Renatus Mkinga; jiandae kuchukua jimbo, unafaa sana!

Ok, ni nakubaliana nanyi kuwa alishindwa katika uchaguzi wa ndani ya chama cha magamba kule songea. Tuelewe kuwa siku zote magamba wanayapenda makapi kuliko cream!
Kitu kingine amabacho tunapashwa kufahamu kuhusu huyu mzee ni namna alivyojitambulisha kwa Watanzania, sampuli ya watu kama yeye ni vigumu mno kuishi na magamba au kupenya katika nafasi za uongozi!
Kwa tabia zake, weledi wake, hulka yake ni TRADE MARK ya Chadema, hili tulikubali waungwana, mawazo yake yanatakiwa ayatoe katika mfumo sahihi wa kisheria ambao ni bunge, naam CHADEMA watakuwa wameongeza ufito mwingine wa kuwararia magamba!
 
Binafsi namkubali sana huyu mzeehasa anapolidadavua shilika la tanesco jinsi lilivyobeeteka na serikali yake kusubiri mvua inyeshe mabwa yajae
 
Jimbo lolote ndani ya jiji la Dar huyo bwana anaweza kuchukua kwa kutumia hoja tu bila kuhonga wapiga kura, tafuteni Mbunge feki yeyote wa CCM ndani ya jiji ili ang'olewe na Mkinga
kwani kuna ambaye
sio fake kweli kwa magamba??
 
ni vizuri tukapata contact zake na kumpa ushauri wa bure!ubunge kwa ccm asahau!ccm haiuziki bila rushwa kwa wazee
 
Anatokea Peramiho, alitaka kugombea ili kumuondoa Prof. Mbilinyi alivyogombea Jenesta Mhagama akatoa jina lake, lakini ni CCM mjamaa anayependa haki penye haki.
Pesa za Voda hakuna haja ya kujadili humu maana ni sawa na pesa ambazo kila mtu anazo hazitolewi matumizi JF.
Ndivyo nimjuavyo Bwn. Renatus Mkinga.
 
kumbe ni kada wa magamba, hapo ndo tatizo lilipo..vinginevyo Mkinga ana uwezo mkubwa wa kujenga hoja na kukosoa pahala muafaka. nasema ni tatizo kwa sababu chama alichopo kwa sasa hakina uthubutu wa kumpa mtu ka yeye nafasi ni bora wawape waimbaji au machizi wa kuzaliwa-lusinde.
 
Huyu mzee ni kichwa tatizo mh!
kunasiku nilikuta ndani ya bus ooh balaaa!
 
Hata kama alikosa mvuto bado ana nafasi y akugombea tena n akuibuka mshindi wa jimbo la Songea Mjini.kuvunjika kwa koleo sio mwisho wa uhunzi. Jamaa anafaa sana huyu jamaa na anjua kujenga na kutetea hoja zake. Nenda Mkinga nenda. Sisi wana JF tuta kusaport kwa hali na mali. Mwaka2015 is mbali na chochote kianaweza kutokea hapa katikati.
 
jana usiku katika kipindi cha malumbano ya hoja kinachorushwa na itv, mwanaharakati na mzalendo wa ukweli ndg renatusi mkinga aliendelea kudhihirisha na kuonyesha uwezo katika kujenga hoja zenye uzalendo na ukombozi kwa nchi yake.
Si jana tu, ndg renatusi mkinga ni maranyingi kwa muda wa miaka mingi amekuwa akiwajambisha magamba kwa hoja zake mara apatapo nafasi ya kufanya hivyo! Mengi yanaweza kusemwa kuhusu yeye, lakini lililo kubwa zaidi ni kumuomba aanze kufanya maandalizi ya mapema katika harakati za kuingia mjengoni mwaka 2015. Huyu jamaa nina aminim kuwa kama atafanikiwa kuingia pale basi magamba watamkoma!
Nakumbuka lisu kabla hajawa mbunge, naye alikuwa kama huyu mzee mkinga, nionavyo mimi mawazo yake yatakuwa na maana zaidi iwapo atayatoa katika mfumo sahihi unaotambuliwa kisheria( bunge) kuliko huko aliko kwani magamba wanamuona mpayukaji.
Renatusi kama unachungulia humu jf naomba uyachukue na kuyapima mawazo yangu juu yako then yafanyie kazi ikibidi.

aaah hili jembe nalikubali kweli tulitafutie jimbo kabisaa
 
Huyu mzee nim mwenyeji wa mkoa Ruvuma, lakini kwa Tanzania yetu ambayo haina ukanda wala ukabila anaweza kugombea jimbo lolote lile maadamu anakubalika, na yeye ana-deserve kugombea jimbo lolote kwa namna alivyojitambulisha katika jamii. Mi nashauri aende Songea mjini au aende kinondoni akamung'oe Azan.
Habari za milioni 100 hapa sio mahali pake, siku zote tunashauri ukikosa hoja kaa kimya, huu ni uwanja wa tafakuri shadidi sio utani wa kitoto unaopwelea!

songea mjini hatutaki wabunge wazee na siasa za kupayuka..Vijana wengi wanajiandaa Songea mjini na wanamvuto.Kila la kher Mkinga kwa mengine.
 
Agombee kwa ticket ya chama cha mapinduzi. Atafaa sana kuibana serikali ya chadema 2015 na kwendelea
 
Jimbo lolote ndani ya jiji la Dar huyo bwana anaweza kuchukua kwa kutumia hoja tu bila kuhonga wapiga kura, tafuteni Mbunge feki yeyote wa CCM ndani ya jiji ili ang'olewe na Mkinga
Kwani yeye kasema yuko chma gani?
 
Siku zote faida ya mapungufu ni hitimisho bwana mkinga kwa mda mrefu amekuwa akitoa mapungufu ya serikali lakini wahusika hawajirekebishi ndo maana mtoa mada ameona akiingia mjengoni ndo itakuwa sehemu pakee ya mawazo yake kufanyiwa kazi
anatoka ruvuma huyo, ila kwani kila mtu anayepinga utendaji wa serikali lazima agombee ubunge? Aendelee kuwa mkosoaji hivyo hivyo!
 
Mi nadhani CHADEMA wafanye kitu na Mkinga kufanya replacement ya Shibuda.

no,no! Soon hapo segerea patakuwa bila mbunge. Yule mwizi wa kura, Makongoro Mahanga hawezi kupona,kwa ushahidi uliotolewa. Asimame pale kupitia CDM. Kwa kuwa ni mjini,taarifa zinawafikia watu kwa urahisi tofauti na akienda mkoani. Namkubali!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom