Report ya Ufisadi iwekwe wazi - Rais Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Report ya Ufisadi iwekwe wazi - Rais Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gamba Jipya, May 14, 2011.

 1. G

  Gamba Jipya JF-Expert Member

  #1
  May 14, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 403
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu ameamuru ile REPORT YA UFISADI itolewe kwa public ili watanzania wawajue wabaya wao, kazi ipo.

  Hongera JK

  TUHUMA za ufisadi zinazoikabili serikali zimechukua sura mpya baada ya Rais Jakaya Kikwete kuagiza ripoti ya tathmini ya rushwa ianikwe mbele ya umma ili uweze kufahamu kabla ya kujadiliwa na Baraza la Mawaziri.

  Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, katika mkutano wa pamoja na nchi wahisani.


  Wakati hayo yakiendelea ndani ya serikali wadau wa kimataifa wa maendeleo kutoka nchi 12 duniani wameamua kuchangia bajeti ya serikali ya Tanzania kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012 dola za Marekani milioni 580 sawa na sh bilioni 840 kwa ajili ya shughuli za maendeleo huku nchi za Uholanzi na Uswisi zikitangaza kijitoa kuchangia bajeti kutokana na mtikisiko wa uchumi.


  Fedha hizo ni nyingi ukilinganisha na sh bilioni 814 zilizotolewa mwaka wa fedha uliopita huku wadau kutoka nchi mbili wakijitoa.


  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu, serikali imejigamba kuwa pamoja na kujitoa kwa nchi ya Uholanzi na Uswisi bado imeweza kufanikiwa kupata kiasi kikubwa cha fedha.


  Hata hivyo nchi hizo zimesema kuwa zitaendelea kufadhili miradi yao ya maendeleo nchini.


  Akitetea mbele ya wahisani hao, ambao mara kwa mara wamekuwa wakitishia kusitisha kuchangia bajeti kutokana na kuwapo kwa tuhuma za rushwa dhidi ya serikali, Waziri Mkuu Pinda alisema ripoti ya hali ya rushwa nchini imetoa picha halisi ya hali ya rushwa na inatarajiwa kutolewa wakati wowote baada ya taratibu kukamilika ili iweze kutangazwa kwa umma na kisha wananchi waijadili kwa kina.


  Pinda alisema alikuwa hajui suala hilo lakini kwa siku ya jana alibahatika kuongea na Rais Kikwete na ndipo aliporuhusu tathmini ya ripoti hiyo itolewe kwa Watanzania na hakuna sababu ya kusubiri hadi kujadiliwa na Baraza la Mawaziri.


  Alisema ufadhili wa kukamilisha tathmini hiyo ulifanywa na wadau hao wa maendeleo kutoka nchi mbalimbali duniani ambao walitaka kufahamu kiwango cha rushwa na maeneo ambayo inaonekana kuota mizizi huku wananachi wakiendelea kuwa maskini.


  Alisema baada ya kutolewa kwa fedha za ufadhili huo kazi ikaanza kwa waliopewa jukumu hilo ambao ni Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) kwa kuzunguka kwa wananchi.


  Pinda alisema serikali inaendelea kukabiliana na kupambana kwa nguvu zote na rushwa nchini lakini akaongeza kuwa ni wakati muafaka kuhakikisha mianya ya rushwa iliyopo katika maeneo mbalimbali inazibwa na kuiwezesha nchi kupata mapato.


  "Wadau wa maendeleo wamesisitiza umuhimu wa kuendeleza juhudi katika kupambana na rushwa na hata kutoa fedha kiasi kikubwa kama hicho ni wazi wamefurahishwa na kazi nzuri tunayoifanya.Hivyo tutaendelea na kazi hiyo," alijitetea Pinda.


  Kwa upande wake Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo alisema fedha hizo zilizotolewa kwa ajili ya kuchangia bajeti ya mwaka wa fedha ujao ni hatua nzuri inayoonesha bado wafadhili wana matumani makubwa katika kusaidia maendeleo ya wananchi na kuongeza kuwa safari hii wahisani hao wameamua kuongeza ufadhili ukilinganisha na mwaka uliopita.


  Nchi zilizochangia kusaidia bajeti ni Canada , Demark, Umoja wa Nchi za Ulaya (EU), Finland, Ireland, Japan, Norway, Sweden, Uingereza, na Benki ya Dunia (WB).


  Naye Mwenyekiti wa Wadau Maendeleo wa Kusaidia Bajeti Kuu ya Serikali (GBS) anayemaliza muda wake, Balozi wa nchi ya Norway, Ingunn Klepsvik, alisema pamoja na kutoa kwa fedha hizo bado kuna maeneo ambao Serikali ya Tanzania inatakiwa kuweka kipaumbele katika kuendeleza mapambano dhidi ya rushwa.


  Aidha alisema hata kama kuna masuala ya changamoto katika utekelezaji bado wanasisitiza kuwa iko mbele zaidi ya nchi nyingine za bara la Afrika.


  Mwenyekiti huyo alisema kuwa bado Tanzania haijaweza kugharamia shughuli za maendeleo kwa kutumia makasanyo yake ya ndani.


  Alisema kuna uhitaji wa kuongeza makusanyo katika mapato ya ndani ili kuiwezesha serikali kujiendesha kwa kutumia fedha zake.


  Alisisitiza umuhimu wa kuongeza kodi kutoka sekta ya madini kwa sababu sasa hivi makusanyo yanyotokana na sekta hiyo yanaendelea kuwa chini.


  Klepsvik alisema serikali inatakiwa kuweka mkazo katika maeneo matatu ambayo ni kutoa huduma ya jamii kwa usawa na ubora.


  Maeneo mengine aliyoishauri serikali kuweka mkazo ni ukuaji endelevu katika sekta ya kilimo ambayo inabeba watu wengi walio maskini.


  Pia alishauri serikali akisema kuwa ni lazima ibadilishe mazingira ya biashara na uwekezaji.


  Kati ya maeneo mengine ambayo alishauri kuboreshwa ni katika utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa.


  Cchanzo: Tanzania daima la leo
   
 2. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #2
  May 14, 2011
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Hizi ngonjera zitaisha lini jamani?! Khaaa... this is disgusting sasa! Hayo mahujumu uchumi yamejulikana zaidi ya miaka 3 sasa, tunacho hitaji nikuona inaswekwa lupango na si kutaka kuijua tena!! :(
   
 3. G

  Gamba Jipya JF-Expert Member

  #3
  May 14, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 403
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu tunataka kupate maoni ya wananchi kwanza, haya mambo yanaenda kisayansi mkuu, ni report ya 2009.
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  May 14, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  asingeamuru kutolewa wafadhili wasingesupport bajeti yake hakuwa na uchaguzi.
   
 5. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #5
  May 14, 2011
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Maoni ya wananchi?! Kwani hii ni referendum kuunganisha nchi?!! Katiba ipo, sheria zipo... deal with it, and do so immediately. Pussyfooting on matters of national interest has a gravely outcome!

  Besides, maoni ya wananchi kuhusu majambazi ya mali ya umma ni kupigwa mawe hadharani!!
   
 6. G

  Gamba Jipya JF-Expert Member

  #6
  May 14, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 403
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu punguza jazba, ile report ilikuwa ijadiliwe na baraza la mawaziri pekee, lakini JK ameamuru iwekwe wazi kwa public ili wananchi waijadili.

  India wazima lakini?
   
 7. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #7
  May 14, 2011
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Umesema ni report ya 2009, mawaziri wamekuwa wakilipwa mishahara kipindi chote hiki in btn mpaka leo hii kwa kazi gani? Iwapo report muhimu kama hiyo walikuwa hawaijaijadili mpaka leo?! Is it coz half of them are implicated, or?! Any plausible reasons for delay pls...
   
 8. K

  Kijallo JF-Expert Member

  #8
  May 14, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 409
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  JK huyuhuyu aitoe kwa wananchi?hiyo ni danganya toto kwa wafadhili,akiitoa kwa watz itaandikwa kwa kiingereza,
   
 9. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #9
  May 14, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Wakishaijadili maoni yao yatazingatiwa?
   
 10. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #10
  May 14, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Vipi kuhusu ile report ya kina Hosea, Mwema na Mnyika(ret.) kuhusu EPA? Yenyewe hainikwi ili wananchi wajue kilichomo? Usanii mwingine!
   
