Reminiscence/travelling Down Memory Lane Forum

Ibambasi

JF-Expert Member
Jul 25, 2007
9,261
4,669
Ndugu wanaJF na administrators,heshimambele kwenu wakuu,

Kwa kuwa tunakaribia kuufunga kabisa mwaka 2007 kuingia 2008 na kwa kuwa nimeona kuna watu wanapenda sana kukumbushana kuhusu enzi zile zilizopita na jinsi watu walivyosota kutafuta maisha (hasa late 1970s an 1980's) nimeona ni vema nikawaomba administrators kuanzisha forum inayohusu mambo yaliyopita kwa ajili ya kuwafanya watu kukumbukia enzi hizo zilizopita (Old good days).Forum hii napenda iitwe REMINISCENCE/DOWN MEMORY LANE/ENZI ZETU.nafikiri ni vizuri pia katika forum hii kupost pia picha za watu na matukio ya enzi zile,mf. timu na wacheza soka wa enzi zile,madj's, club zilizotamba kama vile Mbowe na Rungwe hapa DSM, Mwanaisunguna Muungano Mess kule Tabora, Delux na Magnum Mwanza,etc, pia enzi z kwenda sinema kama vile, New Chox,Empire na Avalon hapa DSM, Liberty Mwanza,Majestic Tanga etc.,fasheni na mitindo ya mavazi,kuzamia meli kwa mabaharia(stoaway).Pia watu watakuwa wakishare na wenzao stori zao za kusaka maisha.

Hii itatukumbusha pia waenzetu tulikouwa nao ambao wengine wametangulia mbele ya haki.Jamani admnistrators na wanaJF naomba tujadili swala hili.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom