Remdesivir kutumika kuua virusi vya korona, nani alisema ukiua virusi mgonjwa nakufa pia na Ebola haitibiki?

Masi Lambo

JF-Expert Member
Apr 8, 2020
532
360
Uingereza kuwaruhusu baadhi ya wagonjwa wa COVID-19 wenye hali mbaya kutumia dawa ya Remdesivir
Wizara ya afya ya Uingereza imetangaza kuwa inapanga kuwaruhusu wagonjwa wa COVID-19 wenye hali mbaya wanaolingana na kigezo kutumia dawa ya kupambana na virusi ya Remdesivir, ili kuwasaidia kupona haraka zaidi.

Remdesivir ni dawa ya kupambana na virusi iliyobuniwa na kampuni ya sayansi ya Gilead ya Marekani, iliyotumiwa kutibu ugonjwa wa Ebola na MERS. Idara ya usimamizi wa chakula na dawa ya Marekani imetoa idhini ya matumizi ya haraka ikiyaruhusu mashirika ya afya ya Marekani kutumia dawa hiyo katika tiba ya wagonjwa wenye hali mbaya.

Kwa mujibu wa wizara ya afya ya Uingereza, hivi sasa nchi kadhaa duniani ikiwemo Uingereza zimefanya jaribio la wagonjwa kuhusu dawa hiyo na takwimu za jaribio la kwanza limeonesha kuwa dawa hiyo inaweza kupunguza kwa siku nne muda wa kupona kwa wagonjwa wa COVID-19
No photo description available.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom