Reported Content: Post in thread 'Fahamu haya kuhusu Dubai kwa upande wa Teknolojia'

Status
Not open for further replies.

Tanzania Tech

JF-Expert Member
Dec 8, 2016
355
276
Post in thread 'Fahamu haya kuhusu Dubai kwa upande wa Teknolojia' by nelly poul has been reported by Tanzania Tech. Reason given:
Makala kwenye uzi huu imechukuliwa kwenye
tovuti ya Tanzania Tech bila ruhusa yoyote makala halisi inapatikana kwenye link hii https://tanzaniatech.one/2017/07/dubai-na-teknolojia/

Content being reported:
Tunafahamu kuwa Dubai ni moja ya nchi tajiri sana duniani, ambayo imepiga hatua kubwa sana kwa upande wa uchumi na teknolojia ya hali ya juu. Ni moja kati ya nchi inayokuwa kwa kasi sana duniani,kutokana na utajiri wake wa mafuta pamoja na rasilimali zingine. Haya sasa Dubai wamekuja na hizi tena kwa upande wa tknolojia;

POLISI ROBOTI KWENYE MIJI MBALIMBALI YA NCHI YA DUBAI (FIRST ROBOTIC COP JOIN DUBAI POLICE).

Polisi roboti hawa wametengenezwa hasa kwa lengo la kulinda nchi ya dubai kwenye miaka ya hivi karibuni. Roboti hao wana urefu wa futi 5,pamoja na uzito wa kilogram 100,wametengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu sana yenye uwezo wa kusoma tabia ya mtu,kwa kuangalia sura (facial expression),ikiwa pamoja na sensor mbalimbali,na kamera zenye uwezo wa hali ya juu wa kutuma video na picha,kwenda makao makuu ya polisi nchini Dubai..duuh hii teknolojia ikifika tanzania sijui itakuaje????.

MAGARI YA KIFAHARI YA POLISI (SUPERCAR POLICE PATROL IN DUBAI).

Kwa bongo na labda nchi nyingine nyingi,aidha Africa au nchi kadhaa ulaya au marekani,tumezoea kuona gari za kipolisi zikiwa za kawaida sana na wala sio za kifahari sana,tumezoea kuona zikiwa za miundo ya kawaida na iliyozoeleka ya kipolisi. Kwa bongo hapa nyumbani gari za polisi (defender au toyota land ctuiser), unakuta zingine zimechoka na kuchakaa tofauti na za nchi za jirani za hapa africa na hadi ulaya, Haya sasa!!!! kwa upande wa nchi ya Dubai,imekuwa tofauti kidogo. Magari ya polisi ni ya kifahari sana na ya gharama ya hali ya juu sana,ambayo yako tofauti na magari ya raia wanaoishi humo (private cars). Jeshi la polisi nchini humo lina magari kama Lamborghini, Bugati, na mengine mengiii!!!!... noma sana hii!!.

MAGARI YALIYOTENGENEZWA KWA GOLD (GOLD EXOTIC SUPERCARS ONLY IN DUBAI).

Magari haya unaweza kuyaona pekee katika miji ya nchi ya Dubai,magari haya mara nyingi unaweza kuyaona kwa watoto wa matajiri,au matajiri wenyewe wenye visima vya mafuta nchini humo.Magari hayo yanatengenezwa kwa kupakwa Gold,amabyo hupakwa kwa kiasi kikubwa sana kwa asilimia 85 ya gari hilo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom