Ripoti ya CAG 2019/2020 na BoT Januari - Machi 2021 itamuinua Rais Samia iwapo atachukua hatua kali

jojipoji koromije

JF-Expert Member
Mar 22, 2017
991
1,412
Wanabodi Nawasalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Awali ya yote Niombe kumpongeza CAG Kichere kwa kuandaa report ya hesabu za Serikali ya mwaka 2019/20 yenye uwazi wa hali ya juu.

Huu ndio tunauita Uzalendo uliotukuka!! Ametusaidia watanzania kujua hata ile miradi tuliyoaminishwa kuwa inatengeneza faida na kutoa Gawio kumbe ukweli ni kuwa walikuwa wanatengeneza hasara, mfano ATCL nk, lakini ripoti hiyo pia imefichua matumizi ya hovyo kama sio ufisadi wa fedha zetu walipa kodi katika taasisi na wizara mbalimbali kama vile Utalii na Mali asili, pia ametuonesha baadhi ya taasisi za Serikali zilizogoma kutoa taarifa zao za fedha kwasababu wanazozijua wao kama vile TANESCO, Hospitali ya Taifa Muhimbili na taasisi nyingine nyingi tu.

Wahusika waliohusika na matumizi mabaya ya fedha na ofisi za Umma bado wapo wanadunda tu na kufanya kazi kama vile hakuna lolote lililotokea.

Baada ya kupendezwa na Report hii ya CAG Mheshimiwa Rais Samia akamuagiza afanye ukaguzi wa taarifa za fedha zilizotoka BOT kwa kipindi cha kuanzia January mpaka March 2021; ni matumaini yangu kwa umahiri wenye uzalendo wa hali ya juu sana aliouonyesha CAG Kichere atatuletea report nzuri sana ambayo itasomwa kwetu wananchi ili tujue ni nani alichota keki ya Taifa kwa manufaa binafsi na itabidi wahusika wawajibishwe.

Kwa hiyo ukiangalia reports hizi mbili muhimu sana za CAG ni reports ambazo zitamuinua sana Mheshimiwa Rais Samia kama ataagiza wale wote walioguswa na taarifa ya CAG washughulikiwe kwa mujibu wa Sheria za Nchi yetu.

Naomba asiangalie nafasi ya mtu yeyote hata kama atakuwa kamteua hivi karibuni; kwani akiwawajibisha namhakikishia watanzania nikiwemo mimi binafsi watampongeza sana na imani juu ya uongozi wake itaongezeka maradufu

Ni heri kuziba ufa sasahivi kuliko kuuacha na mwisho wa siku nyumba kubomoka! Namshauri Mama asikubali kuangushiwa jumba bovu! Wajibisha wahusika wote wa taarifa ya CAG ili Tanzania tubaki salama na wewe!! Tunakuamini Mama najua hauto tuangusha.

Shida kubwa nayoiona ikiwa Mama atawakalia kimya wale watuhumiwa wote wanaoguswa na taarifa hizi za CAG Kichere na kuwafumbia Macho.

Hii itakuwa hatari sana kwa uongozi wake kuaminiwa tena na wananchi!! Imani ikiporomoka hata matumaini ya Uchaguzi wa 2025 yataporomoka.

Naomba nimalize kwa kumuomba Mheshimiwa Rais Samia kuwachukulia hatua kali kwa mujibu wa sheria za Nchi wahusika wote waliotajwa kwenye taarifa za CAG bila kujali nafasi zao au hata kama aliwateua hivi karibuni.

Sisi watanzania tuko pamoja nae. Asihofu Ni heri kujirekebisha kuliko kuishi na Makosa maana hautokuwa na imani katika safari ya Uongozi Wako.
 
Hakika mkuu. Ingawa uandishi wako ni wa hovyo sana mpaka kwenye kusoma inakuwa ni ngumu sana. Huzingatii kanuni za uandishi kabisa kama kuweka aya, kituo, n.k. AU ni COPY & PASTE?
 
Back
Top Bottom