Reli zinaminywa kwa maslahi ya wenye maroli - tufanye nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Reli zinaminywa kwa maslahi ya wenye maroli - tufanye nini?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by kichwat, Apr 21, 2012.

 1. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2012
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,824
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Wananchi na wafanyabiashara tunalia juu ya HUJUMA zinazoendelea kudhoofisha ufanisi wa reli zetu. Lakini huu sasa si wakati wa kuendelea kulia tu. Machozi yakauke, tuchukue hatua za kushinikiza urejeshwaji wa reli ili kufufua uchumi, na msongamano wa maroli barabarani.
  Usafirishaji wa reli una faida za wazi kabisa:
  1. Kupunguza gharama za usafirishaji (kupunguza bei za bidhaa na kuongeza mauzo na faida)
  2. Kuharakisha bulk transportation.
  3. Kupunguza msongamano wa magari makubwa barabarani (kupunguza ajali, kuharakisha safari za watumiaji wengine wa barabara)
  4. Kuhamasisha shughuli za uchumi, uzalishaji na ajira, ktk njia za reli
   
 2. K

  Kagalala JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2,372
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Mimi huwa nikiangalia reli zetu na kulinganisha na wenzetu machozi yananilenga. Tanzania tumeshindwa kujenga reli zaidi ya Tazara (ya mchina) na reli alizoacha Mjerumani. sisi ni kama tumelogwa. Nikiangalia network ya reli zilizo nchi kama UK huwa najiuliza sisi watanzania tuko karne ya ngapi?
   
 3. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Sasa Angola wanajenga reli yao ili mizigo ya zambia na DRC ipite uko kazi tunayo
   
 4. Laigwanan76

  Laigwanan76 JF-Expert Member

  #4
  Apr 27, 2012
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 540
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kwa kifupi WaTZ hatuko serious,hatuna mipango na utekezaji wa dhati......viongozi na wasimamizi wa shughuli za maendeleo wamegeuza nyadhifa zao mitaji ya kujilimbikizia mali.

  Bila kubadilika na kuwa na nia za dhati kwa maendeleo ya taifa hili,daima tutarudi nyuma wakti wengine wanasonga mbele,pamoja na rasilimali zote tulizonazo.
   
 5. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #5
  Apr 27, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Tanzania nchi ya vilaza wa mwisho!

  Reli tuliwapa wahindi gabachori sijui tulitegemea nini.
   
 6. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #6
  Apr 27, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Wapo Vigogo ambao hawataki nchi iendelee wao furaha yao kuona tunabaki nyuma, tunakuwa masikini, tunakosa elimu ili kipindi cha uchaguzi waje watuhonge T-Shirt zenye picha za waheshimiwa.
   
 7. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #7
  Apr 27, 2012
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Tulipata Uhuru wa bendera 1961 tukasahau kupanga mkakati wa kupigania uhuru wa kiuchumi.
  Sasa ni wakati wa kupambana kufa na kupona ili kuutwa Uhuru wa kiuchumi ili tuwe huru kweli.
  Gharama ya kupigania Uhuru wa kiuchumi ni kubwa mara 1000 zaidi ya ile ya Uhuru wa Bendera hasa kama umesubiri miaka 50 tangu upate uhuru wa bendera.
  Tujue kwamba Tutapambana na weusi wenzetu wanaodumisha Utumwa wa kiuchumi kwa kutumia Jeshi la polisi Usalama wa Taifa Fedha za umma Ikulu na hata JWTZ ili kuhakikisha kwamba Uhuru wa kiuchumi unabakia ndoto na unageuka jinamizi la kipopobawa.
   
Loading...