 11. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #11
  May 14, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,047
  Likes Received: 3,080
  Trophy Points: 280
  Kama ni maoni tunaanzia humu ndani,mimi sikubaliani na ufadhiri huu wa kishikaji,hii nchi imesheeni resources za kutosha kutufanya kuwa independent,haya mambo ya ufadhiri ni upuuzi mtupu kwa nini hatujifunzi kujitegemea miaka50 ya uhuru,ukizingatia 40% ya bajeti ndo hyohyo tunakopeshwa na ndo hyohyo utafiti unaonesha inaishia kwa viongozi wetu wezi

  pili nadhani ama tufadhiriwe ama tusifadhiriwe,tunachokitaka sie ni kuyaona na kuyaishi maisha bora na kutimiziwa ahadi tulizoahidiwa,full stop,tunataka maendeleo ya watu na si ya vitu.

  Kwani ufadhiri umeanza leo?waweza kureveal ni kwa kiasi gani kama taifa tumefaidika,je mwaka huu ndo tuone tutafaidika ama ndo vile wakubwa wanakinga viganja ili wakaendelee kujenge mahekaru nchi nzima na kuendelea kuwasomesha watoto wao ughaibuni huku wa kwetu wakiendelea kusota na kayumbas
   
 12. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #12
  May 14, 2011
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Hivi hii TAKUKURU inafanya kazi gani? kwa nini wasiireform??. Na hawa wafadhili nao kwa nini wanatoa pesa kwa hii rotten government??? they really need to stop giving money to Tanzania so that we can learn our fate!! aishhh!
   
 13. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #13
  May 14, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Sipendi tujisifu kwa fedha za msaada kutoka kwa wahisani wakati nchi yetu ina kila kitu kuanzia angani majini mpaka ardhini.
   
 14. Keynes

  Keynes JF-Expert Member

  #14
  May 14, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 499
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Mkuu kama vile ulikua kwenye kichwa changu......Mwaka jana wa bajeti waliwatoa kafara kina mramba na yona kuonyesha transparent mwaka huu naona wamekuja na jipya.

  Kweli ****** kwa siasa tu hajambo.
   
 15. s

  seniorita JF-Expert Member

  #15
  May 14, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  It is a blunt lie to say wananchi waione na wasome....wakati wananchi wanahangaika kutafuta how to make a day, je ni wangapi watasoma na kutoa maoni yao?asi tungeweza kufuatilia events, read them and comment critically on them. Most of our wananchi wangekuwa kama wananchi wa nchi zilizoendelezwa na viongozi wao basi wangefuatilia isuses, wangesoma na hata kutoa critical comments. Contrarily, the majority of our people live in the deep villages, languishing in deep poverty, and caught up in deep crises of life. How can they be of use in analyzing this situation? Then what is the role of constitution and legal department in this country? Hayo yalisemwa tu ili mkate usisitishwe na wafadhili, kwani kama alimaanisha wananchi kuhusika, kwanini hakufanya before the coming of wafadhili? That is such a sad move....and a blunt lie...
   
 16. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #16
  May 14, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Huyu Rais wenu sijui mimi nimwite nini au nani ...... Naomba mnisadie kumpa jina.
  Anafanya mambo kwa kureact tu hakuna jambo ambalo yeye amepanga kufanya ila ni kusbiri upepo unasemaje. Hii nchi ni kama inaongozwa kwa ramli. Haya ndo matatizo ya kuwatumia akina shehe yahaya kuongoza nchi.

  Hii report uwa garagaza haitakuwa na kitu chochote cha maana kwa watatnzania. Mie nawaahidi mtakao isoma mtalia maana pesa yenu itakuwa imetumika kuandaa upuuzi tupu. Utakuta report imejaa maoni tupu hata haweki wazi ufisadi mkubwa mnaoufahamu na hatuwa zitakazochukuliwa.
  Report itajaa rusha ndogondogo tu za uchaguzi wa mwaka jana na za mahakimu wa mahakama za mwanzo na watumishi wadowadogo wa serikali.
  Report hiyo kamwe haitasema ni wafanyabiashara gani hawalipi kodi na watumishi gani wanashirikiana na wafanyabiashara wakubwa kuihujumu nchi.
  In short hii iko kiusanii zaidi ili wahisani watoe tu msaada.

