Report: Makamba backed Manji in suspect land deal (THISDAY)

Mugishagwe

JF-Expert Member
Apr 28, 2006
300
58
THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

NEW details are emerging about the conspiracy over the grabbing of a prime piece of land from the National Muslims Council of Tanzania (BAKWATA) allegedly masterminded by Yusuf Manji’s Quality Group Limited in Dar es Salaam.

THISDAY can reveal how the move was fraudulently hatched, resisted, and eventually pushed by top government officials in the city.

An internal report into the scandal commissioned by BAKWATA says Dar es Salaam Regional Commissioner, Yusuf Makamba, gave his full backing to Mr Manji in the controversial project.

The report was written by a team of BAKWATA sheikhs appointed by the Chief Sheikh, Mufti Issa Shaaban Simba, to investigate the scandal over the property.

According to the report, it was only thanks to the intervention of the former Minister of State in the President’s Office (Regional Administration and Local Government), Brig. Hassan Ngwilizi, that Quality Group’s attempt to develop the land was thwarted.

Brig. Ngwilizi, who lives near the BAKWATA property at Chang’ombe suburb, had objected to the private development of the plot by Mr Manji’s company, the report says.

However, it is alleged that while Brig. Ngwilizi was away for election campaigns last November, Mr Manji quickly seized the opportunity by writing a letter to Dar es Salaam Regional Commissioner, Yusuf Makamba, seeking his help in pushing forward his company’s project.

In the letter dated November 8, 2005, Mr Manji complained about the ’’delay in issuance of the building permit by the Temeke Municipal Council.’’

’’It is now more than 18 months since the date of our application, yet to date, Temeke Municipal Council has not issued us with the Building Permit,’’ Mr Manji said in the letter to Mr Makamba.

He added: ’’Considering the above situation, we seek your office?s intervention at the soonest.’’

Mr Makamba then obliged by instructing his assistant -- the Dar es Salaam Regional Administrative Officer ? to order the Temeke Municipal Council to expedite approval of the building permit to Quality Group.

’’What’s the meaning of this bureaucracy ? we should not discourage investors. (Eliya) Ntandu should supervise this and give them (Quality Group) the building permit,’’ Mr Makamba ordered in handwritten instructions to his assistants on Mr Manji’s letter.

In the memo that the Dar es Salaam RC expressly wrote on the same day of the delivery of Mr Manji’s protest letter, Mr Makamba declared that the disputed property belonged to Quality Group.

Working on Mr Makamba’s orders, the Temeke Municipal Council was forced to grant a building permit to Mr Manji’s company, which immediately built a fence made of corrugated iron sheets around the plot.

The 27-page report written by BAKWATA’s permanent probe committee established that there was fraud involved over the secret change of ownership of Plot Number 311/1 Block T at Chang’ombe to Quality Group.

BAKWATA had reserved the property for the construction of the proposed first Islamic University with the name Millennium University of Tanzania.

But in an unexpected twist, ownership of the plot was secretly transferred from BAKWATA to Mr Manji’s company, in what an internal BAKWATA report describes as ’’fraud and conspiracy.’’

Quality Group claimed to have legally gained ownership of the property with the full knowledge and consent of the Trustees of the proposed university.

However, it was later discovered that the certificate of incorporation issued to the Trustees was eventually withdrawn -- and subsequently cancelled.

The Administrator-General, Ms Christabella Kaisi, withdrew her letter of consent with reference number ADG/Ti/4 of October 2, 2002 given to the Trustees of the Millennium University of Tanzania after realizing that the consent was obtained by false pretence.
 
As a reward, tomorrow, June 20. He will be crowned another political position as MP dominated by president.

May GOD bless our poverty!
 
Makamba kama kiongozi wa mkoa aliingilia kati kutokana na habari alizopatiwa. Katika habari hiyo "This Day" wanajaribu kuonyesha kana kwamba Makamba alifanya kitu kinyume na sheria na hivyo kuachia taswira ya ubovu. Hata hivyo kwa kusoma habari hiyo sioni hata kidogo mahali popote ambapo Mbunge Mteule na Mkuu wa Mkoa wa Dar alishirika katika ufisadi wa aina yoyote. Kama kuna swali ambalo Mzee Makamba anapaswa kujibu ni "je kabla ya kutoa agizo hilo kwa mtendaji kufuatilia alikuwa na uhakika gani kuwa kiwanja ni mali ya Quality Group?

Hata hivyo, Makamba anaweza kuwataka "This Day" kutoa maelezo kama kwa habari hiyo wanamtuhumu yeye (Makamba) kushiriki katika kufanya kitendo chochote kinyume cha sheria na kama Mwanasheria Mkuu anafanya uchunguzi dhidi yake. Kutokana na Kichwa cha habari picha inaachwa kwenye mawazo ya msomaji ya kuwa Makamba alihusika kwa namna fulani kufanya kitendo cha kuvunja sheria. Jinsi gani?...

Report: Makamba backed Manji in suspect land deal

mantiki hapo ni hii:

1.Manji anatuhumiwa kununua kiwanja kiujanja

2. Halmashauri imechelewa kutoa kibali

3. Manji anaomba MM aingilie kati

4. Makamba anaingilia kati kuhakikisha Manji anapewa kibali

HIvyo,

Makamba na yeye ameshiriki kwenye kitendo cha ufisadi!!

Sasa huu ndio ninauita uandishi wa kiuchongezi!!! Subirini KLH News ianze kurusha mahojiano.. we'll put all these people on the spot!! I'm tired of this immature, biased, and unfair reporting!!!
 
Exactly, ndio uandishi mbuzi ninaousema, this Makamba man now yuko very close na JK, yeye sio mtandao ila yuko njiani kuwa kiongozi muhimu wa serikali na huenda karibuni tu atachukua nafasi ya Kingunge, sasa hivi the deal ni kuwaingiza watu wa nyumbani katika sehemu zote nyeti, kwani kama mkuu wa mkoa ni mbunge anyway why ubunge wa rais?
 
Jamani mweeee!
Ebu tuangalie maelezo haya kwa mai makini zaidi na sio mapenzi ya huyu mshirika.
Kulingana na maelezo ya mwanakijiji nambari 2 na 3 ndizo zilizosababisha kuwepo kwa namba 4.
Huyu makamba kama kiongozi lazima afuatilie namba 2 na kuelewa uhalali wake kisha 3 kabla ya kutoa uamuzi wa 4. Haya ndiyo matatizo tunayozungumzia ya hawa ma RC na DC kuwa wao ni miungu wadogo wa wilaya na mikoa. Ikiwa kibali cha ujenzi kimesimamishwa lazima ipo sababu na Makamba aliifahamu kama kweli yeye ni mchapa kazi. Documents zipo, simu zipo na ushahidi tosha kuwa ardhi ile bado ilikuwa mikononi mwa Bakwata. And he knows this personally nje ya ofisi yake kikazi.
 
Mwanakijiji,
Lazima uelewe kwamba kuna tofauti ya kiongozi na mtawala?
Baada ya kashfa zako kwa gazeti hili nimeirudia vizuri nione huo uandishi wa uchochezi. Hli gazeti limeripoti kutoka ripoti ya BAKWATA, siyo wao walioandika. Kama wameripoti habari ya uongo ambayo haimu kwenye hiyo ripoti basi hapo wana makosa. Kama Makamba anataka meelezo fulani kuhusu hiyo ripoti ni kwa nini aliulize gazeti kwani wao ndio walioandika hilo gazeti? Wao wameripoti. Ndiyo ripoti inaweza kuwa ya uongo lakini siyo kosa la gazeti. Soma vizuri hii habari hakuna mambo ya inasadikika au inaaminika wameweka wazi majina ya watu waliosema hayo mambo. Hii ripoti ina kurasa 27 wewe ulitaka waweke Dibaji? Lazime wachukue sehemu ambayo itauza na huo siyo uchochezi. I would careless nani ana makosa ila habari hii imenionyesha ni kazi gani tuliyonayo kuzipa serikali za halmashauri za miji nguvu ili ziwe na maamuzi yao bila kuingiliwa na serikali kuu.
 
