Report: Mv Spice ilibeba abiria zaidi ya 3500 wakati uwezo wake ni abiria 600'

NDOFU

JF-Expert Member
Feb 23, 2009
656
144
Hayo yameelezwa na makamu wa pili wa raisi Zanzibar Balozi seif Idd akitoa taarifa kuhusiana na Riport ya uchunguzi wa ajari hiyo.Maiti zilizopatikana ni 200 huku waliokolewa hai ni zaidi ya 600 hvyo idadi ya wale abiria wasiojulikana walipo ni 2700! Hakika ni uzembe usiosemeka!
 
Kwa nini Balozi amesema maneno machache hivi ndiyo reprt nzima hii au ni wewe umeamua kuleta machache mengine umekalia?Tuta jadili nini sasa hapa mkuu .Umesha sema kwa uchache na umesema ni uzembe usio someka si kzi umesha imaliza au ?
 
Kwamba huo ndio ukweli wa idadi halisi? Kama ndivyo mimi nina-double the number. HakyaMungu!?!!
 
Kwa nini Balozi amesema maneno machache hivi ndiyo reprt nzima hii au ni wewe umeamua kuleta machache mengine umekalia?Tuta jadili nini sasa hapa mkuu .Umesha sema kwa uchache na umesema ni uzembe usio someka si kzi umesha imaliza au ?

He's sharing his excitement with us.
 
Hapo kuna tatizo. Naomba utuwekee ripoti nzima ili tuweze kuujadili.
 
Hili suala ni zito sana, haipaswi kuleta suala kama hili jamvini kwa mistari miwili halafu ukategemea tujiachie kwa mapana na marefu yake, kindly mtoa mada tudadavulie report kamili na source then wanajamvi tuta chip in.
 
Kwa nini Balozi amesema maneno machache hivi ndiyo reprt nzima hii au ni wewe umeamua kuleta machache mengine umekalia?Tuta jadili nini sasa hapa mkuu .Umesha sema kwa uchache na umesema ni uzembe usio someka si kzi umesha imaliza au ?

Sasa mkuu unataka nikuletee ripoti ya kurasa Ngapi? Me nimekujuza kadri habari nilivyoipata!
 
Hapo kuna tatizo. Naomba utuwekee ripoti nzima ili tuweze kuujadili.

Nikuwekee riport nzima?! Hebu jaribu kuwasiliana na wasaidizi na balozi Seifu Idd nadhani wanaweza kutusaidia kwa hilo!
 
ni disaster ni janga lini tutajifunza? kwa nini hawa step down? aah nilisahau kumbe ni tz! watu wanakufa lakini hakuna wa kuwajibika!
 
Hili suala ni zito sana, haipaswi kuleta suala kama hili jamvini kwa mistari miwili halafu ukategemea tujiachie kwa mapana na marefu yake, kindly mtoa mada tudadavulie report kamili na source then wanajamvi tuta chip in.

Kaka huhitaji ripoti kufahamu uzito wa ajali ya mv Spice. Ushuhuda waliokuwapo bandarini on the fateful day unatasho. Mv spice islander saga stinks ,its bad its high crime yet non of us is humble enough to pay reverence to the victims. Mwenyezi Mungu Warehemu Marehemu.
 
Ilikuwa wazi kwani haiingii akilini eti wapiga mbizi hawawezi kwenda meli ilipo na hivyo wakasitisha zoezi inamaana waliogopa kilio cha wapemba!!
 
Hayo yameelezwa na makamu wa pili wa raisi Zanzibar Balozi seif Idd akitoa taarifa kuhusiana na Riport ya uchunguzi wa ajari hiyo.Maiti zilizopatikana ni 200 huku waliokolewa hai ni zaidi ya 600 hvyo idadi ya wale abiria wasiojulikana walipo ni 2700! Hakika ni uzembe usiosemeka!

Naweza kuwa sahihi nikisema waliokufa ni
2700 + 200 = 2900?.

Kuna speculations kwamba serikali iliamuru shughuli za uokoaji zisitishwe kuficha aibu na kihoro cha kukuta melini kuna maiti karibu 300!

Hakuna aliye wajibika hadi sasa!
Wajiuzulu sasa.
Au serikali iseme walitakiwa kufa wangapi ili viongozi wenye dhamana wawajibike kwa kuachia ngazi.

3000?!!!!!
Mungu tusaidie wa TZ.
 
Waziri anayehusika na hii wizara si anatoka Cuf?! Ngoja tusubiri tuone kama Cuf nao wanaweza kuwajibika.
 
Ingekuwa China bila kujali wadhifa wa yeyote aliyezembea nakusababisha vifo na vilema vya maisha kwa raia wasiokuwa na hatia kwa maslahi kesi isingechukua hata mwezi.

Wenye hatia ingekuwa kunyongwa mpaka kufa lakini kwa vile huku ni nchi yakusadikika tume itachunguza taarifa inaweza ikatoka au isitoke siku miezi miaka itapita taratibu kimyakimya itasahaurika.

Kesi itasuasua ilimradi muda unaenda kwa kisingizio cha ushahidi haujakamilika hapo kweli tunahitaji Scotland Yard kutusaidia upelelezi? Lakini mwisho wa siku watuhumiwa wataachiwa na maisha yataendelea kama hakuna kilichotokea tukisubilia limeli lingine liwe kaburi la raia.

Baada ya janga la Mv Bukoba sikutegemea kama serikali inayowajali watu wake ingeshindwa kuchukua tahadhari za makusudi kuona kuwa vyombo vya majini vinadhibitiwa ipasavyo kwa usalama wa abiria Haingii akilini chombo chenye uwezo wakubeba watu 600 kinabeba watu 3500 kama vile hakuna mamlaka zinazodhibiti usafiri wa majini.

RIP wahanga wa ajali hii mbaya.
 
Imethibitishwa kuwaa meli ilibeba abiria 3589,waliopatikana maiti 203,waliookolewa ni 610,ambao hawakupatikana mpk sasa ni watu zaidi ya 2800,hii nikwamujibt wa ndugu wamarehemu waliotoa idadi yandugu zao waliopanda meli hiyo na ambao mpk sasa hawajapatika wameshakufa,ni janga kuu la kitaifa,anatakiwa waziri ajiuzulu bila kuwasahau watendaji wote wa bandari yamalindi zenj ambao wana dhamana ya usafiri na ukaguzi wa vyombo vya majini,bila kumsahau mkurugenzi wa bandari mustafa abood jumbe ambae watu wengi wanamlalamikia kwa utendaji wake mbovu wa kazi na kupenda rushwa,wasipotaka kujiuzulu wenyewe tunakuomba rais shein wafukuze kazi wajinga hawa.
 
Swala la kuwajibika nashauri liingizwe kwenye katiba mpya.
Litaboresha sana utendaji.
Kwa sasa inonekana ni optional na sijui kama kuna sheria ya kumlazimsha mtu kuwajibika au kumlazimsha rais kumwajibsha mtu kutokana na uzembe.
Liwekwe kwenye katiba ili kuondoa uwezekano wa wananchi kuamua kuingia mtaani kutafuta haki.
Kuiwajibsha serikali nzima.
 
Waziri anayehusika na hii wizara si anatoka Cuf?! Ngoja tusubiri tuone kama Cuf nao wanaweza kuwajibika.

Maalim sheif siku moja akitokea ughaibuni baada ya kusikia wazira mhusika kaandika barua ya kujiuzulu, akatoa tamko kuwa waziri asubiri hadi riport ya tume. Sasa tusubiri.
 
Back
Top Bottom