Securelens
JF-Expert Member
- Sep 28, 2020
- 316
- 541
Repoti za Waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa zimeeleza kuwa uchaguzi uliofanyika nchini Oktoba 28 na mchakato wake wote ulikuwa huru na wa haki. Miongoni mwa Taarifa zilizotolewa jana mbele ya waandishi wa habari ni pamoja na repoti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo timu yake iliongozwa na Rais wa zamani wa Burundi Mheshimiwa Sylvester Ntibatunganya.
Jumuiya hiyo imesema walikuwa na watazamaji 59 waliotawanywa mikoa 13 nchini na walifuatilia kwa undani uchaguzi kwenye vituo zaidi ya 160 za kupigia kura maneo mbalimbali nchini zikiwa za mfano zikiwakilisha vituo vingine.
Waangalizi waliokuja nchini siku saba kabla ya siku ya uchaguzi mkuu na kushuhudia kampeni pamoja na kuzungumza na viongozi wa vyama vya CCM, CHADEMA na ACT-Wazalendo wameeleza juu ya kuridhika kwao kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wa haki na matokeo yake yameakisi matakwa ya Watanzania.
Taasisi nyingine ya Kimataifa iliyotoa repoti kama hiyo ni ile ya EISA.