Respect Wakuu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Respect Wakuu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, Feb 24, 2008.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Feb 24, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Wapendwa,

  Ni siku mpya, siku ya furaha. Hakuna haja ya kuwa na majonzi wala kulaumiana kwa yalioshindwa kufanyika kuzuia sekeseke.

  Tumejifunza kutokana na makosa. Naamini umoja na mshikamano wetu utaimarika na kujijenga upya kwa Ari, Nguvu na Kasi mpya!

  Tufurahie ushindi dhidi ya udhalimu wa kufumba midomo ya watu, Taifa, Wazalendo na Demokrasia.

  Poleni nyote kwa kuishi matumbo joto na hata kwa wasiwasi. Tukeshe tukiomba, yamepita nasi tumepewa siku njema ambayo ni mpya na tuamke tukiwa madhubuti. Jitihada zetu na maarifa ndiko kulikotunusuru.

  Naomba nitumie vile vipengele vinne vya Azimio kutamka rasmi, sisi ni Wazalendo, tuna watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora.

  Sisi kama wana JF tunajisifu kwa kuwa na hivyo vitu ambavyo serikali yetu inaona aibu kukiri imevizembea.

  Nasi tukaribishe wote washiriki nasi hapa kundini, walio nasi na hata maadui, tuwakaribishe tuendelee kulijenga Taifa na kujadiliana hoja. We dare to talk openly, we shall over come, onward JF Soldiers! "kumkoma Nyani Giladi"

  Respect Wakuu!
   
 2. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #2
  Feb 24, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Asante Kishoka,

  Taifa letu litakombolewa na sisi wenyewe na ni vyema kuwa JF itakuwepo hapa kusaidia ukombozi wa mamilioni ya watanzania toka kwenye makucha ya mafisadi wasio na huruma.

  Thanks!
   
 3. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #3
  Feb 28, 2008
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Ni maneno makubwa haya.

  Umefika wakati hata kama hali ni ngumu kiasi gani tuje kwenye ugunduzi huu! Kwamba tutajikomboa kupitia sisi wenyewe. Gharama zake ni kumwagika kwa jasho. Jasho litamwagika maana sasa nani alimwage kwa niaba? Hatumuoni! Na hata hawa tuliowachagua ndio kabisa siasa zao sio safi, uongozi sio bora, ardhi na rasilimali zake imekabidhiwa wageni.... hata nuru na mwelekeo hatuoni.

  Jasho letu wenyewe tulimwage, bali kwa juhudi sahihi, maarifa kamili maana hivi hivi mbele hapasogeleki. Vishindo ni vizito..!Ukisikiliza milio ya silaha ya upande wa pili ni nzito. Inabidi kujitolea na kujizatiti. Silaha za ngambo ya pili tunashidwa hata kuzitadhimini...zinarindimka..Ni kusafishana kila kukicha!

  Lakini mabingwa wamesema na wamefundisha kwenye vyuo vikuu vya mapambano kuwa muda kama huo ukifika, usijali aina ya silaha za upande wa pili...!

  Tumia silaha chache na nyepesi lakini...""repeat"" lakini...!

  Jenga Morali ya KuUenzi Utaifa, Uzalendo, Simamia Maadili ya Utu, Maarifa, Juhudi na kujiongoza vizuri, weka maazimio sahihi kwani Hivi ni "silaha kubwa". Na ndio silaha nzito ya JF. Silaha ambayo mpenda ukweli na haki hana sababu yeyote ya kumfanya arudishe hatua moja nyuma, zaidi ya kusonga mbele!

  Ikifikia hapo adui anakaribishwa kwa mikono miwili...kwani bila yeye tutamshinda nani? Bila object ya kushinda... ukombozi utapatikanaje? Maadui wana siginificant use value kwetu .. so tuwaambiaje? Most welcome!!

  Nafikiri hakuna njia rahisi kwenda kujenga Taifa angavu na madhubuti zaidi ya kujitolea wenyewe..KUJITEGEMEA!!!Hapa na pale patakuwa na kurupushani ..lakini nani alisema hatukutegema kuwa hazitakuwepo..? ni sehemu ya mwendo na they are well taken care!!
   
 4. Shukurani

  Shukurani JF-Expert Member

  #4
  Feb 28, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 253
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Maneno mazito sana haya Rev.Kishoka
  Haya maneno ya azimio la Arusha yalikuwa mazito sana. Tunahitaji nguvu kubwa kujikomboa na hili lazima liendelee. Tunajua wakuu ndani ya serikali wanapita hapa na mawazo na maono yetu wanayafanyia kazi. Bila shaka siku moja tutafika. Tunakuwa pamoja japo tunawakilisha toka nje ya mipaka yetu.
   
 5. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #5
  Feb 28, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Ndio
  Ndio ila wana Maisha Magumu
  ila imeuzwa kwa Wakoloni mamboleo,Buzwagi
  hapana,Kula zinaibiwa waziwazi,rejea uchaguzi wa ubungo,Bukoba n.k
  hili lina walakini,tunao bora viongozi na wasanii
   
Loading...