Mzee Es salaam kwanza kwako na waheshimiwa wengine wote .Naamini katika kujadili na kuopata suluhu na si kurushiana ngumu na shutuka ambazo hazina maana japokuwa kila mmoja anayo haki ya kusema mawazo yake kwa usahihi au hata kwa mapenzi kama ambavyo imeonyeshwa hapa .

Mimi Mugushagwe hadi kuamua kuleta kesi hii ina maana nilisha ona majina ya wale watu wa Bakwata ambao wanasema na hali halisi maana wao wanahusika na Mgogoro huo .Wao wamesema na kulaumun kwamba Makamba aliamua kuwaumiza hawa watu .Sasa mimi nikasema well Makamba alisukumwa na kitu kuingila jambo hili kwa haraka sana namna ile ? Ama ndiyi mambo Manji sasa yanakuwa Maji na kwa kuwa naamini atakuwa ama alikuwa na close ties na Srikali iliyopita ama iliyopo ndiyo sababu ya Makamba kukikmbia hovyo na kutoa maamuzi ??

Makamba ni msema hovyo pia kama kweli hapa hajatendewa haki by now tungalisha sikia akisema jambo lakini bado ama kwa kuwa anataka kwenda kwenye kiapo anajiandaa ? Tungoje sasa yeye atasema nini maana atakwua kasoma haya yote .Kila mwenye point yake atajua pa kusimaa lakini kwa sasa tuna haki ya kuhoji Makamba alisukumwa na kitu gani kufanay maamuzi haya ??
 
Sam na Mugi... Makamba hana haja ya kujibu lolote kwani si ripoti ya Bakwata wala uchunguzi wa This Day unaodai kuwa alifanya kitu chochote kinyume cha sheria!
 
Mwanakijiji,
Mkuu wa serikali ya mkoa wa Dar Es Salaam in Makamba, ndiye mkuu wa wale manispaa ya Temeke, kwa hiyo yeye kuwaamrisha au kuwasukuma wale jamaa wa manispaa ni moja kwa moja ni responsible person. Sasa wewe kum-clear Makamba kama hausiki nashindwa kuelewa. Kwa nini Manji alichagua kumandikia barua Makamba? Kwa sababu tu alijua ndiyo mkuu wa serikali ya mkoa wa Dar Es Salaam. Suala ni administration. Sasa hata waislamu au Bakwata wakiamua kushitaki, moja kwa moja Makamba was a principal player on the deal, ana wasaidizi wake ambao wangefanyia hiyo kazi kabla ya kutoa amri kwa manispaa ya temeke. Hiyo ndiyo inadhihirisha ni kiasi gani viongozi wa serikali wasivyojua kufanya kazi zao.
 
Mzee Mwanakijiji said:
Hata hivyo, Makamba anaweza kuwataka "This Day" kutoa maelezo kama kwa habari hiyo wanamtuhumu yeye (Makamba) kushiriki katika kufanya kitendo chochote kinyume cha sheria na kama Mwanasheria Mkuu anafanya uchunguzi dhidi yake. Kutokana na Kichwa cha habari picha inaachwa kwenye mawazo ya msomaji ya kuwa Makamba alihusika kwa namna fulani kufanya kitendo cha kuvunja sheria. Jinsi gani?...

Nashukuru umejijibu mwenyewe. "This Day" hawajafanya uchunguzi wao wameripoti tu. Nimeisoma tena hii habari very professional ukilinganisha na habari nyingine za vyombo vingine vya habari. Sina uhakika na ukweli wa hiyo habari lakini inatia moyo kwamba kuna waandishi wengine wenye uwezo wa kuandika.
 
Mwanakijiji asante kwa kuwa msemaji wa Makamba .Ni kwa nji hii tutabaki kulumbana na kutetea maslahi binafsi badala ya Taifa na kuliangamiza.Makamba hajasema lakini umesema wewe haya kuliko mwenyewe ambavyo angalisema .Maana ya mimi kuzua hii hoja haikuwa kusema Makamba ni responsible ama hapana .Nilitaka tujadili mambo mengi ikiwemo kwa nini Manji akimbilie kwa Mkuu wa Mkoa na yeye kutoa amri kwa Hamshauri ya Temeke.
We really have a long way to go kama unazi huu utaendelea kumbe tuna faida binafsi mimi nilidhani tukanata issues kwa manufaa ya Tanzania ???
 
