Remote control inaitwaje?

Rodwell mTZ

JF-Expert Member
Nov 16, 2012
1,309
1,423
Hamjambo wana JF wenzangu? nina swali naomba kuuliza kama televisioni huitwa runinga kwa kiswahili na decoder huitwa king'amuzi,hivi remote control inaitwaje kwa lugha ya kiswahili ?
 
google translator wanaitafsiri kama kudhibiti kijiji.

hilo neno lenyewe la kingereza halijakaa vizuri, linahitaji neno moja la kiswahili
 
Nashukuru wadau kwa majibu yenu,ila kuhusu hili watu wa BAKWATA wana kazi ya ziada kuliweka neno la kiswahili kwa ajili ya kifaa hichi "remote control" na vifaa vingine amcvyo bado havijapatiwa maneno ya kiswahili.
 
kiswahili hakina utajiri wa maneno kama kilivyo kiingereza, so kuna maneno ya kiingereza tafsiri yake ya kiswahili hulandana na matamshi vile vile ili mradi maana isipotee mfano hiyo remote kwa kiswahili inaitwa Rimoti. au neno Radio kwa kiswahili inaitwa Redio.
 
Nashukuru wadau kwa majibu yenu,ila kuhusu hili watu wa BAKWATA wana kazi ya ziada kuliweka neno la kiswahili kwa ajili ya kifaa hichi "remote control" na vifaa vingine amcvyo bado havijapatiwa maneno ya kiswahili.
Mkuu umeniacha hoi sana, "BAKWATA" sasa hapo wameingiaje? Au ulitaka kusema"BAKITA".
 
Nashukuru wadau kwa majibu yenu,ila kuhusu hili watu wa BAKWATA wana kazi ya ziada kuliweka neno la kiswahili kwa ajili ya kifaa hichi "remote control" na vifaa vingine amcvyo bado havijapatiwa maneno ya kiswahili.
Ninyi sio wafuatiliaji wazuri wa lugha yetu pendwa.Kamusi ya kiswahili karne ya 21 inatafsiri hilo neno kama nilivyo kwambia hapo juu kisengeletua

mafisadi hayana rangi

Back
Top Bottom