  Halafu PM na Mulo wanajisifia kupewa msaada, haya majamaa hayana hata aibu, eti mwaka huu msaada umeongezeka zaidi!
  Hatutaweza kufika tunakoenda kwa kubaki na hii serikali ya ccm iliyozoea misaada na hata siku moja haiwezi kuendesha nchi bila kusaidiwa. Hawa magamba wamezoe kula mapato yote ya ndani na kutegemea misaada tu. Tunadanganywa kila leo mapato yetu ya ndani ni kidogo kitu ambacho si kweli yanagawanwa na watumishi wa TRA na vigogo pamoja na wafanyabiashara wakubwa.

  Kama chadema watachukuwa serikali kitu cha kwanza ni kuanza kujitegemea badala ya kuwaramba miguu wa fadhiri. Kenya wanafinance budget yao kwa asilimia 90 na hawana resources kama za kwetu zaidi ya kilimo na ufugaji na maana wafadhiri hawana lao pale na wakenya wako very proud na maendeleo yao.

  sisi tuna kila kitu kinachoitwa natural resource lakini hatuna lolote tunalofanya zaidi ya kufanya umatonya kwa wazungu.

  Hivi mkulo ni kabila moja na Matonya, mbona anafurahia sana kuombaomba?

  PM naye umasikini umezidi hawezi hatakujikakamua kidogo anapiga magoti na anashiriki usanii wa mkwele kuw watatoa report ili wapewe tu msaada, shame on you PM ni kheri tungekuwa na PM fisadi angekuwa na kiburi kuliko masikini anayewatetemekea wafadhiri!

  My conclusion is taht JK leadership will never take us anywhere economically!
  Tutaendelea na maisha ya kawaida ya mlo mmoja kwa siku ntena wa chapati na chai maana ndo mswahili anacholidhika nacho. Ndo maana bidhaa ya muhimu kwa mswahili ni sukari ndo maana hata mkwele aliongelea kushusha bei ya sukari tu utadhani watanzania tunakula sukari., lakini ndo uswahili huo.

  Kilichobaki ni kumwomba Mungu atupe uvumilivu kama alivyoimba Rose mhando maana bila hivyo yanaweza kutukuta ya misiri hapa.
   
 17. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #17
  May 14, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hata hivyo hii ni ripoti ya utafiti/uchunguzi upi wa rushwa hapa nchini? Utaona kwamba ni ule uliofanywa na TAKUKURU ya Hosea kimya kimya na utakuta imejikita zaidi katika rushwa za matrafiki polisi, manesi hospitalini, makarani wa mahakama n.k. n.k. -- kwamba hizi rushwa ndizo hasa zinawatesa Watz.

  Inawezekana kweli zinawatesa Watz, lakini kukosekana kwa uchunguzi wa kina wa ufisadi wa wakubwa -- kama vile EPA kwa mfano unaonyesha kwamba hiyo ripoti itakuwa changa la machoni tu -- kwani itakuwa imewasevu wakubwa.

  Kama JK na serikali yake ina jeuri kubwa kuhusu vita ya ufisadi basi na aitoe hadharani ripoti ya uchunguzi wa EPA iliyofanywa na kamati ya akina Mwanyika, kama kweli an nia ya kutaka asifiche kitu.

  Hawezi kufanya hivyo kamwe kwani naye yumo katika hiyo EPA.

  Hadi lini Watz watakuwa wanafanywa mafala na serikali ya JK katika vita hii ya ufisadi?
   
 18. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #18
  May 14, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Wanaweza kuitoa ikiwa imechakachuliwa isiwe na uzito wowote..
   
 19. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #19
  May 14, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  punguza munkari na usiwe judgmental mapema hivi. Taarifa iliyopo ni kwamba ripoti itatolewa. Itahusu nini, itakuwa na ukubwa gani, itakuwa katika lugha gani siyo masuala ya kujibu sasa hivi kwa sababu ripoti haijaonekana. Na suala la lugha hapa ni wale walioitayarisha!
   
 20. Chifunanga

  Chifunanga JF-Expert Member

  #20
  May 14, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 291
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Aache kutuyeyusha bana....mafisadi wanajulikana, walitajwa mwaka juzi, wakatajwa tena mwaka jana wakati wa uchaguzi......na pia wametajwa wakati CCM wanajivua gamba.......sasa JK anataka watajwe tena???

  Jamani jamani......tafadhali jamani, mnaongeza tu hasira za wananchi!
   
Loading...