Huku ni kujidanganya kudhani ya kuwa TD wanaandika habari kwa uchunguzi wa kina na bila kuwa na upendeleo. Sam et al mmesema mmeisoma habari hiyo kwa kina na mnafurahishwa na uandishi wa uchunguzi. Labda niwaulize maswali haya ambayo yatawasaidia kuonyesha udhaifu mkubwa wa habari hizo.

a. Kabla ya kuripoti kuwa Makamba alihusika katika mchakato mzima wa Quality Group kupewa leseni, kwa kutoa amri ya kuharakisha mchakato huo na hivyo kuacha taswira ya Mzee Makamba kuhusika na kitendo cha ukiukwaji wa sheria, je TD ilifanya jitihada gani ya kuwasiliana na mzee Makamba na kupata maelezo yake kabla ya kuchapisha habari hizo, hicho kiundishi kinaitwa "Equal Access" m.y.n Ukimpa mpinzani wangu nafasi ya kusema kitu juu yangu, nipe na mimi nafasi ya kueleza upande wangu!!! Huendi hewani hadi umejaribu kupata upande wa pili wa habari!

b. Ingawa katika ripoti hiyo hakuna mahali popote panaposema kuwa Makamba amevunja sheria au amefanya kitendo kilicho nje ya uwezo wake, au amefanya kitendo ambacho hakijawahi kufanywa na kiongozi (no precedent), kwa makusudi kabisa waandishi wa TD wameamua kuwaacha watu watunge masuluhisho yao wenyewe juu ya Mzee Makamba na kuhusika kwake na deal hilo. Tena kwenye tovuti yao wameweka na picha ( ya mzee Makamba na Manji) kabisa isiyohusiana hata kidogo na habari!!! Lengo ni kufanya kile vyombo vya habari vilifanya dhidi ya Dr. Salim!! So far the damage has been done!

c. Ingawa mnataka kufikiri kuwa TD haina upendeleo, je deal zote alizowahi kufanya au anazofanya Mzee Mengi kwa kutumia makampuni yake zimefuata taratibu zote? Je kuna wakati wowote Mzee Mengi amewahi kwenda kwa kiongozi wa juu kuomba msaada wa kuharakishiwa jambo fulani kwani viongozi wa chini wanazembea na kiongozi huyo akaingilia kati? Of course hatujui, kwa sababu TD haiwezi, haitaweza na haiko tayari kuweza kumfanyia uchunguzi mzee Mengi.. why kwa sababu yeye ni mmiliki wa magazeti hayo na yumo katika bodi ya Wakurugenzi!!!!
Hivyo basi, swali ni je TD iko tayari kufanya uchunguzi wa shughuli zote za ippmedia, kama wamefanya kila kitu kwa mujibu wa sheria? Je ikitokea mtu ana ushahidi wa kuonyesha Mzee Mengi akiandika barua ya kuomba favor fulani toka kwa kiongozi wa juu gazeti la TD liko tayari kuchapisha barua hiyo na kusema kitendo hicho ni cha kiovu?

Mkinijibu maswali hayo labda naweza kuanza kulichukulia gazeti hilo kwa makini!! Sasa hivi hakuna chochote isipokuwa ripoti za kisasi, zenye upendeleo na zisizokuwa na nafasi sawa kwa wote!!!!
 
Mwanakijiji
Mbona unag'ang'ania kuwa TD wamefanya uchunguzi na ni wewe tu unayesema huo ni uchunguzi. Hiyo ni ripoti.
Pia naona kama msemaji hapo juu alivyosema umekuwa msemaji wa Makamba. Umejuaje kama TD hawakuwasiliana na Makamba kablya ya kuandika? Na sijaona mtu humu anasema Makamba amefanya makosa, tatizo ni system nzima.
hayo maswali yako mengine kawaulize BAKWATA hao ndiyo walioandika hiyo ripoti ya kurasa 27. Hata ukienda TD nao watakuambia nenda huko huko. Kuhusu Salim ni tofauti kabisa, hivi leo hii ukiambiwa utaje mtu aliyesema SAS ni mwarabu au muuaji utamtaja nani? Angalia hiyo ripoti ya BAKWATA imetaja wahusika kwa majina na nani aliyesema hakuna umbeya au upashkuna kama mtu inamuuma atasema mwenyewe.
 
Sam, inabidi uende kwenye tovuti ya "This Day" usome tamko lao kuhusu wao ni nani na wanafanya nini! Kama TD wameamua kuandika ripoti tu kutoka ile ya Bakwata, kwanini wasiichapishe ripoti nzima ili sisi tu waamuzi badala ya kumega vipande na kujaribu kutulisha!!? Hizi habari nusu nusu ndo miye nazipigia kelele. Mimi si msemaji wa Makamba au mtu yeyote, sina ajenda yoyote bali ile ya kuwapa watu nafasi sawa ya kujitetea!!!

Mwandishi yoyote wa habari ambaye yuko makini, huwezi tu kuandika ripoti na kuichapisha bila kuuliza maswali ya msingi!! Hayo ndo yaliyomkuta Dan Rather wa CBS na ninaona tatizo la watu wa TD.
 
Heeee!
Naona maoni yangu niliyoandika jana yamefutwa....vipi?
Anyway, inabidi nishushe pumzi na kuelewa kinachoendelea.
 
Admin,
Shukran inabidi nirudie nilichosema.
Makamba personally alifahamu bila makabrasha ya ofisini mwake kwamba kiwanja kile kilikuwa cha Bakwata. Na kesi ya kiwanja kile ilikuwa wazi na scandal ilifahamika kote juu. Pia sio Manji peke yake aliyejaribu kukichukua kiwanja kile kwa hiyo Mwanakijiji unapomtetea mtu hali wewe mwenyewe huna ushahidi inazidi kunitisha na nitasema tena mwenzangu unaendeshwa na hisia zako binafsi - dini. Inaonyesha wazi hukutaka kuyatazama madai haya kuwa ni maelezo TD wameyanukuu Bakwata ili kuhalalisha matokeo ya kesi nzima.
Makamba ni Judas, kanunuliwa kwa msukumo fulani ambao wewe na mimi hatuufahamu isipokuwa kutofuatilia kwake sheria na kuchukua madaraka mkononi mwake ni ishara dhahiri ya ukiukaji sheria na kuonyesha misuri ya RC.
Matokeo kama haya ndiyo yanayowafanya wananchi kupinga kuongozwa na RC badala ya kiongozi ambaye amechaguliwa na wananchi kwa maslahi yao. Bahati nzuri imekuja kwamba huyu RC sii mwamuzi wa mwisho, kesho ukweli utakuja toka na utashughulikiwa kitaifa. Ingekuwa serikali ya majimbo basi ndio imetoka hiyo!... na madhara yake tusingeweza kuyaongelea hapa.
 
Luteni Makamba ammiminia mabusu mfadhili wa miradi

2005-07-21 14:57:21
Na Maabad Msuya, Temeke


Baada ya kushindwa kujizuia kuonyesha furaha yake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Luteni Yusuph Makamba, amejikuta akimfagilia mfadhili wa miradi mbalimbali wilayani Temeke Bwana Yusuph Manji na kumtaka agombee ubunge wa jimbo la Kigamboni kwa tiketi ya CCM.

Kama vile haitoshi Mkuu huyo wa Mkoa kwa kuonyesha ni jinsi gani alivyovutiwa na kufurahishwa na ufadhili huo, aliamua kumpa mabusu Bw. Manji kama ishara ya shukrani na furaha.

Luteni Makamba ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo, baada ya kuvutiwa na mwamko wa wakazi wa eneo hilo, naye ameahidi kuchangia Sh. milioni 1.5, kati ya hizo, milioni moja ikitoka mfukoni mwake na laki tano kwenye mfuko wa ofisi yake.

’Kusema kweli umenifurahisha sana na ili kukuonyesha ni jinsi gani umenifurahisha nakuomba usogee tena hapa karibu yangu ili nikupe busu la furaha,’ akasema Mkuu huyo wa Mkoa na kisha akaanza kumimina mabusu mfululizo.

’Kutokanana na moyo wako huo unafaa kuwa mbunge wa jimbo la Kigamboni kwa tiketi ya CCM, kwa kuwa kitendo cha kukubali kufadhili miradi inayogharimu mamilioni ya fedha inaonyesha dhahiri kuwa una uchungu na maendeleo ya wananchi,’ akasema Luteni Makamba.

Akasema mkoa wa Dar es Salaam unahitaji watu wanaoguswa na maendeleo ya kijamii kama hayo na kwamba huo ukereketwa wa maendeleo alionao Bw. Manji, unaonyesha anaweza’kufiti’ ubunge wa jimbo la Kigamboni.

Akasema hilo siyo tatizo kwa kuwa jimbo hilo halina mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM.

Bw. Yusuph Manji, ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Quality Group, amekubali kushirikiana na wananchi wa kata hiyo kuchangia miradi mbalimbali.

Mfadhili huyo atafadhili utengenezaji wa barabara ya njia panda ya Nzasa hadi Kilungule ambayo ina urefu wa kilomita nne na kuweka makaravati pamoja na mifereji ya maji ya mvua kwa gharama ya Sh. milioni 72.

Bw. Manji pia atasaidia uchimbaji wa kisima cha maji katika mtaa wa machinjioni cha pampu ya mkono chenye thamani ya shilingi milioni 3.5, na kuongeza shilingi milioni 1.5 ili kukamilisha kiasi cha shilingi milioni 2.5 zilizotakiwa zichangwe na wananchi kama mchango wa nguvu za wananchi kwenye mradi wa maji unaogharimu shilingi milioni 50 unaofadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia Water Aid.

Mradi kama huo pia utatekelezwa katika mitaa ya Mianzini, Kimbangulile na Majimatitu ambapo bado michango inaendelea ili kukidhi moja ya masharti ya kuchangia asilimia 5 ya gharama za mradi.

Pia Bw. Manji, amejitolea kuwaondolea umasikini vijana wa eneo hilo ambapo atatengeneza mikokoteni 20 yenye thamani ya sh. 800,000, kwa ajili ya kuvipatia vikundi vya vijana vilivyopo kwenye kata hiyo ili kupunguza kero ya ukosefu wa ajira.

Nao wananchi wa eneo hilo wameonyesha kufurahishwa na ufadhili huo ambapo wamempongeza na kumshukuru Bw. Manji, kwa kuonyesha moyo wa ukereketwa katika suala la maendeleo.

SOURCE: Alasiri
http://www.ippmedia.com/ipp/alasiri/2005/07/21/45036.html
 
Mkandara, hili suala la dini umelileta wewe... Makamba ni Muislamu, Manji ni Muislamu, ripoti ya Bakwata ni ya Waislamu.. sasa sijui udini mimi wa nini!?
 
Mzee mwanakijiji,
Ni matokeo ya hiyo kesi na nani anapoteza. Manji ni mtu binafsi mfanya biashara na Makamba pia umetumia cheo chake, yaani hata kama majina yao yangekuwa Peter na Paul na mnyonge ni mkristu usingekuwa na maamuzi ya aina hiyo. Huna ushahidi wala kesi nzima huifahamu kuweza kubeza upande wenye makosa.
Tunawazungumzia viongozi wetu kwa kuangalia maamuzi yao pale haki inapotakiwa bila kujali dini, kabila ama rangi. Marais wetu wa kiafrika wote washenzi lakini hatuangalii wao kwa rangi zao kuwa kielelezo cha madai yetu ya rushwa na ukandamizaji bali vitendo vyao kwa kundi la watu (watanzania). Mtu yeyote anayewatetea viongozi wetu lazima kuna yale anayofurahia ktk matokeo ya maonezi hayo na sio kufuata haki.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom