last edited by a moderator: Jan 6, 2009
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Jan 5, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Babu naona umeamua ku share ndoto ya jana usiku nini?..lol
   
 3. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2009
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  LOL....ndoto ndizo zenyewe!!

  Lakini kusema ukweli haya maeneo mawili tungeweza kuyatumia kubadilisha mji wa Dar. Hivi umeshawahi kupanda kule Makongo Juu, halafu ukapata view mzima ya eneo hili? Yaani kumejaa mapori na vijijumba vilivyochoka walivyotuachia mkoloni. Tunaweza kufanya makubwa sana kama jeshi litakuwa tayari kuyaachia haya maeneo mawili.
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Jan 5, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Mazee Makongo Juu anga zangu hizo. Ni kweli kuna vipori na vijumba vilivyochoka lakini pia kuna mansion za nguvu. Najua Daniel Yona ana jumba huko na vingunge wengine mafisadi. Ila tatizo la hiyo sehemu ni maji ya bomba. Kwa vile kuko juu pressure wakati mwingine ni ndogo sana. Oh well, na matatizo mengine kibao....
   
 5. v

  vassil Senior Member

  #5
  Jan 6, 2009
  Joined: Apr 13, 2008
  Messages: 121
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  mawazo mazuri kabisa ila nji hii mawaz mazuri hayana nafasi ya kutosha
   
 6. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #6
  Jan 6, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Had same thoughts about Lugalo, lkini mzee si umeona jmaa wanajenga tena flats mpya kama kumi hivi. That means they are no close to what others are thinking over that area.
   
 7. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #7
  Jan 6, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Inawezaka kuna vitu vingi sana vimejengwa/wekwa underground katika maeneo haya! Hii inaweza kufanya wazo la kuwahamisha kuwa ndoto na pia kuyatumia maeneo hayo kwa shughuli za kiraia kuwa si salama.
   
 8. W

  Waleed Waleed Member

  #8
  Jan 6, 2009
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante kwa kuwa muona\mtaka maendeleo.

  Nakubaliana na mawazo yako kwa 100%; pamoja na wachangiaji wengine.

  Tatizo la viongozi wengi wa nchi hii ni kutokuwa na UWEZO wa ubunifu hata kwa mambo ambayo siyo very much technical; wengi wao wanajua kujaza matumbo yao tu; na ni kwa leo tu wala si kesho.

  Ukiangalia mji wa DSM unahitaji reengineering of her masterplan, kwani hakuna maeneo muhimu yanayo upa mji hadhi pamoja na sifa ya kupendwa na wenyeji na wageni.

  Tazama Fukwe zetu almost zote ziko hovyo. Kilio changu ni eneo la COCO BEACH, hili ni kama limesahaulika kabisaaa.

  Hata watoto wangu hukataa kuenda eneo hilo kwa uchafu ulipo. Maeneo ya namna hiyo kwenye nchi za wenzetu ni yakuvutia kupita kiasi; kwani hutengenezwa na kuwezesha watu kupata burudani na starehe za aina tofauti tofauti, vile vile huiingizia serikali mapata ya makubwa.

  hubu tupige kelele wote kwa pamoja hawa City Fathers WAAMKE ili mji huu uwe wa kuvutia; usiwe kama alivyo KUKU; kuamka asubuhi na kukimbizana na panzi kabla ya kurudi bandani inapotimu magharibi
   
 9. T

  TAZARA CLUB Member

  #9
  Jan 6, 2009
  Joined: Feb 6, 2007
  Messages: 45
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 15
  QM sawa kwa mawazo yako yakuona kuwa kambi zetu ziko ndani ya makazi ya watu wengi, lakini hiyo sio sababu, kwani nilipita pale WINSOR BARKSHIRE IN UK jirani kabisa na WINSOR CASSTLE LILEjumba la kifalme na ngome ya empire ya waingereza nilishangaa kuona kambi kubwa ya jeshi iko katikati ya mji huo ambao unavutia watalii toka sehemu mbalimbali duniani, yaani hiyo kambi ya KING GEORGE II NI KUBWA SANA wala huwezi pima na hizi zetu za Lugalo na Mgulani lakini mbona wenzetu hawana wazo la kuzihamisha, cha msingi ni kujenga ukuta kuzunguka eneo hilo la jeshi ili liwe ndani ya ngome pia kuondoa uwezekano kabisa wa ile barabara ya bagamoyo kupita katikati ya Lugalo na kuamua itumike old bagamoyo road hadi kawe mwisho then hadi junction ya kuingia tanki bovu, gharama ya kuhamisha kambi hizo ni kubwa sana ni afadhali hili wazo langu. suala la new Dar kuna maeneo mengi tu ya kuhamishiwa mji huko kama vile mbweni ,boko, kigamboni hadi gezaurore, chanika, chamanzi, kisarawe, etc ni plan tu halafu itekelezwe
   
 10. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #10
  Jan 6, 2009
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Hizo flats wanaweza kuzifanya kuwa mradi. Kama wakihama wanaweza kuzikodisha kwa raia. Kwa hiyo unaweza kuwa mradi wa jeshi uraiani.

  Lakini mbona tayari kuna raia wengi tu wana-hang maeneo hayo? Baadhi ya sehemu ya Kawe, wameruhusu raia waishi. Isitoshe kuna shule ndani ya jeshi ambazo wanafunzi wake wengi wanatoka uraiani.

  Sasa kama kuna mapandikizo ardhini mwao (sisemi kama hayapo), si wanahatarisha usalama wa raia waliozagaa maeneo hayo? Au?
   
 11. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #11
  Jan 6, 2009
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Tazara Club,

  Nikikunukuu:

  Hivi umeshawahi kupita maeneo ya jeshi ya Mgulani na Lugalo siku za usoni? Je unafikiri kwa jinsi yalivyo sasa yanaweza kuwa vivutio vya watalii?

  La hasha! Jeshi letu limeshindwa kuyaendeleza maeneo hayo. Ukipita upande wa maeneo ya shule ya msingi ya Mgulani, kuna vijijumba vidogo vidogo vilivyochoka tulivyoachiwa na mkoloni (humu ndimo wanakaa kuruta). Jinsi vilivyochoka, unaweza hata kuvisukuma kwa mkono mmoja na vikadondoka. Vivyo hivyo, vijumba hivyo vipo lugalo. Tena Lugalo kuna mpaka mapori pia.

  Hivyo basi, hakuna shaka, jeshi limeshindwa au halina nia ya kuendeleza maeneo hayo.

  Tatizo ni kwamba wameshindwa kuendeleza eneo lao. Ile ardhi pale imebaki kuwa kama "raslimali iliyokaliwa na majuha wa uzalishaji." Kwa hiyo hata kama waweke ukuta au kuhamisha barabara, ishu itabaki pale pale......

  Labda pengine, badala ya kuhamisha jeshi zima, wanaweza kupunguza eneo lao na kubakia sehemu ndogo tu. Size ya eneo la kama pale Mlalakuwa au Upanga ingewatosha. Yaani, wangeweza kumiliki eneo dogo tu kwa ajili ya mambo ya administrative. Lakini mazagazaga mengine yote wangeyasogeza nje ya mji.

  Tena unajua, sio lazima jeshi wayaachie yale maeneo completely. Wangendelea kuyamiliki tu, halafu wakayaazimisha kwa private sectors. Halafu jeshi kwa kushirikiana na serikali wangefanya usimamizi wa uendelezaji na mazingira katika maeneo hayo.

  Kwani si jeshi limejiingiza kwenye biashara mbalimbali - wamejenga kumbi kibao ndani ya ngome zao kwa ajili ya shughuli za harusi na mikutano. Isitioshe wanataka kujiingiza kwenye biashara za ulinzi huko maofisini na majumbani. Sasa kwa nini wasijiingize kwenye biashara ya land leasing, land development na real estate pia???

  Ni kweli.

  Lakini kwa mtazamo wangu, ukiondoa Kigamboni, sehemu nyingi ulizozitaja zinafaa kuwa sehemu za makazi, badala ya sehemu za ofisi, biashara, na vivutio.

  Lugalo na Mgulani ni sehemu ambazo zinaweza ku-shift focus ya city center kwa kiasi kikubwa. Zinaweza kabisa kufanya Dar ionekane kama ina city center tatu, na kufanya jiji zima lionekane kubwa zaidi. Ni kama vile unapotundika mirror dining room . Ile reflection ya lights za chandelier inafanya dining na living room zionekane kubwa zaidi. Kwa hiyo, Lugalo na Mgulani zinaweza kabisa kuwa reflection ya Dar Chandelier (downtown Dar).
   
 12. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #12
  Jan 6, 2009
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,274
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Nafikiri si lazima wahame(kunaweza kuwa na ugumu) ila wanaweza
  1. Kutoa baadhi ya maeneo kwa jiji hasa yale ambayo hayajaendelezwa.
  2. Kuruhusu barabara zipite katika maeneo yao mf. Changanyikeni/Makongo juu kuwepo na njia ya kutokea Kawe/Kunduchi/Tegeta nk.
  3. Kuboresha maeneo yao yawe yanavutia
   
Loading...